Pigo la mwisho kwa Thadei Ole Mushi: Katoliki wakataa kumzika kwa kuwa aliwapinga TEC kuhusu DPW

Pigo la mwisho kwa Thadei Ole Mushi: Katoliki wakataa kumzika kwa kuwa aliwapinga TEC kuhusu DPW

sasa hoja yangu ni tuhuma za Muumin wao THADEO OLE MUSHI ambazo mtandaoni zimevuma wiki nzima kunyimwa haki yake ya mazishi kwa taarifa kuwa alipinga waraka wao kuhusu bandari. Kanisa linapaswa litoke lijieleze kama tuhuma hizo ni kweli au la na kama pia viongozi wa serikali wakatoliki walioshiriki kufanikisha mkataba wa bandari pia hawatawazika?

Tunataka Kanisa litoe ufafanuzi kwa umma kwanini lilikataa kushiriki katika mazishi ya OLe Mushi, na kama sababu ni hiyo hapo juu basi serikali ichukue hatua Kali kwa kulifutia usajili
Duh! Mkuu; Hebu fanya ka-utafiti kako binafsi kasikoegemea kuvuma kwa Taarifa za Mitandaoni halafu urudi tena hapa.
 
Vipi kuhusu na wale wakatoliki waliopinga hadharani waraka wa Papa kuhusu kuwabariki mabwabwa. Nao watatengwa? Wakifa watagomewa kuzikwa kikatoliki?
Naongezea: Je, na maaskofu wa Zambia na Malawi nao itakuwaje bila kusahau na yule Padre aliyefukuzwa?
Nionavyo mm ni kwamba Hoja ya kutozikwa kwa huyo ndg. SIO narudia tena SIO kupinga waraka wa TEC. Arejee mambo yake Katika Jumuiya Ndogondogo(JNNK). Huko ndo lilipo chimbuko la kunyimwa huduma ya kuzikwa na kanisa.
 
Kanisa Katoliki lagoma kuendesha Ibada ya misa ya mazishi ya Thadei Ole Mushi kwa sababu ALIPINGA WARAKA WA BARAZA LA MAASKOFU WA KANISA KATOLIKI TANZANIA (TEC) Uliopinga uuzwaji wa Bandari, uliotolewa tarehe 18 August 2023 na TEC.

Thadei Ole Mushi alipinga hadharani waraka wa TEC, kupitia andiko lake la tarehe 18 August 2023 lenye kichwa cha Habari "WARAKA WA MAASKOFU SIO ITHIBATI ZA MAONI YA WATANZANIA"

Juzi ndugu na msemaji wa familia Bwana Victor Tesha, alitangazia dunia kwamba ibada ya mazishi ya kumuaga ndugu yetu Thadei Ole Mushi kwa Dar es Salaam ingefanyika katika kanisa la St. Peter - Oysterbay.

Lakini watu wengi ikiwemo mimi tulipofika kanisa la St. Peter's Oysterbay, tulikuta milango ya kanisa imefunga na hakuna dalili ya kuwepo kwa misa yoyote.

Uamuzi wa haraka kutaarifu watu waelekee Muhimbili katika kanisa la Pamoja (siyo Katoliki) ukafanyika na pakaendeshwa ibada na mapadre ambao ni marafiki wa karibu wa Thadei Ole Mushi na siyo Paroko anayehusika katika parokia yake ya Muhimbili.

Leo familia imekwaa tena kisiki kingine Mkoani Kilimanjaro, Uru nyumbani kwa Thedei Ole Mushi baada ya Parokia ya Uru nyumbani kwa marehemu kugomea kuendesha mazishi na kufunga milango kiasi cha kupelekea kutafutwa kwa wachungaji wa madhehebu ya Kipentekoste pale Uru.

Baadae ibada ikaendeshwa na kasisi akiwa amevaa t-shirt nyeusi na sio mavazi halisi ya ibada kwa mujibu wa taratibu. Na wala hakukuwa na kwaya ya Kanisa.

Wajuzi na wasomi wa kanisa Katoliki wanasema ukipinga Waraka wa Maaskofu ni sawa na kuasi kanisa kwa kukataa mafundisho yake, hivyo kama utafariki kabla ya kurudishwa kundini utakuwa umefariki kama muasi nje ya kanisa na hivyo kanisa halitohusika na mazishi yako.

Hili ni Somo kubwa na funzo kwa wanasiasa na watu wote ambao tulikuwa hatujui uzito na maana ya waraka wa baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) ambao hutolewa na kusomwa makanisa yote ya waumini wao.

Kama na wewe ni muuumini wa kanisa katoliki na unajua uliropoka na kupinga lolote kuhusu waraka ule wa TEC fanya haraka urudishwe kundini.

VIJANA🙄
Kwa hiyo ina mana maaskofu wa RC wanavyompinga Papa wao kuhusu kubariki ndoa za jinsia moja nao watatengwa sababu uamazi wa Papa ndio uamuzi wa kanisa? pia mbona katibu wa baraza la maaskofu yeye alihudhuria ile hafla juu ya bandari kule ikulu ina maana nae watamfungia milango ya kanisa itakapofika siku yake?
 
WAmejaa unafiki hao watu
Kwa hiyo ina mana maaskofu wa RC wanavyompinga Papa wao kuhusu kubariki ndoa za jinsia moja nao watatengwa sababu uamazi wa Papa ndio uamuzi wa kanisa? pia mbona katibu wa baraza la maaskofu yeye alihudhuria ile hafla juu ya bandari kule ikulu ina maana nae watamfungia milango ya kanisa itakapofika siku yake?
 
Hapa ndio dini yangu huwa inanichosha kabisa!

Hata wakatae kumsalia, what difference does it make to a dead man?🧟‍♂️ AbsoFREAKINGlutely NONE!!!!
Kama hakuna any difference Kwa nini ndugu wa huyo dead man walienda kuomba marehemu wao asaliwe wasingekwenda kuomba hiyo misa kabisa.
Umeleta hoja ya hovyo sana.
Huyo marehemu namkumbuka sana alikuwa ana hoja za hovyo hovyo sana.
Kumbe kanisa halikusalia mwili wake mfu.
Safi sana Kwa kanisa katoliki halina unafki.
Natumaini kwa sasa kiimani jamaa litakuwa motoni linaungua.
Wanasiasa acheni unafki na kanisa katoliki liheshimiwe milele
 
Back
Top Bottom