Kumekuwepo na picha inayozunguka mitandaoni ikimuonesha mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akizungumza na Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho huku mandhari ya nyuma ya picha hiyo yakiwa na picha yenye chupa ya konyagi.
Picha inayodaiwa kuwa na chupa ya Konyagi
Ukweli wa picha hii upoje?
Picha 1 kati ya 4 zilizowekwa na Tundu Lissu kwenye mtandao wa Twitter
Picha inayodaiwa kuwa na chupa ya Konyagi
Ukweli wa picha hii upoje?
Picha 1 kati ya 4 zilizowekwa na Tundu Lissu kwenye mtandao wa Twitter
- Tunachokijua
- Februari 1, 2023, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu A. Lissu aliweka picha nne kwenye Mtandao wa Twitter zikiambatana na ujumbe unaosema “Reconnecting with Chairman Mbowe after years of enforced separation” baada ya kutokuwa pamoja tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Ukizitazama picha hizi halisi, hakuna hata moja yenye Chupa ya konyagi kama baadhi ya watu wanavyodai.
Hivyo, kwa kutumia ushahidi huu, picha yenye Chupa ya Konyagi siyo halisi na haina ukweli wowote.
Chupa ya konyagi inayoonekana kwenye picha ni istizahi inayofanywa na wapinzani wa Mbowe ambao wanaamini maneno yaliyosemwa Bungeni miaka kadhaa iliyopita kuwa tukio la yeye kuanguka kwenye ngazi lilisababishwa na ulevi wa konyagi.