Picha ya Marlyn Monroe yavunja rekodi, yauzwa kwa Bilioni 450. Je, huyu mwanadada alikuwa na kipi cha ziada?

Picha ya Marlyn Monroe yavunja rekodi, yauzwa kwa Bilioni 450. Je, huyu mwanadada alikuwa na kipi cha ziada?

New York,Marekani.

Picha ya mwanadada Marlyn Monroe iliyopigwa mnada hapo jana imevunja rekodi kwa kununuliwa kwa dola za kimarekani milioni 195($195 Mil) ambazo ni sawa na Shilingi Bilioni 450 za Kitanzania.

Picha hii pia imevunja rekodi ya kuwa ndio picha ya gharama zaidi kwa picha zilizochorwa katika karne ya 20.

Picha hii ilichorwa na mchoraji Andy Warhol mwaka 1964 ilinunuliwa na Bwana Mary Gagosian katika mnada ambao ulichukua chini ya dakika nne tu.

Marilyn Monroe alizaliwa June 1,1926 na alifariki August 4,1962 akiwa na miaka 36.

Je huyu dada alikuwa na kitu gani cha ziada kiasi cha picha yake kuuzwa ghali namna hii?

Kwa kadri nilivyomsoma inasemekana alikuwa mwigizaji,model na sex symbol(mtanisaidia hapa) na pia inasemekana aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Raisi John F Kennedy na ndugu yake Robert F Kennedy,Je kuna mengine unayajua kuhusu huyu mwanadada?.

Picha ya kwanza ndio iliyovunja rekodi.

Ahsante.View attachment 2218974View attachment 2218975View attachment 2218979View attachment 2218981
she is real beautiful 🤍
 
Wazungu hutowaweza, utasikia sjui paka wa maiko jaksoni, sijui kitamba cha supastaa gani alilia akafutia machoz msiba wa mkewe, yaani ni mambo ya kiwaki waki kinoma.
[emoji3][emoji3],hivi na sisi hatuwezi kujipaisha tukajipa thamani?Mfano tukasema ile fimbo ya Mwalimu Nyerere tukaipa mastori ya ajabu halafu tukatua nayo pale New York kama royal tour hivi tukamwambia Rostam ajifanye kama mnunuzi ataje dau kubwa kinoma ili waanze kupandia dau,wakati mwingine na sisi tunalala sana.
 
Labda kuna kitu wanatuficha ila hio picha hata sebuleni kwangu siitundiki
Inashangaza sana,japo Picha zenye gharama za juu huwa ni za kawaida tu nadhani labda story behind hio picha au uzushi uliowekwa na ndio hupaisha thamani ya kitu
 
Mabeberu Yanajifagilia Sana
Kweli nasisi tuige tu hakuna namna,mfano jino la Mkwawa hadithi yake ina maajabu sana tungeipamba halafu tukaliuze kwa bei chafu
 
[emoji3][emoji3],hivi na sisi hatuwezi kujipaisha tukajipa thamani?Mfano tukasema ile fimbo ya Mwalimu Nyerere tukaipa mastori ya ajabu halafu tukatua nayo pale New York kama royal tour hivi tukamwambia Rostam ajifanye kama mnunuzi ataje dau kubwa kinoma ili waanze kupandia dau,wakati mwingine na sisi tunalala sana.
Itabidi tupige propaganda za viwango vya ISO kabisa [emoji23]
 
Kuna vitu huwa siwaelewi wazungu, hasa ninaposoma novel zao...utakuta matajiri wanaenda kwenye gallery wanashindana kununua mchoro...let say wa mti...sijui umekatwa Tawi moja, wananunua Kwa mabilioni ya pesa...
Sijui hata wanapataga Raha gani...!!
Naona sasa hata Kwa maisha halisi wanafanya pia.
Wenzetu wako tofauti sana
 
I was just watching a new Marilyn Monroe documentary "The Mystery of Marilyn Monroe: The Unheard Tapes" on Netflix this past weekend.

Yani haya maisha yanavyoenda sasa hivi inawezekana watu wameamua kum pump Marilyn Monroe kuuza vitu vyao.

Inawezekana pia ni genuine nostalgia.


Unaonekana ni msomi mkubwa wa mambo ya physics au astronomy. Bisha..?!
 
Usishangae sana,
Sisi waafrika wananunua kamba ya mtu aliyejinyonga,
Maji ya maiti,nyuzi za sanda.
Yaani basi tu dunia uwanja wa fujo, wenye kujua zaidi ya maana ndo hugharamikia kununua wavitakavyo,ndio maana wewe unajiuliza picha tu ina nn cha ziada,aliyenunua ndio anajua zaidi.
Ni kweli,Kuna kipindi fulani huko Tabora ilianguka basi likaua watu wengi,sasa pale eneo la ajali palimwagika damu nyingi,siku walipolitoa tu lile basi ule udongo wa pale ulichimbwa na wananchi mpaka kukabaki mashimo,ule udongo wote wenye damu ukachukuliwa,sijui walienda kufanyia nini.
 
Unaonekana ni msomi mkubwa wa mambo ya physics au astronomy. Bisha..?!
Nabisha.

Mimi si msomi mkubwa wa mambo hayo, ni msomi wa kawaida.

Ila, katika jamii yetu hakuna wasomi wakubwa wengi wa mambo hayo, hata msomi wa kawaida anaonekana msomi mkubwa.
 
Back
Top Bottom