Pikipiki za masafa marefu (Cross countries)

Mhhh, bei yake huwa kubwa. Unanunua na kwenda kuliREMBA mwenyewe unavyotaka. Kuna watu hufanya kazi hiyo ila siyo Kiwanda. Ni kama ile program ya PIMP MY RIDE.



Bie si nzuri sana, inategemea na ukubwa wa Pikipiki na kama ni mpya au imetumika.

Angalia hapa kwa USA: http://www.cycletrader.com/Harley--...6953,Trailer|3284663&vrsn=hybrid&year=2014:*&

 
Wakuu anayefahamu aina hizo za pikipiki anijuze nahitaji kununua.
Ni pikipiki kubwa kimuundo na ni nene, pembeni nyuma huwa na kitu kama begs ngumu. Mara nyingi nawaona nazo raia wa kigeni hasa wanaotokea South Africa...

Kwa anayetaka kukosha macho juu ya madude ya ukweli ninayo yazimika aone japo kw aufupi tu...ndo utajua tofautit kati ya boda boda na vyombo vya wanaume.

1..Harley davidson motorbikes
2.bmw motorbikes
 
unazohitaji wewe nimezielewa,ni kubwa,ndefu kwenda juu na ni kwa ajili ya masafa marefu,kwa ushauri wangu tu angalia vitu hivi viwili youtube afu unipe feedback.

1.KTM lc8 adventure(in short search ktm motorbikes for adventure)
2.search yamaha for adventure
bikes hizi ni kubwa na zinapita kokote,hata hawa bike tourers wengi huwa wanatumia aina hizi za bikes ,i mean ktm na yamaha.
 
Intelligent, ngoja kesho nikipita mitaa yangu nitapiga picha niziweke hapa, then utaniambia ipi umependa nitakuunganisha na jamaa wanaouza!!
 
Pasco ilikufanya vibaya ilikufanyaje?? Kama una picha ya hizo bike tuwekee tuweze kuona tofaut ya racing bike na hizo zingine ulizozitaja
 
Nunua SANLG peleka kwa fundi welding achomelee hizo bags (case closed)
 

Kumbe Pasco ndio maana bahari huwa inajaa na kupwa randomly at chaotic movement? Je miaka hiyo hawakuweza kufanya skull CT Scan au waliona sio lazima?

Anyway miaka hiyo ulituringishia sana na mpikipiki wako mpaka ukafanya nami niweze kununua mkweche wa Yamaha Enduro ambayo mitaa ya ubungo ubungo tulikuwa wawili tu mimi na jamaa wa Maquis du Zaire?

Umenikumbusha swala moja muhimu sana nalo ni pale unaponunua chombo cha moto basi ni lazima ufikirie wapi unapata spair na mafundi wako na umegusia pikipiki za BMW za Polisi na mafundi wao ambao wanaweza kukupatia Spare,

Miaka hiyo hiyo nilizipenda sana VW Golf tukiziita "tetracycline" zikiwa nyingi tu kwenye kitengo chao na bahati mbaya nikaingia mtego kuwa nitapata spare na mafundi kutoka hukohuko, basi nikakivaa kimoja hivi na kikiweka vizuri kiasi lakini baada ya kama mwaka nikagundua kuwa vinakufa na hata wao kuvifufua inakuwa inshu kubwa ...haraka haraka nikamtafuta rodi lofa mmoja hivi nikamsukumia,

Funzo kubwa hapa ni maangalizo uliyotoa kuhusu Usalama na uhai kwanza halafu ni lazima watu wajaribu kuona mbele ni wapi atapata spare na mafundi
 
Huo upande BMW ni monsters

Jipange kuanzia 25m

Ila mimi huwa nakubali sana off road bike za Yamaha na Honda
 
Kumbe Pasco ndio maana bahari huwa inajaa na kupwa randomly at chaotic movement? Je miaka hiyo hawakuweza kufanya skull CT Scan au waliona sio lazima?
Mkuu vipik2 , you could be right, kwa situation niliuokutana nayo, CT Scan ndio hatua ya pili baada ya full body e-ray. By then CT Scan ya Muhimbili ilikuwa imeharibika, hivyo kufanya CT Scan ni Regency, TZS. 800,000 +200,000 za ambulance yao, TZS. 100,000 per trip!.

Baada ya Muhimbili nilikwenda India, CT Scan na MRI ikafanyika tena, nikamalizia South Africa.
P
 

Issue ya Skull CT Scan nimechomekea kama nduguyo anavyochomekeaga na ililenga makala zako ambazo hubadilika badilika kama flight schedule za shirika letu pendwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…