Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Habari za jumapili!
Zile porojo za Watu waongo kuwa mzazi ni mzazi zinaenda kufutika. Kila siku nawaambia hapa, mahusiano ya Watu yanatokana zaidi na ukaribu wao jinsi wanavyoishi na kutendeana.
Kuzaa sio sababu ya mtu kukupenda.
Upendo unasababu kuu zifuatazo;
1. Hisia za ndani.
Hii mara nyingi ni baina ya wapenzi. Lakini pia inaweza kutokea tuu ukampenda mtu from nowhere na sio kwamba mna uhusiano wa kimapenzi.
2. Mahusiano mazuri
Upendo wa kutengeneza ni ule mtu anakupenda kwa sababu unafanya mambo fulani mazuri kwàke.
Kwa mfano kumsaidia, kumhudumia, kumpa vitu vizuri na kumtendea mambo yote mema.
Mtu hawezi akakupenda ati kisa wewe ni mzazi wake au mtoto wake.
Kama kuzaa pekee ingekuwa ni sababu ya kupenda basi wazazi wangependa watoto wote sawa jambo ambalo haliwezekani.
Na kama mtu kuwa mzazi ni sababu ya kumpenda basi kusingekuwa na ile mtoto kumpenda Baba kuliko Mama au kumpenda Mama kuliko Baba. Hii inamaanisha kuwa kuna sababu zaidi ya kuwà mzazi au kuwa mtoto ndipo upendwe.
Andiko hili limelenga kuwafanya Watu wawajibike, wajue kuwa upendo kwa sehemu kubwa unajengwa na mahusiano mazuri, ukaribu wenye wema na uungwana kuliko kitu kingine.
Mabadiliko ya maisha hasa katika utafutaji wa riziki, mabadiliko ya muingiliano wa kiutamaduni yamechangia pakubwa katika kupungua kwa upendo baina ya Wazazi. Zamani ilikuwa ni Baba lakîni kwa sasa janga hilo linaenda kuwapata kina mama.
Zamani ilisemwa kuwa Mama na mtoto upendo wao hautenganishwi lakini hoja kubwa katika hilo ni kuwa Wamama zamani walikuwa karibu na watoto wao kuliko Wababa. Hiyo ikafanya mama aonekane kama anajitoa zaidi kuliko Baba jambo ambalo halikuwa sahihi.
Mambo yamebadilika, siku hizi wanawake wameanza kuingia katika kutafuta riziki tena kwa umbali mrefu.
Wengine huenda kusoma mbali na kuacha watoto wao kwa Bibi au ndugu zao.
Uchunguzi wangu usiotia shaka unaonyesha kuwa watoto wengi zaidi ya asilimia 90 walioishi mbali na wazazi wao yaani baba na mama yao hawana mapenzi tena na wazazi wao.
Hakuna ukaribu wowote. Hakuna uhusiano wowote. Upendo hakuna.
Uzae kwa uchungu, au kwa ganzi, au kwa namna yoyote ile. Elewa kuwa hiyo haina maana yoyote kwa yule unayemzaa ukizingatia kuwa wakati hayo yanafanyika mtoto anakuwa hana akili yoyote na hiyo Mungu kaiweka kwa hekima kubwa.
Mtoto ni malezi. Uhusiano wa Watu ni kukaa karibu na kushirikiana.
Kama Taikon nashauri, tujitahidi sana kuishi na watoto wetu au familia ili kuepuka matatizo huko mbeleni.
Ikiwa itashindikana kuishi na watoto wetu basi hiyo itamaanisha upendo baina yetu utakuwa umeshindikana na hakutakuwa na wakumlaumu hasa Mtoto.
Mahusiano yatabaki kuwa yakawaida kama ya ndugu tuu na wala sio mahusiano ya Mama na Mwana au Baba na Mwana.
Hicho ndicho ambacho vijana wengi na mabinti wengi kwa sasa wanapitia. Wengi wanajilazimisha kupenda wazazi wao lakini wanashindwa, wanaishia kuteseka. Huwezi lazimisha ukaribu ambao haukuwepo kwa mtu ambaye alitakiwa awe karibu lakini akawa mbali.
Najua kuna Watu watakuja na hekaya za kibiblia ambazo hazina uhalisia na wengine watakuja na hadithi za Kale za kimila ambazo nyingi ni uongo usio na uhalisia wowote.
Nasisitiza, hakunaga ukaribu au upendo kisa mtu alimzaa fulani. Ukaribu na upendo uliopo ni aidha wa asili(hiyari) au ule wa mahusiano mazuri.
Vijana wa sasa ni vizuri hayo tuyaelewe mapema ili huko mbele tuendako ambapo tutakuwa Watu wazima akili zikiwa zimekomaa na kubadilika zikihitaji familia, ukaribu na upendo kutoka kwa watoto wetu tusiwe na vizuizi vyovyote.
Robèrt Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam