Picha ya mafuriko chuo cha CBE, aliyejenga chuo awajibishwe

Picha ya mafuriko chuo cha CBE, aliyejenga chuo awajibishwe

Mvua ya masaa tu chuo kimekuwa mto, aliyejenga hapa atafutwe awajibishwe. Mambo ya hovyo sana haya, hakukuwa na upembuzi yakinifu.

Leo watu wamehailisha mitihani Dar es Salaam Campus kisa chuo kujaa maji.

USSR View attachment 2511702
View attachment 2511704
Kama.barabara zinajengwa Bila mitaro ya kuchukua Maji unatarajia nini? Dar salaam wanajua kujenga maghorofa marefu lakini barabara pembeni hazina mitaro. Jana hapo post nguma ya morogoro road kuazia kituo cha kisutu kupanda juu kulikua hakupitiki barabara zimejaa maji. Ila pembeni kuna majengo marefu yamejaa nakshi.hadi paani. Poor dar es salaam.
 
Hii serikali inafanya kazi kwa kutegeana, kuna watu wamegoma kabisa kufanya majukumu yao. Wakati mabwawa yamekauka tulihangaika na umeme, sasa mabwawa yamejaa kwa mvua tunahangaika na mafuriko. Inasikitisha kwa kweli kwa sababu bahari ipo mita 500 tu kwa nini kuwe na mafuriko katikati ya jiji?

Yaani hata kuzibua mitaro ya kupeleka maji baharini hadi waje wawekezaji ?
Tuko busy kupeana PhD za heshima mkuu.
 
It's easier to bulldoze all the buildings erected on the main waterways.
Nimekulia Dar na nimesoma Forodhani na tanganyika library nimeitumia tangu utotoni hakuna mvua iliyokuwa inatuama mjini. Hakukuwa kitu kama hicho, huo ni mkondo wa maji uliozuiwa na ujenzi holela.
Ikiamriwa bulldozer mnapiga kelele mpaka benki ya Dunia.
Nimesoma Upanga primary, O-Level Fodhani zamani sana. Ni mtu mzima hapa, tulitumia libraries za British Council, Tanganyika library na USIS(in the eighties) na ni kweli mafuriko yamekuwa mengi zaidi ya ilivyokuwa back in the day(literally miaka hiyo hakukuwa na mafuriko CBD area) lakini ukiishi ughaibuni unaona mifumo ya drainage inavyojengwa na inavyofanya kazi. Dar(town center na maeneo yote ambayo huwa yanafurika) inawezekana sana kujenga mifumo ya drainage itakayo kabili mafuriko, it takes a will and a lot of money. Ni kitu kinachowezekana kabisa, kukwepwa gharama za kujenga hiyo mifumo ni kukaribisha aina nyingine za gharama pamoja majanga yanayoweza kusababishwa na mafuriko.
Kabla ya yote waanze na mto Msimbazi, wavunje/wabomoe structures zote(hadi jengo la klabu yangu ya Wananchi) wautanue, wauchimbe uwe na kina kirefu maeneo yote ya jirani yajenge systems za kumwaga maji mto Msimbazi hiyo iwe ni phase one kwani ndiyo rahisi somehow. Phase two ndiyo iwe ya underground systems kwa CBD area kwa maana ya maeneo ya Posta na surrounding areas, it can be done.
 
Woooow! Mpaka Raha yani uyo Photographer ni Mtata.
 
Back
Top Bottom