Uchaguzi 2020 Pierre Liquid atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Iringa Mjini, asema Msigwa anang'oka pale

Uchaguzi 2020 Pierre Liquid atangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Iringa Mjini, asema Msigwa anang'oka pale

Tofauti ya Pierre na wafuatao ni ipi?
1. Msukuma
2. Lusinde
3. Mtulia na rafikie Mtolea
4. Sugu
5. Bwege
6. Professor J
7. Lameck Airo
8. Na wengine kibao

Mara nyingi hawa huchangia maada zenye mbwembwe za kisiasa, kitu ambacho Pierre hatoshindwa lakini zile maada ambazo zinazohitaji shule hutowasikia...
 
Kimsingi Bunge letu ni toothless,hata akienda hao kwenda kugonga meza wanafaa
 
Ha ha ha hakika sasa ubunge umekuwa kama u monitor wa darasa la 3A ,sasa piere anawekwenda bungeni kugawa vinywaji au kuwa mtunga sera na sheria za nchii hii?

“Mimi natangaza nia ya kwenda kugombea Jimbo la Iringa Mjini. Mimi kule ndio maeneo ya kwetu kule ndiko alikozaliwa mama, Mchungaji Msigwa anatoka pale,”- Piere Liquid


Ndio maana kuna uzi nilisema ni rahisi sana kuwa mbunge kuliko kuwa mfagiaji wa bunge (angalau mfagiaji anatakiwa kuwa na cheti cha form four,awe na certificate of cleaning and maintenance)bila kusahau ajue lugha zote mbili kwa ufasaha

Pata picha mbunge lina
Harmonize
Piere liquid
Steve Nyerere
Kingwendu
Shilole
Irene Uwoya
Mwana FA

Hatarii hii lazima meza za bunge zipasuke kwa makofi.....mungu atupe uhai tufike Oktoba.
Mwana FA ni kichwa mkuu...
 
Yaani kwa CCM ubunge ubunge umekuwa kitu rahisi sana,hadi wenda wazimu wanatamani!
 
Yaani kwa CCM ubunge ubunge umekuwa kitu rahisi sana,hadi wenda wazimu wanatamani!
 
Kawazidi wote hao elimu dunia,ila ukimsikiliza kwenye siasa ni mweupw mno hakuna kitu labda kama ana kwenda kutunga nyimbo

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
Nimemsikiliza mwana Fa alihojiwa, na juzi juzi alikuwapo nafikiri clouds ama wasafi akihojiwa yeye na joe makini, hajui kujenga hoja kabisaaaaaa....joe makini alionekana ndio mkomavu maana anajenga hoja na kujibu maswali kimpangilio.
fa hajui kujenga hoja, siasa hatoiweza labda abebwe nanyimbo zake..
 
Pierre alikua katika hali gani kipindi anatangaza nia😀😀 isije kua liquid
 
Back
Top Bottom