Pigo la mwisho kwa Thadei Ole Mushi: Katoliki wakataa kumzika kwa kuwa aliwapinga TEC kuhusu DPW

Pigo la mwisho kwa Thadei Ole Mushi: Katoliki wakataa kumzika kwa kuwa aliwapinga TEC kuhusu DPW

Sijawahi kuona waislam wanamsusia marehemu. Wana ushirikiano sana kwenye misiba, taarifa zikitolewa chaap wamefika shughuli inaanza.
Ni waislam siyo? Wakatoliki wao wana taratibu zao. Huwezi kuwa jambazi na huhudhurii kanisani halafu ikifika siku ya mazishi unataka kanisa likuzike.
 
Ndo hivyo tena Thadei Ole Mushi kaenda motoni milele na milele kwa kosa la kupinga waraka wa kanisa takatifu katoliki la mitume, ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi ufufuko wa miili na uzima wa milele.
Ameen, R.I.P
 
Hili swala la kanisa katoliki kususia ibada za mazishi kwasababu tu marehemu labda alikua hashiriki jumuiya ndogo ndogo au alikua hana sakramenti ya ndoa au tu kama ishu kama hii ya Thadei na kususia ni wazi inakosea tunahukumu tumejeuka Mungu sasa
 
Kuzikwa ni kuzikwa tu hata ukitupwa.

Ukizikwa kikristo ama kiislam hakuna kitachoongeza mwili wako utaoza na kubaki mifupa na kututengenezea rutuba udongoni.
Sawa Je Thadei Ole Mushi aliamini kama unavyoamini? Kama ndivyo basi msilaumu Kanisa.
 
Nani analia Kirchhoff?

Naelezea ujinga ambao kanisa lenu limekumbatia.

Nyie endeleeni kubariki ushoga maana ndo kazi mnayoiweza.

Hizo PhD za falsafa na Theology kwa hao mapadri wenu bado sioni umuhimu wake kama bado wako na akili ambazo ni primitive kama hizo..
Si Ujinga. Ni Imani. Ikiwa Unaamini Mafundisho ya Kanisa na kuyafuata utazikwa kwa utaratibu wa Kanisa. Na Kanisa litahusika Kuzika miili ya Waumini Marehemu waliokufa kayika Hali ya Neema ya Utakaso.

Huamini usilie lie.
 
Kati ya vitu vya kipumbavu ambavyo kanisa katoliki huwa wanafanya mojawapo ni hili, mtu ameshafariki alikuwa muumini katika imani, unakataa kumuwekea misa eti kwa sababu hakutoa zaka, aliwapinga, hakuhudhuria Jumuiya , hoja za kipumbavu kabisa!!
 
Kanisa Katoliki lagoma kuendesha Ibada ya misa ya mazishi ya Thadei Ole Mushi kwa sababu ALIPINGA WARAKA WA BARAZA LA MAASKOFU WA KANISA KATOLIKI TANZANIA (TEC) Uliopinga uuzwaji wa Bandari, uliotolewa tarehe 18 August 2023 na TEC.

Thadei Ole Mushi alipinga hadharani waraka wa TEC, kupitia andiko lake la tarehe 18 August 2023 lenye kichwa cha Habari "WARAKA WA MAASKOFU SIO ITHIBATI ZA MAONI YA WATANZANIA"

Juzi ndugu na msemaji wa familia Bwana Victor Tesha, alitangazia dunia kwamba ibada ya mazishi ya kumuaga ndugu yetu Thadei Ole Mushi kwa Dar es Salaam ingefanyika katika kanisa la St. Peter - Oysterbay.

Lakini watu wengi ikiwemo mimi tulipofika kanisa la St. Peter's Oysterbay, tulikuta milango ya kanisa imefunga na hakuna dalili ya kuwepo kwa misa yoyote.

Uamuzi wa haraka kutaarifu watu waelekee Muhimbili katika kanisa la Pamoja (siyo Katoliki) ukafanyika na pakaendeshwa ibada na mapadre ambao ni marafiki wa karibu wa Thadei Ole Mushi na siyo Paroko anayehusika katika parokia yake ya Muhimbili.

Leo familia imekwaa tena kisiki kingine Mkoani Kilimanjaro, Uru nyumbani kwa Thedei Ole Mushi baada ya Parokia ya Uru nyumbani kwa marehemu kugomea kuendesha mazishi na kufunga milango kiasi cha kupelekea kutafutwa kwa wachungaji wa madhehebu ya Kipentekoste pale Uru.

Baadae ibada ikaendeshwa na kasisi akiwa amevaa t-shirt nyeusi na sio mavazi halisi ya ibada kwa mujibu wa taratibu. Na wala hakukuwa na kwaya ya Kanisa.

Wajuzi na wasomi wa kanisa Katoliki wanasema ukipinga Waraka wa Maaskofu ni sawa na kuasi kanisa kwa kukataa mafundisho yake, hivyo kama utafariki kabla ya kurudishwa kundini utakuwa umefariki kama muasi nje ya kanisa na hivyo kanisa halitohusika na mazishi yako.

Hili ni Somo kubwa na funzo kwa wanasiasa na watu wote ambao tulikuwa hatujui uzito na maana ya waraka wa baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambao hutolewa na kusomwa makanisa yote ya waumini wao.

Kama na wewe ni muuumini wa kanisa katoliki na unajua uliropoka na kupinga lolote kuhusu waraka ule wa TEC fanya haraka urudishwe kundini.

VIJANA🙄
kosa kubwa wakatoliki huwa wanalifanya, ni mapadre kujiona wao ni miungu watu wanaowapeleka watu kwa Mungu, ndio maana hata kama unasali kwao kama huendi jumuiya wanaweza kukuadhibu namna hiyo. padre anaogopwa, anaheshimiwa kuliko chochote, wakati ni wanadamu tu, wazinzi tu na wezi tu hawana lolote na watakua wa mwisho kufika mbinguni I tell you.
 
Wambie maana hawajui kua Pope ni mwakilishi wa Yesu hapa duniani. Asemacho Pope amesema Yesu.
 
Kati ya vitu vya kipumbavu ambavyo kanisa katoliki huwa wanafanya mojawapo ni hili, mtu ameshafariki alikuwa muumini katika imani, unakataa kumuwekea misa eti kwa sababu hakutoa zaka, aliwapinga, hakuhudhuria Jumuiya , hoja za kipumbavu kabisa!!
Sio lazima kuwa mkatoliki...nenda kwingine ambako hakuna utaratibu bwashee
 
Kati ya vitu vya kipumbavu ambavyo kanisa katoliki huwa wanafanya mojawapo ni hili, mtu ameshafariki alikuwa muumini katika imani, unakataa kumuwekea misa eti kwa sababu hakutoa zaka, aliwapinga, hakuhudhuria Jumuiya , hoja za kipumbavu kabisa!!
Fuateni taratibu za Kanisa lenu kama huziwezi ni bora ukae pembeni mapema na utafute panapokufaa uabudu huko.

Ukikubali kukaa katikati ya waumini kubali pia kufuata miongozo yao.
 
Na kanisa wasiposhiriki kwenye shughuli za mazishi, Marehemu anapungukiwa nini?

Kwanzaa hizi misa zinaulazima gani? Binadam tumejiwekea mfumo wa kihovyo. Azikwe au lah won’t change any thing ,and Mushi is at peace now

Kabla ya katolic, watu walikuwa wanazikwa vip
Dini ni institutions km institutions nyingine
Dini hazitoki kwa mungu. Dini zinatoka kwa binadamu ndio maana haya hutokea
 
Back
Top Bottom