Pre GE2025 Picha ya Samia kwenye mitungi ya gesi ni ya nini? Haya ndio mambo CHADEMA wanapinga. Msimamizi wa vyama vya siasa yupo kama kipofu na kiziwi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu,

Kama lengo ni kuwatoa wananchi kutoka kutumia kuni na wahamie kwenye nishati safi, picha ya Samia inafanya nini kwenye mitungi hiyo?

Picha ya Samia ipo kwenye mitungi sababu yeye ndio mtengenezaji wa mitungi hiyo? Au kampuni yake ndio inafanya usambazaji? Yeye ndio kanunua mitungi hiyo kwa pesa yake mfukoni? Yaani pointi ni nini kuweke sura yake hapo?

Msimamizi wa vyama vya siasa kazi yako ni nini? Au majukumu yako yanaishia kwa wapinzani pekee? CCM wanaenda kinyume na sheria left and right lakini kimyaaa mmeufyata. Halafu mnashangaa CHADEMA kutaka mabadiliko ya sheria, sheria ambazo hata mtoto anaona aibu kwa yanayofanyika!

Chawa ndio mmeona hii ndio njia bora kabisa ya kumfanya mama apendwe baada ya njia zote kubuma? :BearLaugh: :BearLaugh: :BearLaugh:

Bado moja haisomi wala mbili haisimami?:BearLaugh::BearLaugh::KEKLaugh:

Ni shida sana kuwa na washauri ambao kichwani ni poda... kila siku ni kuaibika tu:BearLaugh::BearLaugh:
Ccm daima Samia mitano
 
Tungeanza kuhoji picha ya Samia ilipowekwa kwenye bendera ya taifa, lakini pia kwa taarifa yako zipo unifomu za bodaboda zenye picha ya Samia zinaandaliwa, hii ni sehemu ya kampeni ya urais.
 
Wakuu,

Kama lengo ni kuwatoa wananchi kutoka kutumia kuni na wahamie kwenye nishati safi, picha ya Samia inafanya nini kwenye mitungi hiyo?

Picha ya Samia ipo kwenye mitungi sababu yeye ndio mtengenezaji wa mitungi hiyo? Au kampuni yake ndio inafanya usambazaji? Yeye ndio kanunua mitungi hiyo kwa pesa yake mfukoni? Yaani pointi ni nini kuweke sura yake hapo?

Msimamizi wa vyama vya siasa kazi yako ni nini? Au majukumu yako yanaishia kwa wapinzani pekee? CCM wanaenda kinyume na sheria left and right lakini kimyaaa mmeufyata. Halafu mnashangaa CHADEMA kutaka mabadiliko ya sheria, sheria ambazo hata mtoto anaona aibu kwa yanayofanyika!

Chawa ndio mmeona hii ndio njia bora kabisa ya kumfanya mama apendwe baada ya njia zote kubuma? :BearLaugh: :BearLaugh: :BearLaugh:

Bado moja haisomi wala mbili haisimami?:BearLaugh::BearLaugh::KEKLaugh:

Ni shida sana kuwa na washauri ambao kichwani ni poda... kila siku ni kuaibika tu:BearLaugh::BearLaugh:
Nikiukuta nyumbani kwangu (ijapo najua haiwezekani kupelekwa pale kwakuwa mimi ninatumia akili yangu vizuri) nitaulipua kiasi kwamba mpaka hilo li-chuma lote litaungua.
 
Wananchi wa Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini mwa Tanzania wameeleza kukerwa na mitungi ya gesi yenye picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, wakisema inashawishiwa na rushwa katika mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Wanasisitiza kuwa picha hizi ni alama ya juhudi za kisiasa za kumtangaza Rais Samia, ambaye wanadai hakubaliki miongoni mwao.

Wakazi hawa wamesema kuwa, licha ya jitihada za kuhamasisha matumizi ya gesi ya kupikia, mitungi hiyo inakuja na malengo yasiyo ya kweli.

Wanaonyesha wasiwasi kuhusu utata wa kisiasa unaohusiana na matumizi ya mitungi hiyo.

Wengi wanasema kuwa ni vigumu kuelewa ni kwa nini serikali inatumia rasilimali hizi kujaribu kuimarisha picha ya kiongozi, wakati matatizo makubwa kama umaskini, ukosefu wa ajira na huduma duni za jamii yanayowakabili wananchi hayapatiwi kipaumbele.

Maswali mengi yanaibuka kutoka kwa wananchi kuhusu mustakabali wa mitungi hiyo ya gesi.

Wanauliza, ikiwa mitungi hiyo itakamilika, ni nani atakayewajazia gesi, hasa wanapokosa uwezo wa kifedha wa kununua.

Hali hii inadhihirisha ukosefu wa mipango ya muda mrefu ya kuhakikisha upatikanaji wa nishati hii muhimu.

Wananchi hawa wanashindwa kuona mantiki ya kupokea mitungi ya gesi wakati hakuna uhakika wa kuweza kuendelea kutumia gesi hiyo kwa sababu ya hali yao ya kiuchumi.

Wakati huo huo, wananchi wanasisitiza kuwa mitungi ya gesi si kipaumbele chao. Wana matatizo mengi yanayohitaji umakini, kama vile huduma za afya, elimu, na miundombinu.

Mtu mmoja alieleza, "Kwa nini tunpewe mitungi ya gesi wakati hatuna chakula mezani? Tunahitaji msaada wa dharura katika nyanja za msingi za maisha yetu."

Wakazi hawa wanajitahidi kuelewa ni kwa nini serikali inatumia rasilimali za umma kwa ajili ya kampeni za kisiasa badala ya kutatua matatizo halisi yanayowakabili.

Wanajua kuwa mitungi hiyo ni sehemu ya mkakati wa kisiasa wa kufanikisha malengo ya Rais, lakini wanataka viongozi wao wazingatie masuala ya msingi yanayohitaji uangalizi wa haraka.

Mitungi hiyo ya gesi imekuwa ikikumbwa na malalamiko kutoka kila pembe, huku wengi wakisema ni sehemu ya mbinu za kisiasa za kumwonyesha Rais Samia kama kiongozi anayejali maslahi ya wananchi.

Hata hivyo, wananchi wanabainisha kuwa si picha ya Rais inayohitajika, bali ni vitendo vinavyoweza kuboresha maisha yao ya kila siku.

Wakati wa mkutano mmoja wa jamii, wananchi walionesha hasira zao kwa kuandika mabango yanayoonesha kukataa mitungi hiyo.

Walisema, "Sisi ni wapiga kura, sio wapokeaji wa rushwa." Kauli hii ilionyesha hisia zao za kutokufurahishwa na hatua hii ya kisiasa na jinsi inavyoweza kuathiri uchaguzi ujao.

Katika hali hii, ni wazi kuwa wanahitaji kushiriki katika maamuzi yanayohusu maisha yao. Wananchi wanataka kujua ni nani anawawakilisha na ni kwa namna gani wanavyoweza kuchangia katika kupanga mipango ya maendeleo.
Wanasisitiza kuwa ni lazima viongozi wawajibike kwa mahitaji ya watu badala ya kujenga picha za kisiasa.

Miongoni mwa maoni mengine, baadhi ya wananchi walikumbusha kuwa ni muhimu kwa viongozi kuzingatia mahitaji halisi ya jamii.

Wanasema, "Tunahitaji viongozi wanaotujali na kutafuta suluhisho la kudumu, sio wale wanaotafuta umaarufu kupitia matangazo yasiyo na maana."

Kwa hivyo, mitungi ya gesi yenye picha ya Rais Samia imekuwa sehemu ya mjadala mpana wa kisiasa, huku wananchi wakipaza sauti zao kukataa mbinu hizi wanazoziona kama za kisiasa zaidi kuliko za kusaidia.

Wanataka kuona mabadiliko halisi katika maisha yao, badala ya ahadi zisizotekelezwa.
Uchawa umezidi kikomo
 
Wakuu,

Kama lengo ni kuwatoa wananchi kutoka kutumia kuni na wahamie kwenye nishati safi, picha ya Samia inafanya nini kwenye mitungi hiyo?

Picha ya Samia ipo kwenye mitungi sababu yeye ndio mtengenezaji wa mitungi hiyo? Au kampuni yake ndio inafanya usambazaji? Yeye ndio kanunua mitungi hiyo kwa pesa yake mfukoni? Yaani pointi ni nini kuweke sura yake hapo?

Msimamizi wa vyama vya siasa kazi yako ni nini? Au majukumu yako yanaishia kwa wapinzani pekee? CCM wanaenda kinyume na sheria left and right lakini kimyaaa mmeufyata. Halafu mnashangaa CHADEMA kutaka mabadiliko ya sheria, sheria ambazo hata mtoto anaona aibu kwa yanayofanyika!

Chawa ndio mmeona hii ndio njia bora kabisa ya kumfanya mama apendwe baada ya njia zote kubuma? :BearLaugh: :BearLaugh: :BearLaugh:

Bado moja haisomi wala mbili haisimami?:BearLaugh::BearLaugh::KEKLaugh:

Ni shida sana kuwa na washauri ambao kichwani ni poda... kila siku ni kuaibika tu:BearLaugh::BearLaugh:
Hivi nini kimeipata CCM?
Yaani wanawaacha watu kama Kabudi, Bashiru Ally , Mkumbo ,Mwigulu, Januari , Majaliwa, Tibaijuka , Tagamenda , Dr. Angela Kairuki n.k.
Wanatuletea mtu asiyejua hata katiba ya chama chake sembuse katiba ya nchi na sheria za mikataba ya kimataifa .
Kama katiba ka dogo kama ka vikoba hajui basi tuna hatari kubwa sana kama taifa.

Mafisadi na Mabeberu wanataka Rais asiyezijua sheria za mikataba ili aelekezwe na wazee na wapambe ndio maana wanatoa mabilioni ya pesa ili asipate hata mshindani ndani ya chama .

Hii nchi mitano tena ni hatari kuliko hatari ya enzi ya utumwa .
 
Wananchi wa Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini mwa Tanzania wameeleza kukerwa na mitungi ya gesi yenye picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, wakisema inashawishiwa na rushwa katika mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Wanasisitiza kuwa picha hizi ni alama ya juhudi za kisiasa za kumtangaza Rais Samia, ambaye wanadai hakubaliki miongoni mwao.

Wakazi hawa wamesema kuwa, licha ya jitihada za kuhamasisha matumizi ya gesi ya kupikia, mitungi hiyo inakuja na malengo yasiyo ya kweli.

Wanaonyesha wasiwasi kuhusu utata wa kisiasa unaohusiana na matumizi ya mitungi hiyo.

Wengi wanasema kuwa ni vigumu kuelewa ni kwa nini serikali inatumia rasilimali hizi kujaribu kuimarisha picha ya kiongozi, wakati matatizo makubwa kama umaskini, ukosefu wa ajira na huduma duni za jamii yanayowakabili wananchi hayapatiwi kipaumbele.

Maswali mengi yanaibuka kutoka kwa wananchi kuhusu mustakabali wa mitungi hiyo ya gesi.

Wanauliza, ikiwa mitungi hiyo itakamilika, ni nani atakayewajazia gesi, hasa wanapokosa uwezo wa kifedha wa kununua.

Hali hii inadhihirisha ukosefu wa mipango ya muda mrefu ya kuhakikisha upatikanaji wa nishati hii muhimu.

Wananchi hawa wanashindwa kuona mantiki ya kupokea mitungi ya gesi wakati hakuna uhakika wa kuweza kuendelea kutumia gesi hiyo kwa sababu ya hali yao ya kiuchumi.

Wakati huo huo, wananchi wanasisitiza kuwa mitungi ya gesi si kipaumbele chao. Wana matatizo mengi yanayohitaji umakini, kama vile huduma za afya, elimu, na miundombinu.

Mtu mmoja alieleza, "Kwa nini tunpewe mitungi ya gesi wakati hatuna chakula mezani? Tunahitaji msaada wa dharura katika nyanja za msingi za maisha yetu."

Wakazi hawa wanajitahidi kuelewa ni kwa nini serikali inatumia rasilimali za umma kwa ajili ya kampeni za kisiasa badala ya kutatua matatizo halisi yanayowakabili.

Wanajua kuwa mitungi hiyo ni sehemu ya mkakati wa kisiasa wa kufanikisha malengo ya Rais, lakini wanataka viongozi wao wazingatie masuala ya msingi yanayohitaji uangalizi wa haraka.

Mitungi hiyo ya gesi imekuwa ikikumbwa na malalamiko kutoka kila pembe, huku wengi wakisema ni sehemu ya mbinu za kisiasa za kumwonyesha Rais Samia kama kiongozi anayejali maslahi ya wananchi.

Hata hivyo, wananchi wanabainisha kuwa si picha ya Rais inayohitajika, bali ni vitendo vinavyoweza kuboresha maisha yao ya kila siku.

Wakati wa mkutano mmoja wa jamii, wananchi walionesha hasira zao kwa kuandika mabango yanayoonesha kukataa mitungi hiyo.

Walisema, "Sisi ni wapiga kura, sio wapokeaji wa rushwa." Kauli hii ilionyesha hisia zao za kutokufurahishwa na hatua hii ya kisiasa na jinsi inavyoweza kuathiri uchaguzi ujao.

Katika hali hii, ni wazi kuwa wanahitaji kushiriki katika maamuzi yanayohusu maisha yao. Wananchi wanataka kujua ni nani anawawakilisha na ni kwa namna gani wanavyoweza kuchangia katika kupanga mipango ya maendeleo.
Wanasisitiza kuwa ni lazima viongozi wawajibike kwa mahitaji ya watu badala ya kujenga picha za kisiasa.

Miongoni mwa maoni mengine, baadhi ya wananchi walikumbusha kuwa ni muhimu kwa viongozi kuzingatia mahitaji halisi ya jamii.

Wanasema, "Tunahitaji viongozi wanaotujali na kutafuta suluhisho la kudumu, sio wale wanaotafuta umaarufu kupitia matangazo yasiyo na maana."

Kwa hivyo, mitungi ya gesi yenye picha ya Rais Samia imekuwa sehemu ya mjadala mpana wa kisiasa, huku wananchi wakipaza sauti zao kukataa mbinu hizi wanazoziona kama za kisiasa zaidi kuliko za kusaidia.

Wanataka kuona mabadiliko halisi katika maisha yao, badala ya ahadi zisizotekelezwa.
Sa si wasipokee!!
 
Ni vile anajua kabisa hana ushawishi kwa hiyo anajitahidi sana kila sehemu kue na jina au picha yake kutaka kuwahadaa watu na vile wanajua udhaifu wa wapiga kura wengi ulipo basi wanacheza na gape tuu
 
Ukitekwa na na kupotezwa tutailau serikali au kalamu yako ya uandishi. Mambo mengine muwe mnakaa kimya tu! Tuko ktk kipindi kigumu mno.
woga ni dhambi. na waoga hawataiona mbingu., woga huzaa unafiki. Mwanadamu alizaliwa siku moja na atakufa siku moja. huwa ninauchukia sana unafiki,.

JESUS IS LORD&SAVIOR
 
Tuacheni wivu na Mama,kwani picha ikiwa kwenye mtungi wa gesi inakuuma nini
2025,Tupo na Mama
 
Wanaogawa mitungi ni watanzania wenye mapenzi mema na Dr Samia. Wanaogawiwa mitungi hawajalazimishwa kuipokea ila kwa utashi wao wanapokea mitungi. Hii inaonyesha mama anakubalika. Msajili wa vyama hahusiki na maamuzi ya wanaomkubali Mama.
 
Back
Top Bottom