Ndugu zangu Watanzania,
Kwa Hakika Tuna Rais mbele yetu kama Taifa, Tuna kiongozi mwenye upendo na Taifa hili, tuna Jemedari hodari ambaye wakati wote ni Mshindi,tuna kiongozi mwenye maono ,maarifa na akili kubwa mbele yetu,tuna Rais ambaye anajua wajibu wake na kufurahia kazi yake. Tuna Komandoo ambaye amejitoa mhanga kupigania Taifa lake.
Tuna Field Marshall Katika Taifa letu. Rais Samia Rais Samia analeta raha sana kwa Taifa letu. Ndio sababu unaona hata nyuso za watanzania mitaani zina furaha ,tabasamu , matumaini na bashasha kubwa sana. Kwa sababu ya kuwa na mfariji Wa Taifa mwenye upendo ,huruma ,ukarimu , unyenyekevu na kujitolea kwa ajili ya watanzania wote.
Ni kiongozi ambaye kila akitoka nje ya mlango wake anatoka na fursa mkononi kwa ajili ya watanzania,anatoka na majawabu kwa kero za wananchi,anatoka na fursa za ajira kwa vijana ,anatoka na kikombe cha furaha kwa ajili ya watanzania. Rais Samia ni Kama nuru au Mwanga katikati ya giza.
Embu Tazama katika picha hii ya siku ya leo ambayo imemfanya hata mlinzi wake wa kushoto au waweza kusema kulia kwake akapatwa na tabasamu katika uso wake kuashiria kufurahia . Kwa hakika Rais Samia ni Mpango wa Mungu Mwenyewe kuongoza Taifa letu. Yaani huchoki kumfuatilia Mama . Ni kama nyota ya asubuhi . Rais Samia ni Neema na baraka kwa Taifa letu. Ndio maana mambo yanakwenda yakiwa yamenyooka kama rula. Kwa sababu aliye kitini ni mwenye kibali cha Mungu.
Rais Samia Ishi Maisha marefu Mama yetu. Wewe ni Mwanga na nuru ya Taifa letu uliyeleta furaha na tabasamu kwa mamilioni kwa mamilioni ya watanzania. Umefanyika baraka na neema kwa watu wa makundi Yooote.
View attachment 3426405
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa Maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.