PreGE2025 Picha: Tunduma yavunja rekodi ya mahudhurio kwenye mikutano ya No Reform No Election Kanda ya Nyasa

PreGE2025 Picha: Tunduma yavunja rekodi ya mahudhurio kwenye mikutano ya No Reform No Election Kanda ya Nyasa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Na hawakulazimishwa kwenda kwenye mkutano,sisi huku kujaza hivyo mpaka wananchi tuwajaze kwenye tipa na mabasi
Screenshot_2025-03-27-21-48-16-1.png
 
Hizi hekaya haziwezi kubadili chochote haziwezi kuongeza hata kura kumi siku ya uchaguzi. Kuna kundi kubwa sana la wasomi wanaoelewa CCM inafanya nini muda huu.
Wasomi wa "majalalani" ndio wanaoielewa CCM inafanya nini,lakini kwa wasomi walioelimika na kutopofushwa na vyeo, tunaona "ombwe" pale juu.
Ungewahi kuwa hata mjumbe wa seneti ya Chuo Kikuu kimoja hapa nchini, ungejua nazungumza nini!
 
Uchaguzi Uhuru hauna mwenyewe Sema CCM wanaogopa sijui kwa nini ukizoea vya kunyonga CCM chama changu uwa kinaniangusha Uogq
 
Kinachofanyika kwenye chaguzi wote huwa tunakiona, nadhani bado mnaamini wananchi ni wajinga hawajui lolote. Huenda huu uoga wa watanzania kuhusu uchafu unaofanyika kwenye chaguzi ili ccm kutangazwa washindi kwa shuruti, mnachukulia ni watu kutokujua ukweli, ama kuridhika na ushenzi huo.
Yanafanyika mengi sana huko huko kwa hao wananchi hawahitaji kudanganywa na siasa za wizi wa kura.

Uibe kura kwa sababu gani wakati asilimia 80 ya TZ inawaka umeme na barabara zinaendelea kujengwa.

Uibe kura kwa sababu gani wakati vivuko vimejengwa na madaraja yanamaliziwa?.

Uibe kura kwa sababu zipi wakati kodi inakusanywa kitaalam na kazi yake inaendelea kuonekana kwenye maisha ya watu wa kawaida?.

Malalamiko ya wizi wa kura ni humu mitandaoni, huko kwa mwananchi wa kawaida yanafanyika mengi sana yenye kuhalalisha kura zote zinazopigwa.
 
Wasomi wa "majalalani" ndio wanaoielewa CCM inafanya nini,lakini kwa wasomi walioelimika na kutopofushwa na vyeo, tunaona "ombwe" pale juu.
Ungewahi kuwa hata mjumbe wa seneti ya Chuo Kikuu kimoja hapa nchini, ungejua nazungumza nini!
Ujumbe wa seneti ya chuo kimoja haulingani na namna kodi inayokusanywa inavyojenga madaraja na barabara kila kona ya nchi hii.

Ujumbe wa seneti ni kitu kidogo sana kulinganisha na namna wakulima wa mahindi wanavyoendelea kuyauza kwa majirani zetu kila kukicha.

Hakuna haja ya kuiba kura ikiwa viwanja vya ndege vinavyofunguliwa vinawezesha wakulima kuuza mazao yao moja kwa moja huko Ulaya na Asia.

Hizi riwaya za chuki mwisho wake ni humu humu JF.
 
Acha ujinga basi, watu walalamika uchaguzi kuchakachuliwa wewe unaleta ngonjera gani hapa? Usitufanye wajinga bwana
Uchakachue uchaguzi kwa sababu zipi wakati katika kipindi cha miaka mitano CCM ipo kazini ikitekeleza ilani zake kwa hao hao wananchi?. Punguza hayo malalamiko ya jumla jumla, yanakwenda yakipoteza mantiki.
 
EL ndo alishinda, sema wizi ulipindua uhalisia
EL alikuwa bingwa wa propaganda, na huo mchezo alijifunzia CCM hivyo asingeweza kushinda kwa ujanja ambao mshindani wake ndio aliyemfundisha.

JK alivyofanya mabadiliko kwenye tume ya uchaguzi siku chache kabla ya uchaguzi akawa amemmaliza EL.
 
Yanafanyika mengi sana huko huko kwa hao wananchi hawahitaji kudanganywa na siasa za wizi wa kura.

Uibe kura kwa sababu gani wakati asilimia 80 ya TZ inawaka umeme na barabara zinaendelea kujengwa.

Uibe kura kwa sababu gani wakati vivuko vimejengwa na madaraja yanamaliziwa?.

Uibe kura kwa sababu zipi wakati kodi inakusanywa kitaalam na kazi yake inaendelea kuonekana kwenye maisha ya watu wa kawaida?.

Malalamiko ya wizi wa kura ni humu mitandaoni, huko kwa mwananchi wa kawaida yanafanyika mengi sana yenye kuhalalisha kura zote zinazopigwa.
Kama umeme kuwaka kunakupa kura, mbona makaburu wa africa kusini hawakupata? Hizo nchi nyingine umeme unakowaka mbona vyama tawala vimeshindwa?
 
EL alikuwa bingwa wa propaganda, na huo mchezo alijifunzia CCM hivyo asingeweza kushinda kwa ujanja ambao mshindani wake ndio aliyemfundisha.

JK alivyofanya mabadiliko kwenye tume ya uchaguzi siku chache kabla ya uchaguzi akawa amemmaliza EL.
Duh 🙄
 
Back
Top Bottom