Picha ya mafuriko chuo cha CBE, aliyejenga chuo awajibishwe

Pia mbona hata stendi ya Gold Star Kariakoo kwa magari yanayotokea Gongo La Mboto huwa panajaa sana maji na mighorofa kama yote tu imejaa pale?

Hapo vipi?
 
Mainjijia watafanya nini kama mmejenga baharini bwashee
Bahari huwa inahamishwa, D'Salaam basically ilikuwa ni swamp ilikuwa na mashamba ya mpunga back then when it was still a fishing village lakini haimaanishi hawawezi kujenga drainage system ya maji kuwa hayatuami. It's a very costly project but if there is a will it can be done.
 
Mleta mada hicho chuo kimejengwa jana? Je miundombinu inaendana na uhitaji kwa sasa? Je ni hapo tu ndio panafurika?
Unaposema awajibishwe je kama ni uzembe wa watumiaji kutozibua chemba kwa wakati. Umewaza hayo yite au umekuja kubwabwaja tu hapa
 
It's easier to bulldoze all the buildings erected on the main waterways.
Nimekulia Dar na nimesoma Forodhani na tanganyika library nimeitumia tangu utotoni hakuna mvua iliyokuwa inatuama mjini. Hakukuwa kitu kama hicho, huo ni mkondo wa maji uliozuiwa na ujenzi holela.
Ikiamriwa bulldozer mnapiga kelele mpaka benki ya Dunia.
 
Serikali yote iwajibishwe kwa kuachia watu wangawa viwanja holela bila kuangalia vyanzo vya maji na mikondo

Huo mji ni hatari kwa kila kitu
 
Huyu kweli lni azima atawajibishwa. Yaani pale CBE Mkuu wa Chuo ni Profesa mmoja smart sana halafu amenyooka kuzidi hata rula. Kwa ubabaishaji huu, namhurumia mtu fulani mahali fulani
 
Hii serikali inafanya kazi kwa kutegeana, kuna watu wamegoma kabisa kufanya majukumu yao. Wakati mabwawa yamekauka tulihangaika na umeme, sasa mabwawa yamejaa kwa mvua tunahangaika na mafuriko. Inasikitisha kwa kweli kwa sababu bahari ipo mita 500 tu kwa nini kuwe na mafuriko katikati ya jiji?

Yaani hata kuzibua mitaro ya kupeleka maji baharini hadi waje wawekezaji ?
 
Mkuu kwani contract ya ujenzi wa chuo ilihusisha na miundombinu ya kupeleka maji baharini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…