Pigo la mwisho kwenye mbuyu huwa na madhara zaidi kuliko mengine, unamaliza kazi!

Pigo la mwisho kwenye mbuyu huwa na madhara zaidi kuliko mengine, unamaliza kazi!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,316
Reaction score
871,876
Unajua kinachoangusha mti uliokuwa unakatwa sio lile pigo la mwisho.. Japo hilo ndio huonekana kama ndio limemaliza kazi
Nyuma yake kabla kuna mengi yalishapiga mengine on target na mengine off target.. Lakini kila moja lilileta madhara yake kwa namna yake!

Kwa ukubwa wake na kwa udogo wake kuna baadhi ya miti huchakazwa na shoka lakini huahirisha kuanguka hata hivyo huachwa na udhoofu mkubwa kutokana na majeraha iliyopata
Kwenye somo la kilimo sometimes kuna njia ya kuukausha mti bila kuuangusha..

Kama ikionekana mahali ulipo ukianguka unaweza kusababisha madhara na uharibifu.. Huo humenya ngozi/ganda lake kuuzunguka. Ganda la mti ndio hutumika kama mishipa ama mtandao wa kupeleka chakula juu kwenye matawi toka chini ardhini kwenye mizizi

Kwa kumenya ganda kuuzunguka hukata mawasiliano ya chakula na mti hufa taratibu kwa kuanza kunyauka na hatimaye kufa kabisa
Njia hii si sahihi sana kama mnaandaa shamba jipya ambapo vichaka, magugu, visiki, mimea na miti isiyotakiwa inabidi vyote vikatwe ving'olewe vichomwe moto na kusafishwa kabisa!

Ni wakati wa kuandaa shamba jipya... Bado shoka moja tu mbuyu uende chini.. Kishapo mizizi ing'olewe, vichaka vifyekwe, magugu yang'olewe na vyote vichomwe moto kuashiria msimu mpya na pando jipya..!

Good morning Tanganyika...!
 
Nyuzi za humu siku hizi kama hujawahi kupitia CUBA au walau uwe na C tatu kwenye vyeti vya elimu ya kati....utabakia kushangaa shangaa Tu.....
20250425_124430.jpg
 
Umri ule kwa Mwanamke ulikua ni wa kupumzika na kula pensheni ya 80%

Sijui nani kamdanganya kuhangaika na watanganyika,….

Wanamchosha Mama wa watu kwa maslai yao binafsi
Kwenye kuteleza kuna maanguko matatu
1. Usalimike kufika chini
2. Ufike chini na kusimama chap bila kuumia bali kuchafuka kidogo tuu
3. Ufike chini kwa mweleka mkubwa uumie na kushindwa kusimama tena.. Na kama utaweza kusimama hutakuwa sawa kama mwanzo
 
Nilimuuliza Askofu wangu katoliki ambae ni mtu wa kutoficha kali zake thabiti yeye ni mkurugenzi wa vijana yaani akisikia kesi ya mkatoliki simu hii utasemwa live utaamani ufe nikamuuliza baba kwa nini kanisa linakaa kimya na yote haya akanijibu hivi :
'' Mwanangu the only mimi ni kiongozi wa dini sio kiongozi wa siasa kaisome biblia yako mahusiano ya ahabu na nabii eliya ,eliya kazi yake ilikuwa kumpa ukwel nini sauti ya Mungu inasema ,kazi ya kuamua kutubu au kufanya moyo mgumu hiyo ni vita ya Mungu ,Mwanangu hupaswi kupigana kwa niaba ya mungu utashindwa uache apigane mwenyewe. akasema biblia imeeleza wazi Efeso 6: kwa maana vita vyetu si vya nyama na damu bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya

Akasema baada ya zile waraka huwa vita inahamishiwa uwanja huo wa nyama na damu unapigwa kiroho juu ya WAKUU WAO WA GIZA wanaowasaidia kutoka bagamoyo ,kigoma ,sumbawanga etc

Hivo Mungu au mwenye nguvu yeyote huwa hapandi ujue anapiga mapigo vipi ndio maana huruhusiwi zurura eneo la jeshi lolote .

AKANIAMBIA YEZEBEL HATOSHINDA''
 
Mafarisayo hataki amani kabisa mda wote mnashambulia tu.
 
Mafarisayo hataki amani kabisa mda wote mnashambulia tu.
Mgeni siku ya kwanza
mpe mchele na panza;
mtilie kifuani,
mkaribishe mgeni.

Mgeni siku ya pili
mpe ziwa na samli;
mahaba yakizidia,
mzidishie mgeni.

Mgeni siku ya tatu
jumbani hamuna kitu.
mna zibaba zitatu,
pika ule na mgeni.

Mgeni siku ya nne
mpe jembe akalime.
akirudi muagane,
aende kwao mgeni,

Mgeni siku ya tano
mwembamba kama sindano,
hayeshi masengenyano,
asengenywayo mgeni.

Mgeni siku ya sita;
mkila mnajificha;
mwaingia vipembeni
afichwaye ni mgeni.

Mgeni siku ya saba,
si mgeni ana baa.
hata moto mapaani
katia yeye mgeni,

Mgeni siku ya nane;
njoo ndani tuonane.
atapotokea nje,
natuagane mgeni,

Mgeni siku ya kenda;
enenda mwana kwenenda!
usirudi nyuma nenda,
utokomee mgeni.

Mgeni siku ya kumi
kwa mateke na magumi.
hapana afukuzwaye,
Ila ni yeye mgeni.
 
Unajua kinachoangusha mti uliokuwa unakatwa sio lile pigo la mwisho.. Japo hilo ndio huonekana kama ndio limemaliza kazi
Nyuma yake kabla kuna mengi yalishapiga mengine on target na mengine off target.. Lakini kila moja lilileta madhara yake kwa namna yake!

Kwa ukubwa wake na kwa udogo wake kuna baadhi ya miti huchakazwa na shoka lakini huahirisha kuanguka hata hivyo huachwa na udhoofu mkubwa kutokana na majeraha iliyopata
Kwenye somo la kilimo sometimes kuna njia ya kuukausha mti bila kuuangusha..

Kama ikionekana mahali ulipo ukianguka unaweza kusababisha madhara na uharibifu.. Huo humenya ngozi/ganda lake kuuzunguka. Ganda la mti ndio hutumika kama mishipa ama mtandao wa kupeleka chakula juu kwenye matawi toka chini ardhini kwenye mizizi

Kwa kumenya ganda kuuzunguka hukata mawasiliano ya chakula na mti hufa taratibu kwa kuanza kunyauka na hatimaye kufa kabisa
Njia hii si sahihi sana kama mnaandaa shamba jipya ambapo vichaka, magugu, visiki, mimea na miti isiyotakiwa inabidi vyote vikatwe ving'olewe vichomwe moto na kusafishwa kabisa!

Ni wakati wa kuandaa shamba jipya... Bado shoka moja tu mbuyu uende chini.. Kishapo mizizi ing'olewe, vichaka vifyekwe, magugu yang'olewe na vyote vichomwe moto kuashiria msimu mpya na pando jipya..!

Good morning Tanganyika...!
Watu mma mafumbo😄
 
Back
Top Bottom