Kumekuwa na picha inayomuonesha kijana amegongwa misumari mikononi huku picha hiyo ikiwa inahusishwa na matukio mbalimbali likiwemo matukio ya fumanizi (Tazama
hapa, hapa, hapa na
hapa)
Uhalisia wa Picha ni upi?
JamiiiCheck imefuatilia picha hiyo na kubaini ni picha halisi na Si ya kutengenezwa au kuhaririwa. Ufuatiliaji wa kimtandao kupitia Google Reverse Image umebainisha tukio hilo liliwekwa
mtandaoni mara ya kwanza Agosti 29, 2019. (Tazama
hapa hapa hapa na
hapa)
Moja ya watu waliochapisha tukio hilo siku ya Agosti 29 2019 ni mwanaharakati na kiongozi wa Chama Cha National Unity Platform (NUP),
Bobi Wine alieleza kuwa kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Kasumba Baker aliyekuwa na umri wa miaka 21 alivamiwa na watu 2 wasiojulikana ambao walimpiga kichwani pamoja na kumgongelea misumari mikononi.
Aidha tukio hilo
lilichapishwa na New Vision tarehe 29, Agosti 2019 ambao walieleza kuwa kijana Kasumba baker(21) alivamiwa na watu wawili ambao hawakujulikana, siku ya Agosti 25, 2019 alipokuwa anatoka kazini kwake ambao walimpiga kichwani na kumgonga misumari mikononi, wanaeleza kuwa Kasumba alikuwa mkazi wa Avis Kivvulu Nchini Uganda. Baada ya tukio hilo alilazwa Mulago Hospitali kupatiwa matibabu huku Polisi walidai kufanyia
uchunguzi ili kuwabaini wahusika waliotekeleza tukio hilo.
Kwa mujibu wa BBC ambao
walichapisha taarifa hiyo tarehe 30, Agosti 2019 walieleza kuwa tukio hilo lilizua
mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wakilihusisha tukio hilo na Siasa za nchini Uganda.