Pikipiki za masafa marefu (Cross countries)

BMW zipo hapa Kinondoni kwa Mpemba karibu na Makaburi ya kinondoni, kuna ki-super market mjinga kimejaa Wapemba ndio wanaziuza but ni used
 
Google ; Harleydavidson na BMW motorbikes kuanzia 750cc utakutana nazo!!!!

Mkuu nimeangalia, BMW ndio chombo cha ukweli, hiyo ya Harleydavidson sio kali halafu haziendani na mazingira ya bongo, pia inaonekana ni kwa ajili ya starehe tu sio masafa ya mbali kwani ni fupi sana.
 
BMW zipo hapa Kinondoni kwa Mpemba karibu na Makaburi ya kinondoni, kuna ki-super market mjinga kimejaa Wapemba ndio wanaziuza but ni used

BMW za cc ngapi? na wanauza bei gani?
 
BMW zipo hapa Kinondoni kwa Mpemba karibu na Makaburi ya kinondoni, kuna ki-super market mjinga kimejaa Wapemba ndio wanaziuza but ni used

Kama hana mfuko mzuri bora achukue used aipige service. Maana mpya ni pesa ya kununua gari kruger used.
 
Mwendokasi sawasawa na umbali gawanya kwa muda

Velocity = Distance ÷ Time taken.

Sasa mkuu mwendo kasi si inategemea upo na gear namba gani? mfano umeweka gear namba tatu halafu unavuta mafuta hadi mshare unagonga kwenye 90 utasema umetumia mwendo gani kwa saa?
 
Mkuu Inteli, mimi ni bike lover and at one time nilikuwa namiliki 5 big bikes, sasa japo siendeshi tena, lakini bado namiliki bikes 2, off road na on road.
  1. Big Bikes are expensive, Bei zina range from US $ 6,000 hadi 18,000 depending on brand and status.
  2. Bongo hakuna dealers wa big bikes, mahali pa karibu ni South ila ghali, bali kuna watu wachache wanaoleta big bikes ila siku hizi sizioni, na mara moja moja hutokea wazungu wakaziuza bikes zao matangazo unaweza kuyaona sehemu za wazungu wazungu, Slip way, Shoppers etc, Mlimani City etc. Njia rahisi na bei rahisi hivyo the best option ni kuagiza kama wanavyoagiza magari.
  3. Hakuna spares za big bikes bongo, bali ukinunua Honda CBX 750 na BMW 750 unaweza kupata spares kwenye karakana ya polisi, Kilwa Rd (maafande wanakuibia!), chini ya hapo ni kuagiza tuu and it takes 3 days kwa spares from South, 5 days ukiagiza toka Dubai, 14 days ukiagiza toka Japan.
  4. Kwa vile hakuna show window ya big bikes bongo pia hakuna authorised dealers wala services, ila kuna mafundi wa bongo wanatumia tuu undundu kufungua bike ya aina yoyote, mmoja wa jamaa wazuri sana anaitwa Amiri yuko pale Magomeni Mikumi mkono wa kulia kuelekea Kigogo.
  5. Big bikes ziko imara sana, my last bike niliopata nayo ajali, ni Harley Davidson Buell Thunderbold 1100cc, niliinua US na nimekaa nayo 2 years haikuwahi hata kupata pancha!, speed ni 240kmh. Dar-Moro natumia 1:45 hrs, Dar-Dodoma 3:45 hrs, Dar-Arusha 5 hrs!.
NB. Angalizo, kwanza Tanzania hatuna barabara za big bikes hivyo the risk is too big!. Wenzetu wan a bike lane kwenye barabara zap hivyo cross country is safe.

Pili madereva wetu wa magari sio makini kivile kwenye long distance, hivyo you have to be extra extra careful.

Pasco
 

Miongoni mwa watu makini hapa jf ni pamoja na Pasco. Bonge la taarifa na uzi ufungwe.
 

mkuu vipi kuhusu hizi adventure bike,unaweza ukasafiri nazo masafa marefu kupitia njia zote yani lami na vumbi?
 
Naweza kununua kupitia ebay?
cc😛asco
Yes you can, il the best way ni kwenda kuona, unafanya test ride ndipo unanunua.

Uzuri wa big bike is you have to love it, if you can spend US $ 20,000 for a bike, why don't you spend extra 3,000 ukinunua round trip air ticket, unapewa 3 nights full board kwenye 5 star hotel, na amino usiamini, ukienda mwenyewe, the choice is bigger and the price inashuka!.

Pasco
 
Kuna chama cha bikers jina lake nimesahau lakini kwa mwaka huu walikutana mji mmoja unaitwa Alice Springs barani Australia. Hope unaeza google na wana updates nyingi sana za bikes.

Bei zake unaeza ingia hata gumtree ukasaka na kuona, ila kwa average zile common bikes sio chini ya $10,000
 
mkuu vipi kuhusu hizi adventure bike,unaweza ukasafiri nazo masafa marefu kupitia njia zote yani lami na vumbi??
Big bikes pia ziko za aina mbili, kuna on road/street bike, hizi zinataka lami tuu na kuna off road zinacheza na kote, vumbi na lami.

Kama wewe pia ni mpenzi wa off road, njoo pale viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, kila Jumapili saa 10:00-12:00 bike lovers wa off road wanakuta pale na kufanya fun ride za off road.

Pasco
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…