Picha: Siku Magufuli alivyozindua kiwanda cha Rostam Morogoro

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Hii ilikua ni February 12 mwaka 2021,na baada ya hapo hii ndo ilikua ziara yake ya mwisho kwani baada ya hapo alienda hadi Dsm mbezi kuzindua stend na ikawa ndo mwisho wa kuonekana kwake.

Nimeweka picha zote.

Rais Magufuli ampongeza Rostam Aziz kwa kuanzisha kiwanda Morogoro

Ijumaa, Februari 12, 2021

Muktasari:

Rais Magufuli amezindua Kiwanda cha Ngozi cha ACE Leather Tanzania Limited-Kihonda

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ampongeza mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz kwa kuanzisha kiwanda mkoani Morogoro.

Mbali na pongezi hizo, Magufuli amemshukia mbunge wa Morogoro Mjini Aziz Aboud kwa kushindwa kuendesha viwanda.

“Nakupongeza sana Rostam kweli nakupongeza kwa sababu rafiki yako mbunge wa hapa ameshindwa kuendesha viwanda viwili. Mimi huwa ni mkweli nazungumza kwa uwazi, Aboud alichukuwa viwanda viwili vikubwa cha Calvan na Moplo.

“Kiwanda cha Moplo kilikuwa kinahusika na mafuta ya kupikia, mimi nasema hadharani sikufichi, ulipewa viwanda tangu mwaka 1996 hadi mwaka jana walipokunyang’anya uliwanyima ajira hata wapigakura wako,” amesema Magufuli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo, Ijumaa Februari 12, 2021 wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Ngozi cha ACE Leather Tanzania Limited-Kihonda, kinachomilikiwa na Rostam.

Katika maelezo yake Rais Magufuli amesema, “huu ndiyo ukweli na mimi nitabaki siku zote kusema ukweli, nasema uongo ndugu zangu? Aliitikiwa kweli na wananchi. Abood amekaa na viwanda vya Moplo na Calvan kwa zaidi ya miaka 25.

“Huyu leo simpongezi ingawa jana nilimpongeza kwenye viwanda ndugu Abood hujafanya vizuri. Nikiondoka Morogoro sijasema hili nitakuwa mnafiki,” amesema Rais Magufuli.

Katika hafla hiyo Rais Magufuli amesema Kiwanda cha Calvan kiliuzwa kwa Benki ya CRDB, ambayo hata hivyo hawakukiendeleza, huku akimuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Geoffrey Mwambe kusimamia suala hilo na kiwanda hicho kifanye kazi.

Screenshot_20250829-234045~2.jpeg
Screenshot_20250829-234214~2.jpeg
Screenshot_20250829-234154~2.jpeg
Screenshot_20250829-234134~2.jpeg
IMG_7076.jpeg
IMG_7077.jpeg
 
Hii ilikua ni February 12 mwaka 2021,na baada ya hapo hii ndo ilikua ziara yake ya mwisho kwani baada ya hapo alienda hadi Dsm mbezi stend na ikawa ndo mwisho wa kuonekana kwake.

Nimeweka picha zote.

Rais Magufuli ampongeza Rostam Aziz kwa kuanzisha kiwanda Morogoro

Ijumaa, Februari 12, 2021

Muktasari:

Rais Magufuli amezindua Kiwanda cha Ngozi cha ACE Leather Tanzania Limited-Kihonda

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ampongeza mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz kwa kuanzisha kiwanda mkoani Morogoro.

Mbali na pongezi hizo, Magufuli amemshukia mbunge wa Morogoro Mjini Aziz Aboud kwa kushindwa kuendesha viwanda.

“Nakupongeza sana Rostam kweli nakupongeza kwa sababu rafiki yako mbunge wa hapa ameshindwa kuendesha viwanda viwili. Mimi huwa ni mkweli nazungumza kwa uwazi, Aboud alichukuwa viwanda viwili vikubwa cha Calvan na Moplo.

“Kiwanda cha Moplo kilikuwa kinahusika na mafuta ya kupikia, mimi nasema hadharani sikufichi, ulipewa viwanda tangu mwaka 1996 hadi mwaka jana walipokunyang’anya uliwanyima ajira hata wapigakura wako,” amesema Magufuli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo, Ijumaa Februari 12, 2021 wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha Ngozi cha ACE Leather Tanzania Limited-Kihonda, kinachomilikiwa na Rostam.

Katika maelezo yake Rais Magufuli amesema, “huu ndiyo ukweli na mimi nitabaki siku zote kusema ukweli, nasema uongo ndugu zangu? Aliitikiwa kweli na wananchi. Abood amekaa na viwanda vya Moplo na Calvan kwa zaidi ya miaka 25.

“Huyu leo simpongezi ingawa jana nilimpongeza kwenye viwanda ndugu Abood hujafanya vizuri. Nikiondoka Morogoro sijasema hili nitakuwa mnafiki,” amesema Rais Magufuli.

Katika hafla hiyo Rais Magufuli amesema Kiwanda cha Calvan kiliuzwa kwa Benki ya CRDB, ambayo hata hivyo hawakukiendeleza, huku akimuagiza Waziri wa Viwanda na Biashara, Geoffrey Mwambe kusimamia suala hilo na kiwanda hicho kifanye kazi.

View attachment 3458185View attachment 3458188View attachment 3458189View attachment 3458191View attachment 3458195View attachment 3458196
Kwahili nakataa. Magufuli alianza kutembea na AC na feni hata sehemu ambazo kwa mtu mwenye afya njema hapahitaji usaidizi wa hewa. Kuonesha alikuwa tayari amedhurika tazama mwonekano wale kwenye hizo picha.
 
Back
Top Bottom