Picha: Wafuatao ni samaki tunaowapata sana hasa ukanda huu wa Lindi beach

Picha: Wafuatao ni samaki tunaowapata sana hasa ukanda huu wa Lindi beach

Samaki wa baharini huwa siwapendi Mimi ukinipa samaki wa maji baridi sato ama perege!
Naona wako poa
Watu mliokulia mikoani hii ndio kauli yenu most of the time. Kimsingi hamjui ladha ya samaki wa baharini kuwa ndio ladha ya samaki mwenye virutubisho vingi zaidi kuliko samaki wa kawaida wa maji baridi ambaye hana nutritional value ya juu ukifananisha na samaki wa baharini.
 
Watu mliokulia mikoani hii ndio kauli yenu most of the time. Kimsingi hamjui ladha ya samaki wa baharini kuwa ndio ladha ya samaki mwenye virutubisho vingi zaidi kuliko samaki wa kawaida wa maji baridi ambaye hana nutritional value ya juu ukifananisha na samaki wa baharini.
Ndio hivyo mkuu ila Mimi nimesema kile ni kipendacho,hayo mengine siyajui ila pia Asante kwa comment yako!
 
Mnaoishi bara Poleni sio kidogo endeleeni kutunyima protein ya nyamaPori, senene na kumbikumbi. Tunaokaa pwani ya Bahari Hindi tunaendelea kufaidi sea food.
Kibua-huyu najua maarufu sana hasa Kwa dar
Changu-huyu Lindi na Mtwara Kwa wingi
Lupapa
Chewa - huyu wa supu kabisa moja ya samaki mwenye bei nzuri watoto wa kivinje na Mchinga wanaelewa
Kipepeo - huyu hata mimi mwenyewe Sina maelezo yake mengi sana sijawahi kumla
Pronzi sijui nimwite bronzi - jamii ya kambakochi na mwenyewe wakubwa bei yake nzuri
Dagaa mchele-wa buku waliokaangwa unakula na ugali na maji ya baridi
Kolekole-kilwa na somanga Safi Sana
Ngisi - mtoa wino huyu na pweza unamkubali yupi?
Kiatu - huyu samaki Kiatu hana nyama nyama chembamba

WOTE WAKO PICHANI HAPO
View attachment 3000382
View attachment 3000381
Mkuu hao dagaa kamba wanauzajerhuko
 
Sasa ukisema Sea food si ndio maana ya kusema samaki wa baharini au wewe unajua Sea food ni wali maharage? [emoji23][emoji23][emoji23]

Sea food sio samaki pekee yake
1.kaa ni mdudu lakini ni seafood
2.kome/makome ni jamii ya konokono
3.mwani ni majani ya baharini yanalimwa ufukweni
 
Kuna siku nilichemsha supu ya kolekole( fillet)+ngisi+ukwaju mbichi, huwa napendaga tu kula hasa mida ya jioni, ila Ile siku nilikuwa na wageni wawili..kilichotokea dah.
 
Na sisi tunaokula samaki wa Mto Kilombero pamoja na vile vijito vyake vidogo vidogo, tusiwe wanyonge! Tuje na sisi tusifie samaki wetu bhana! Kuanzia Kambale, Kitoga, Mkunga, ndipi, njuju, perege, ngogo, mlamu kalia ndili, , nk.

Tena kama hao mlamu kaliandili na huu msimu wa ubwabwa mpya!! 😋 Aisee shughuli yake si mchezo.
 
Jongoo bahari tu bei yake imesimama kuliko sato!

Wengi hawamli jongoo bahari lakini jiulize bei yake ni kubwa mno mno... katika soko la Dunia ndio balaa

Sato sijui anashindana bei
Misamaki yenu sio mitamu
 
Back
Top Bottom