Pigo la mwisho kwa Thadei Ole Mushi: Katoliki wakataa kumzika kwa kuwa aliwapinga TEC kuhusu DPW

Pigo la mwisho kwa Thadei Ole Mushi: Katoliki wakataa kumzika kwa kuwa aliwapinga TEC kuhusu DPW

Kila binadamu ana siri ambayo atakufa nayo na hatamuambia mtu
Je wao ina maana hawana?
Siwezi kuamini kuwa kuna mwanadamu hana dhambi
Sasa utamuombeaje mwenzio
Kama hawatamzika naamini watamzika wengine ili mradi aingie kwenye tumbo la ardhi
Na litatumeza wote
 
Kanisa Katoliki lagoma kuendesha Ibada ya misa ya mazishi ya Thadei Ole Mushi kwa sababu ALIPINGA WARAKA WA BARAZA LA MAASKOFU WA KANISA KATOLIKI TANZANIA (TEC) Uliopinga uuzwaji wa Bandari, uliotolewa tarehe 18 August 2023 na TEC.

Thadei Ole Mushi alipinga hadharani waraka wa TEC, kupitia andiko lake la tarehe 18 August 2023 lenye kichwa cha Habari "WARAKA WA MAASKOFU SIO ITHIBATI ZA MAONI YA WATANZANIA"

Juzi ndugu na msemaji wa familia Bwana Victor Tesha, alitangazia dunia kwamba ibada ya mazishi ya kumuaga ndugu yetu Thadei Ole Mushi kwa Dar es Salaam ingefanyika katika kanisa la St. Peter - Oysterbay.

Lakini watu wengi ikiwemo mimi tulipofika kanisa la St. Peter's Oysterbay, tulikuta milango ya kanisa imefunga na hakuna dalili ya kuwepo kwa misa yoyote.

Uamuzi wa haraka kutaarifu watu waelekee Muhimbili katika kanisa la Pamoja (siyo Katoliki) ukafanyika na pakaendeshwa ibada na mapadre ambao ni marafiki wa karibu wa Thadei Ole Mushi na siyo Paroko anayehusika katika parokia yake ya Muhimbili.

Leo familia imekwaa tena kisiki kingine Mkoani Kilimanjaro, Uru nyumbani kwa Thedei Ole Mushi baada ya Parokia ya Uru nyumbani kwa marehemu kugomea kuendesha mazishi na kufunga milango kiasi cha kupelekea kutafutwa kwa wachungaji wa madhehebu ya Kipentekoste pale Uru.

Baadae ibada ikaendeshwa na kasisi akiwa amevaa t-shirt nyeusi na sio mavazi halisi ya ibada kwa mujibu wa taratibu. Na wala hakukuwa na kwaya ya Kanisa.

Wajuzi na wasomi wa kanisa Katoliki wanasema ukipinga Waraka wa Maaskofu ni sawa na kuasi kanisa kwa kukataa mafundisho yake, hivyo kama utafariki kabla ya kurudishwa kundini utakuwa umefariki kama muasi nje ya kanisa na hivyo kanisa halitohusika na mazishi yako.

Hili ni Somo kubwa na funzo kwa wanasiasa na watu wote ambao tulikuwa hatujui uzito na maana ya waraka wa baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambao hutolewa na kusomwa makanisa yote ya waumini wao.

Kama na wewe ni muuumini wa kanisa katoliki na unajua uliropoka na kupinga lolote kuhusu waraka ule wa TEC fanya haraka urudishwe kundini.

VIJANA🙄

Tunaomba uthibitisho kama amekataliwa sababu ya kukataa tamko la TEC! Ninachojua, kanisa huwa halikuziki kama ulikuwa sio mwana jumuiya wake, au hukufunga ndoa rasmi, au ulikataa kwa hiari yako kushiriki na kuwa mwana kanisa. Kwanini lisubiri ufe ndio lije kukuzika, wakati ukiwa hai ulikuwa hauna habari nalo?
 
Vipi na maaskofu waliopinga hadharani issue ya Papa ya kubariki mashoga?

Nao watasuswa?
Hii ya kutozikwa na kanisa naamini ni uongo mkubwa. Kanisa litazikaje mtu ambaye hakushirikiana nalo wakati akiwa hai? Wanajuaje imani yake sasa?
Kuwa mbobezi kwenye mitandao ndio kuwa mwana kanisa? Tupeni ushahidi kuwa sababu ya kukataa tamko la TEC ndio maana aliachwa bila kuzikwa na kanisa.
Mimi nampinga Papa na mafundisho yake bandia. Ila sijafukuzwa kanisani na hakuna aliyefukuzwa kanisani. Maana anajua anachofanya sio sawa. Ndio maana anaishia kusema wanaokataa ni wanafiki.
Msiliongelee kanisa kama hamjachukua muda wa kujifunza na kulielewa.
 
sasa hoja yangu ni tuhuma za Muumin wao THADEO OLE MUSHI ambazo mtandaoni zimevuma wiki nzima kunyimwa haki yake ya mazishi kwa taarifa kuwa alipinga waraka wao kuhusu bandari. Kanisa linapaswa litoke lijieleze kama tuhuma hizo ni kweli au la na kama pia viongozi wa serikali wakatoliki walioshiriki kufanikisha mkataba wa bandari pia hawatawazika?

Tunataka Kanisa litoe ufafanuzi kwa umma kwanini lilikataa kushiriki katika mazishi ya OLe Mushi, na kama sababu ni hiyo hapo juu basi serikali ichukue hatua Kali kwa kulifutia usajili
 
Shetani hana Rafiki , Thadei aliwakana Wakatoliki wenzake akaabudu kizimkazi , ulitaka iweje ?
 
Taarifa za kutozikwa na kanisa kwa kuwa alipinga waraka wa TEC wewe umezitoa wapi? Usiishie tu kusema mitandaoni, taja ni mtandao gani na mhusika aliyesema ni nani?
 
Shetani hana Rafiki , Thadei aliwakana Wakatoliki wenzake akaabudu kizimkazi , ulitaka iweje ?

Sidhani kama Kanisa halikumzika kwasababu hizo mnazotaka kuwaaminisha watu. Lazima tujiulize au tuchunguze kwanza kama marehemu alikuwa anafuata taratibu zote za kanisa?

Magufuli alipingana na vitu vingi vya kanisa lake mwenyewe tena hadharani, mfano ni tahadhari ya Covid19, hakuzikwa kwa taratibu za kanisa?
 
Kama ni suala la bandari basi kuna viongozi wa serikali na chama chungutele hawatazikwa na RC sababu walipinga waraka wa Charles Kitima
 
sasa hoja yangu ni tuhuma za Muumin wao THADEO OLE MUSHI ambazo mtandaoni zimevuma wiki nzima kunyimwa haki yake ya mazishi kwa taarifa kuwa alipinga waraka wao kuhusu bandari. Kanisa linapaswa litoke lijieleze kama tuhuma hizo ni kweli au la na kama pia viongozi wa serikali wakatoliki walioshiriki kufanikisha mkataba wa bandari pia hawatawazika?

Tunataka Kanisa litoe ufafanuzi kwa umma kwanini lilikataa kushiriki katika mazishi ya OLe Mushi, na kama sababu ni hiyo hapo juu basi serikali ichukue hatua Kali kwa kulifutia usajili
hilo kanisa halikurupukagi na wala halibaibaiki na kasoro au dosari za imani ya moja ya waamini wake kiujumlajumla wala kisiasa...

kama kuna isue binafsi kumuhusu miongoni mwa waamini wake, basi ni issue ya kanisa mahalia alikokua anashiriki muamini huyo sala za Jumuia, vyama vya kutume na huduma nyingine za kanisa mahalia,

lakini na hata hivyo sio muhimu sana kwani,
Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe...
 
Unawafananisha wakatoliki na Mh Nape Nauye Lissu kutamka "maagizo kutoka juu" akaita press ndani ya dakika tano. Wakatoliki sio wehu hivyo
 
RC ni centralised, sio kama hao wengine.
Kamwe hawana huo muda wa kujibujibu hoja za kila mtu.
Usitegemee jibu lolote la kitaifa,nenda kwenye jumuiya yake utapewa majibu
 
Sidhani kama Kanisa halikumzika kwasababu hizo mnazotaka kuwaaminisha watu. Lazima tujiulize au tuchunguze kwanza kama marehemu alikuwa anafuata taratibu zote za kanisa?

Magufuli alipingana na vitu vingi vya kanisa lake mwenyewe tena hadharani, mfano ni tahadhari ya Covid19, hakuzikwa kwa taratibu za kanisa?
Kama unataka kulipangia kanisa basi lipangie
 
Kama unataka kulipangia kanisa basi lipangie
Silipangii kanisa, ila napingana na sababu zenu za kisiasa.

Kama Kanisa lingekuwa lilisusia kwasababu hizo za waraka, hakuna Paroko angekanyaga kwenye huo msiba. Ila kwa hali iliyoelezwa na mleta uzi, inaonesha marehemu alikuwa hashiriki mambo ya kanisa. Au pengine alikuwa anaishi na mwanamke na hakuwa na ndoa.

Kama ilikuwa ni kupingana na kanisa badi Magufuli asingezikwa na kanisa.
 
Wapumbavu tu hao,
Hata akiachwa barabaran yeye anapungukiwa nn?ooh, anaye hukumu ni mungu,bull shit!
 
Back
Top Bottom