Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar

Pinda, Muungano, na Hatima ya Zanzibar


Shule kweli muhimu. Msome hapa Profesa Othman aliyosema kuhusu huu Muungano
http://www.kongoi.com/forty-years-of-the-union-is-it-withering-away-by-prof.-haroub-othman-2.html . Na yeye hakuwatakia mema?

Asante sana Fundi Mchundo na kwa kuongezea Profesa Othman anasema hivi,
However one might view the circumstances that made Zanzibar merge with Tanganyika in 1964, the fact of the matter is that Zanzibar was not annexed or forcefully incorporated. It agreed on the Union out of its own free will and as a result of decisions made by its own organs.
Ni hayo malalamiko yasiyo na msingi yaliyomfanya Mwalimu Nyerere kuyaita ya kijinga na kumkemea Raisi wa Zanzibar, Salmin Amour kwa maneno yanayofanana na haya (samahani the quote may not be exact)
Ni tabia kama ya mtoto mdogo, ukimpakata anakunyea na ukimwacha analalamika na kulialia myee, myee !
Kaazi kweli kweli !
 
Hivi ni wewe, Marcus JUNIUS Brutus, uliyemsaliti Julius Caesar aliyekupenda kama mwanae hasa ukizingatia uhusiano wake na mama yako Servilia Caepionis? Au ni wewe Francis Bacon, Attorney General aliyemtosa rafiki yake kipenzi Robert Devereux, Earl wa Essex katika kutaka kujikomba kwa Malkia Elizabeth?

Leo hii unaubeza Muungano ambao serikali ya Zanzibar na Pemba iliingia kwa hiari yake? Unamlaumu Nyerere ambae ndiye pekee aliyempokea na kumpa hifadhi Sayyid Sir Jamshid Bin Abdullah Al Said na waziri mkuu wake Muhammad Shamte Hamadi alipokimbia kwenye meli yake iliyoitwa Seyyid Khalifa? Huyo huyo Nyerere aliyewaondolea John Okello ( raia wa Uganda ambae alitokea Pemba wakati wa Mapinduzi na alikuwa mwanachama wa ASP) ambae alitaka kuendeleza mtindo wa chinja chinja? Leo kweli mnambeza?

Unasahau kuwa hiyo nchi iliyoingia kwenye muungano na Tanganyika ni Jamhuri ya Zanziba na Pemba (sio Zanziba kama unavyotaka kutuambia) na kuunda serikali ya Tanganyika na Zanziba ambayo miezi sita baadae ikajiita Jamhuri ya Muungano ya Tanzania! Unasahau kuwa wakati mnapigiwa ving'ora, mnalazimishwa kuolewa na weusi wa huko kwenu mlipokewa na kupewa hifadhi huko mnakokulaani hivi sasa? Hata pale mlipomuua Rais wenu wa kwanza ni Nyerere huyo huyo aliyekataa kuwakabidhi wakina Abdurahman Babu akijua mlichotaka kuwafanyia. Ni Nyerere huyo huyo aliyewapatia mwokozi wenu Jumbe ambae hakuwa na ufuasi mkubwa katika Baraza la mapinduzi.

Mnasema hamkuridhia Muungano na ati Nyerere aliwarubuni! Unasahau ni Rais wenu ( ambae hakuenda shule) ndiye aliyempa likizo ya wiki moja Attorney General wake Wolfgang Dourado na kufuata ushauri wa mganda Dan Nabudere badala yake? Mwenzake alimtumia AG wake Roland Brown kuhakikisha maslahi ya upande wake. Hapa nani alaumiwe? Na ni Nyerere huyo aliyekataa Muungano wa jumla akisisitiza kuwa identity ya Zanzibar ni lazima ilindwe! Leo amekuwa muovu? Mnasahau pia kuwa kikatiba za nchi zao wakati huo, hao marais wawili walikuwa na haki kuingiza nchi zao katika mkataba wowote. Mnadai Baraza la Mapinduzi halikuridhia Muungano? Mbona Babu na Khamis Abdallah Ameir wamekiri kuwa ulijadiliwa katika Baraza na kukubalika baada ya Abdallah Kassim Hanga kuutetea kwa nguvu zake zote? Hanga huyo huyo mliokuja mnyonga baadae! Mnasahau kuwa mlikuwa na chama chenu cha ASP na ni kwa ridhaa yenu wenyewe mkakitosa na kukubali kuungana na TANU kuunda CCM mwaka wa 1977. Leo mnadai kubururwa na CCM, hamkuona hilo mlipoimba ngonjera kufurahia kifo cha ASP? Mnasahau kuwa hata katika kamati ya Nyalali, kwenye suala la Muungano ni wazanzibari watatu tu katika 11 waliotaka muundo wa serikali tatu na saba walitaka muundo uliopo uendelee. Wakati huo, watanganyika 9 kati ya 11 walitaka serikali 3 na ni wawili tu walitaka muundo wa sasa uendelee. Hao wenzenu si walijua maslahi wanayopata kutokana na muundo wa sasa na kama alivyosema Pinda, hasara mtakayopata ukivunjika ( na kila mmoja anajua kuwa muundo serikali tatu ni kituo tu katika safari ya kuvunja Muungano)!

Uvumilivu una mwisho na Pinda amewaambia msichotaka kusikia. Kama hamna haja na Muungano si heri mseme wazi badala ya kuendeleza malumbano yasiyo na tija. Si mna uwakilishi katika Bunge? Kwa nini maneno haya msiyasemee huko badala ya kubakia ambako hao mnaowabeza hawako?

Shule kweli muhimu. Msome hapa Profesa Othman aliyosema kuhusu huu Muungano http://www.kongoi.com/forty-years-of-the-union-is-it-withering-away-by-prof.-haroub-othman-2.html . Na yeye hakuwatakia mema?

Nilikuwapo.

Amandla................

I am not of such inhuman characters.
"I was the justest judge that was in England these last fifty years. When the book of all hearts is opened, I trust I shall not be found to have the troubled fountain of a corrupt heart. I know I have clean hands and a clean heart. I am as innocent of bribes as any born on St Innocents Day." Sir Francis Bacon.


Unaposema "iliingia kwa hiari yake" sina hakika kama neno la kiswahili "hiari" lina maana pana kama neno kama hilo katika lugha yako ya kwanza ya kikabila.

Hakuna popote katika kumbukumbu za Baraza la Mapinduzi lilipokaa na kupitisha kauli za kuridhia Muungano. Hata Mh. Jumbe ambaye alikuwa ndo mshauri mkuu wa Karume hakuwa na habari ya maafikiano kati ya Karume na Nyerere, kwa kauli yake mwenywe Jumbe (yupo na aitwe aulizwe au maandiko yake yaletwe hapa kwa rejea) anasema wakati anarudi katia ziara ya kikazi kutoka Pemba alikutana na Karume Ikulu na kumhabarisha kuwa yeye Karume ameshakubaliana na Rais Wa tanganyika kuunganisha nchi zao kuwa jamhuri, na kumtaka yeye Jumbe akubali, Hapa pana Baraza gani la Mapinduzi lililokaa ambalo Jumbe asihusike katika kupitisha uamuzi mzito kama huo.

Tena Jumbe anaendelea kusimulia kuwa wakati anatoka uwanja wa ndege anakwenda kisiwandui aliwakuta akina Bhoke Munanka, Rashidi Kawawa na timu yao, ndo kwanza wanamaliza mazungumzo na karume, na wao kumtaka Jumbe akikutana na Mzee Karume asiache kusisitiza akubali mipango yao ya kuungana, hili ndo unaliita ww baraza la Mapinduzi?

Nyerere kwa kauli yake mwenyewe anasema kuwa alipomwendea Karume kwa shauri la kuunganisha nchi, Karume alikubali bila kufikiri na kama utakumbuka hotuba ile (J.Chisano alikuwapo wakati Mwalimu akisema hivyo) alimalizia akasema kuwa "...Karume mwanamme bwana..."

Ridhaa ya wazanzibar ilivyotafutwa na kumbukumbu zipo ni mkutano wa hadhara alioutisha Karume katika viwanja vya Maisara Suleiman, na kuwauliza wananchi aliowaita yeye kuwa "..wanawakilisha mikoa yote ya Zanzibar..." kuwa kama wapo tayari Jamhuri ya Zanzibar iungane na tanganyika na watu woote hapo wakaitikia ndiyooo, nani angebisha?? Hilo ndiyo unaloliita baraza la Mapinduzi???

Hakuna " hansard" wala "minutes" za kikao cha Baraza la Mapinduzi zinazoonyesha wajumbe walikutana wapi, wangapi, agenda, maazimio,kura, waliokubali, waliokataa n.k kwako ww hiii ndo ridhaa????

Yaliyotokea ni akina Mfaranyaki na Twala, akiwamo na Okello kumbishia Karume asifanye pupa la kuunganisha nchi kwanza. Mfaranyaki alipoleta kubisha zaidi akaambiwa kwanza Zanzibar si kwao akiendelea kidomo domo atarejeshwa kwao unengerekoni, akaufyata, kadhalika na Okello, nawenzake n.k na kilichowakuta watu hawa kinajuulikana katika historia ya muungano.

Na kama unavyotaka watu waamini kuwa kuungana huku hakuna hila basi kwanini Karume amfukuze Dourado katika wakati ambao anahitajika na kwanini Nyerere akamfukuza Bashir Swanzy katika wakati ambao uhalali wa muungano unatafutwa?

Kama Jumbe alijuwa kuwa muungano huo una ridhaa ya baraza la Mapinduzi kwa nini alimfukuza Damian Lubuva{mwanasheria mamluki aliyeletwa na Nyerere Zanzibar} na kumrejesha tanganyika na Jumbe kuandika "petition" katika mahakama ya katiba kuhoji uhalali wa Muungano, si angekuja na makubaliano ya baraza la mapinduzi tu kuweka sawa palipokosewa kama walivyokubaliana, je hapa hapotoshi kuthibitisha kuwa Muungano huu ni wa kichochoroni, kati ya Nyerere na Karume tu?

Kama Nyerere hakuwaburuza wazanzibar katika muungano kwanini hakukubali kuwapa fursa kuhoji uhalali wake ili wananchi wajiridhishe kuwa kinachofanyika ni sahihi kwa ridhaa zao na taratibu zao, na badala yake akatengeneza majasusi wakaipora "petition" ya Jumbe kabla hata kufika kwa mrajis wa Mahakama kuu, na kumfikia yye Nyerere. Kwanini hili isiwe hoja kuwa Nyerere aliwan'ga'ngania wazanzibar kwa kuwakataza hata kuhoji muungano na kufukuza rais wao, mbona hakuwataka warudi Baraza la mapinduzi kupitisha shauri la kumuondoa rais ambaye baraza hilo ndilo lililomteua.

Hapa unatwambia uwongo wako kuwa eti Nyerere alishinikiza Jumbe achaguliwe kwa kuwa hakuwa akikubalika na Baraza la Mapinduzi, kumbukumbu zipo kuwa baaada ya Karume Kutangazwa amefariki, Baraza la Mapinduzi lilikutana na kumteuwa Jumbe ambaye alikuwa msaidizi nambari moja wa Mzee Karume na ndiye aliyetoa tangazo la serikali rasmi kuhusu kifo cha Mzee Karume na uamuzi wa Baraza la Mapinduzi kumteua yye rais kwa muda, wakati gani Nyerere alifanya mchakato wa ushawishi katika hali tete kama hiyo. Huo ni uwongo.

Nani kachangia mauwaji holela na kumpa kichwa cha kufanya atakavyo karume kama si Nyerere? Karume alipokuwa akiwashughulikia anaowaita maadui wa Muungano, niNyerere unaedai hakulazimisha muungano aleinyamaza kimya bila kuhoji kitu, kwakuwa ushetani wake ulikuwa unalindwa kwa mkono wa chuma, iweje Makamo wa rais wa Jamhuri anauwa watu ww bosi wake uwe hujuwi au usiwe dhamana na hili(On the same principle of vicarious liability that the act of the servant is the act of the master) na ndo yeye Nyerere bila ya aibu, utu, huruma wala soni kwa Mungu wake, aliyewakabidhi Hanga na Mzee wetu Othaman Shariff wakauliwa Zanzibar(assessory after the fact) nayeye Nyerere pia muuwaji.

Leo unaniletea hadithi za white paper ndugu yangu mm nilishiriki mwaka 1998 kisiwandui na katika matawi mbalimbli ya chama, kuandika maoni ya kubuni kwa niaba ya CCM kujidai kuwa Muungano wa serikali mbili uendelee bila kujuwa kuwa natumiwa kulinda maslahi ya wachache. (Naujutia muda ule mpaka leo na maisha nitakuwa mpinzani kulipa dhulma ile). Takwimu hizi bandia za nini kuzitegemea ww???

Nani kashawishi ASP na TANU ziungane? unajuwa jinsi Mzee Thabit Kombo Jesha alivyolia kwa kwi kwi kama mtoto mdogo ASP ilipouliwa kwa "ushawihsi wa kibabe" wa Nyerere na "ulevi" wa Jumbe tu?

Unanambia Mar. Prof. Haroub Othman kasema na kama na yeye hakuwa katutakia mema. Kusema ndugu kila mtu anasema ni uhuru wake kusema, kuandika, lakini Othmnan alikuwa Prof. hakuwa Mtume au Nabii kuwa alichokisema na kuandika ndo maagano na amri za lazima kufata, hayo yalikuwa ni mawazo yake, na tulikuwa tukitofautiana kistaarabu pale kituoni kwake siku hizo na yeye wakati mwengine hukiri kuwa kuna mambo yamekosewa na yanaleta matatizo sasa. Hii haimaanishi kuwa msimamo wa wazanzibar wote kuwa na muungano wa haki siyo sahihi!

Bado tutaendelea kudai kuwa Muungano huu wa dhulmau urekebishwe na kama haiwezekani kurekebishwa tusiumizane vichwa wala tusitishane kila upande utazame maslahi yake bas.

J,
 
Last edited:
teh pinda kawaapiga kamkwara..anayetaka kuvunja muungano avunje ..aone itakuwaje???....mwaka huu watamwandama kweli!!!
 
huyu jumbe mara aiwe shujaa wa kufungua petition ...mara alaumiwe..maneno mengi tu!!..afteral huyu jumbe siku zote amekuwa akilala bara tangu akiwa rais...na hata marais wakiomfuata....

...na hata sasa yupo pale kigamboni ...hajapata kulala zaizibar tangu aondoke....urais!!..hata enzi zile ana nguvu akienda shereheni ...anarudi na boti ya jioni!!
 
Thank you Junius, Tafadhali usichoke kuwasomesha hawa kwani mioyo na akili zao zimeshapigwa muhuri kuamini kila alichokifanya / alichokisema huyo Nyerere wao ndio sahihi. Nyerere anajulikana kua ndiyo master mind wa most of the znz killings without any doubt. Nina hakika alichokiandika Fundi wa macho ni just copy and paste, let him know that anajadiliana na watu wanao andika kwa kujiamini na wenye kujua history na most Nyerere's propagandas.
 
Mimi ni admin wa mzalendo.net ambayo ni community website ya wazanzibari, tumepiga kura ya maoni juu ya muungano huu, na haya ndio maoni ya wapiga kura 80 (Clean votes hakuna mtu aliepiga zaidi ya mara moja):


  1. 46% hawataki muungano kabisa, wameshachoka kuburuzwa na kupotezewa utaifa wa visiwa vyao.
  2. 42% wanataka Serekali 3, Tanganyika, Zanzibar na Serekali ya Muungano.
  3. 7% hawataki mabadiliko wameredhika kabisa 🙄
  4. 5% wanataka serekali 4, Tanganyika, Unguja, Pemba na Muungano..
Suala la moja bila genocide ya kuwauwa wazanzibari wote, naona kama haiwezekani....suali muhimu kuna ulazima wa Tanganyika kumwaga damu kuhakikisha kuwa muungano unadumu?...😕

Aaaagh I forgot this was Pinda && Tanganyika's day dreams!

Cheers
Hawa wenzetu Wa-danganyika wao huita kura ya maoni wanapokutana Dodomaa na akasimama Makamba kwa uhuni na ubabe alioupata jeshini baadae akauliza " Nani hataki muungano" sasa hapo unategemea jibu gani ?
Wa zenji walipotaka kuungana na kuundwa serikali ya mseto, waliambiwa waite kura ya maoni, mbona hatujasikia kuitwa kura hiyo kwa mambo ya huu udhulumaji uitwao muungano ?
 
Mimi ni admin wa mzalendo.net ambayo ni community website ya wazanzibari, tumepiga kura ya maoni juu ya muungano huu, na haya ndio maoni ya wapiga kura 80 (Clean votes hakuna mtu aliepiga zaidi ya mara moja):


  1. 46% hawataki muungano kabisa, wameshachoka kuburuzwa na kupotezewa utaifa wa visiwa vyao.
  2. 42% wanataka Serekali 3, Tanganyika, Zanzibar na Serekali ya Muungano.
  3. 7% hawataki mabadiliko wameredhika kabisa 🙄
  4. 5% wanataka serekali 4, Tanganyika, Unguja, Pemba na Muungano..
Suala la moja bila genocide ya kuwauwa wazanzibari wote, naona kama haiwezekani....suali muhimu kuna ulazima wa Tanganyika kumwaga damu kuhakikisha kuwa muungano unadumu?...😕

Aaaagh I forgot this was Pinda && Tanganyika's day dreams!

Cheers

Nadhani haujui sampling ni nini. Katika watu milioni moja(population ya Z'bar) uta chukuaje maoni ya watu 80 kama maoni ya wazanzibar? Kura ya huo mtandao wako hauna maana yoyote kwa maana it is not representative of the population.Kura yako is about 0.008% ya population ya Z'bat so can you really take that seriously? Na hata hao watu 80 there is no way you can prove to us that wote ni wazanzibar(again fault in the sampling).

I sure hope opinions za watu huko Z'bar hazipo influenced na statistics kama hizi.
 
Eeh bwana msimalaumu mheshimiwa sana maana kuna mambo mtu unaweza ukastahamili kwa kukaa kimya lakini inafika wakati inabidi ubwatuke
Hawa jamaa ni sawa na mtu aliye katika tawi la mti analipiga msumeno kwenye shina cha tawi inabidi waambiwe ukweli.

Mimi siyo mtaalam lakini kwa hesabu za upesi upesi tu ni kuwa ndugu zetu hawa ambao hivi sasa wanaishi huku bara ni wengi kuliko walio kisiwani. Watu wa bara walioko kisiwani ni ndogo sana.
Wenzetu hawa wanafaidi matunda ya muungano kuliko sisi lakini kila siku ni kulalamika tu. Kwa vile mimi ni muota njozi za mchana ninaruhusiwa kuota kisheria natarajia baada ya waraka huu nitavuta njozi ya kuota tawi linakatika matokeo ya kukatika kwa tawi hili nitawaarifu baada ya kuamka
 
Zanzibar tatizo ni kero za maisha sio za muungano, wanashindwa kugundua baina ya tatizo la muungano na tatizo la maisha, iwapo watapata ufumbuzi wa kero za maisha hakuna kero za muungano, SMT wajaribu kusaidia kutatua kero za maisha kule Zanzibar hatutosikia tena kero za muungano
Ni kweli kabisa shida ya Muungano ni ugumu wa maisha unaosababishwa na ufisadi wa serikali ya CCM inafikia hatua hata huku tanganyika itafikia kipindi lazima kieleweke bado kidogo tu maana hatuwezi kuendelea kuona wachache wanaishi maisha ya anasa wengine tukitamani kujishibisha kwa mabaki ya mezani kwao maana mali asili zote za bara wameuza hakuna faida yoyote kwa taifa bora wazanzibari washughulikie mafuta yao
 
Kwa kuanzia wafanyakazi wote Wa Tanzania walipwe mishahara sawa- kwa kazi moja bila upendeleo!

Kwa nini mwal. primary Visiwani alipwe mshahara kidogo kuliko bara? Huu ni uungwana?

Je kweli hii ni nchi moja?
 
Kwa kuanzia wafanyakazi wote Wa Tanzania walipwe mishahara sawa- kwa kazi moja bila upendeleo!

Kwa nini mwal. primary Visiwani alipwe mshahara kidogo kuliko bara? Huu ni uungwana?

Je kweli hii ni nchi moja?

Mwalimu wa primary visiwani ana lipwa kiasi gani na mwalimu wa primary bara analipwa kiasi gani?
 
Asante sana Fundi Mchundo na kwa kuongezea Profesa Othman anasema hivi,
Ni hayo malalamiko yasiyo na msingi yaliyomfanya Mwalimu Nyerere kuyaita ya kijinga na kumkemea Raisi wa Zanzibar, Salmin Amour kwa maneno yanayofanana na haya (samahani the quote may not be exact)
Kaazi kweli kweli !

Namuheshimu sana Professa Othman lakini hayo yalikuwa maneno yake na ya wakati fulani. Tulishuhudia mabadiliko ya mtazamo wake kipindi kilichofuata baada ya maneno hayo.
Inawezekana kwa mujibu wa Elimu yake tukayapa hadhi maneno yake lakini hayo yalikuwa ni mtizamo wake kwani unaposema zanzibar unamaanisha kiongozi au wananchi? Hebu tuangalie ni sehemu gani au ni document gani inayoonyesha ushahidi kuwa Wazanzibari walishirikishwa katika hiyo Hiari anayozungumza Profesa Othman(marehemu)? Au kwa ufahamu wako kuwa kiongozi ndio wananchi iweje ubeze matakwa ya Dr Salmin Amour ambaye naye alikuwa ni Rais wa Zanzibar kama alivyokuwa Karume alieitia Z'bar kwenye Muungano?
Zaidi ya hivyo Binaadamu ana haki ya kubadili kitu pale kinapokuwa hakina faida naye tena na kwa mantiki hiyo Wazanzibari wana haki ya kudai mfumo wanaouona utaokuwa na Faida kwao, kwani Si tulifuta Azimio la Arusha, Ujamaa na kujitegemea, Chama kimoja na mengi mengine ambayo tuliyaona kuwa ni matukufu hapo kabla?
 
huyu jumbe mara aiwe shujaa wa kufungua petition ...mara alaumiwe..maneno mengi tu!!..afteral huyu jumbe siku zote amekuwa akilala bara tangu akiwa rais...na hata marais wakiomfuata....

...na hata sasa yupo pale kigamboni ...hajapata kulala zaizibar tangu aondoke....urais!!..hata enzi zile ana nguvu akienda shereheni ...anarudi na boti ya jioni!!

Na nyumba yake aliita "Mtu kwao". kuwapiga kejeli wale waliomsulubu kwa kutetea Zanzibar baada ya kuona kuwa alitegwa na nyerere.

Pengine unaweza ukafahamu kwanini anakuwa wakati shujaa na wakati ni msaliti.
Msaliti kwa kuzani kuwa akipeleka Zanzibar kwa jamaa zake atapata utambuzi zaidi kutoka kwa jamaa zake.

Shujaa kwa vile alikuwa tayari kujisawazisha baada ya kuona makosa yake.
 
Eeh bwana msimalaumu mheshimiwa sana maana kuna mambo mtu unaweza ukastahamili kwa kukaa kimya lakini inafika wakati inabidi ubwatuke
Hawa jamaa ni sawa na mtu aliye katika tawi la mti analipiga msumeno kwenye shina cha tawi inabidi waambiwe ukweli.

Mimi siyo mtaalam lakini kwa hesabu za upesi upesi tu ni kuwa ndugu zetu hawa ambao hivi sasa wanaishi huku bara ni wengi kuliko walio kisiwani. Watu wa bara walioko kisiwani ni ndogo sana.
Wenzetu hawa wanafaidi matunda ya muungano kuliko sisi lakini kila siku ni kulalamika tu. Kwa vile mimi ni muota njozi za mchana ninaruhusiwa kuota kisheria natarajia baada ya waraka huu nitavuta njozi ya kuota tawi linakatika matokeo ya kukatika kwa tawi hili nitawaarifu baada ya kuamka

Bwana mdogo unaweza kuorodhesha hizo faida na tuzijadili tuone kama kweli Wazanzibari wanyamaze kimya kwani huenda faida hizo wakazikosa?
 
Mwalimu wa primary visiwani ana lipwa kiasi gani na mwalimu wa primary bara analipwa kiasi gani?

MwanaFalsafa1,

1. Mwal. 1st Appoitment Bara 180,000 (Net) wakati visiwani ni 120,000 (net).

2. Nesi akiajiriwa bara 250,000 (net) wakati Visiwani ni 120,000 (net).

3. Daktari 1st appointment Bara 700,000..viswani 250,000


Wakati Nesi, daktari na Mwalimu anamhudumia Mtanzania huyo2!

Je huu ni uungwana??

Na tunasema tuko ktk nchi moja??
 
Mg3,
Ha, ha, ha, ha, maneno mazito haya. Kwangu mimi huyu Kheri ni muhuni tu, kama yeye anajiamini saana na yuko kwenye kamati kuu ya CCM, kwa nini asisubiri kwenye kamati kuu amvulie uvivu Pinda? Kama kweli wazanzibar wameamua wanaogopa nini kusema hatutaki muungano? Mnakumbuka hotuba ya JK kwa wabunge wakati alipokuwa anaelezea kuhusu kama zanzibar ni dola au lahh, aliwapasha tena na kuwaambia zanzibar si dola kwa nchi za nje, na akawaambia tatizo nini kama kuna kitu si waseme tu. Wazanzibar kuweni open hamna anayewazuia, na mnatakiwa mjue wabara sasa wamechoka na kelele za kike za jikoni.

Tumekuwa tukishuhudia majigambo na maneno ya kejeli tu lakini hoja ni chache na zinapotokea zinakuwa dhaifu. Unajua sababu ni nini/ Sababu ni kuwa Wazanzibari wana hoja za haki kwa hivyo jitahidini vipi mtajikuta mnajiumbua. Hili ndilo linalomkabili Pinda na viongozi wengine wa Bara wakiwemo Wabunge. Wazanzibari wanasimamia haki yao wakati kina Pinda wanasimamia ubabe kwa kutumia Katiba lakini Katiba yenyewe inawapa haki Wazanzibari. Katiba inaposema kuwa Tanzania ni Muungano wa zilizokuwa Jamhuri mbili zilizo huru inamaliza utata wote.
Zanzibar kama sehemu moja ya Muungano ina haki yakuamuwa sio kulazimishwa na bahati mbaya wengi HAWALIELEWI HIlo. Walitawaliwa sasa wanataka watawale wao na bahati mbaya Binaadamu hakuumbwa atawaliwe maisha na Zanzibar imefika wakati wake kujinasua na mfumo wa kutawaliwa.
 
mimi naamini kila mtu ambaye ni rai wa Tanzania anahaki ya kuhoja kila kitu na hasa maswala muhiyo nayo defini future yake na kizazi chake kijacho.
Viongozi kama Pinda na wabunge hawapaswikutoa majibu ya KIBABE na kitisho kama ''eti muungano univunjika nani ataumia'' badale yake watoe majibu sahii ya kutoa nafasi watu kufanya analysis ya kina juu ya future ya nchi
Mimi naamini hakuna wengi wanataka kuona muungano ukiishi milele lakini kikubwa ni ANINA (KIND) ya muungano ndio mjadala na hilo watawala hawataki lizungumiziwe ndoo maana wana-push ili wale anaohoji aina yakuungano waonekane kama wanataka mungano uvunjike ambayo ambapo si kweli
(ungumu wa masha,ahadi za uongo na ainaya muungano ndio mjadala)
 
MwanaFalsafa1,

1. Mwal. 1st Appoitment Bara 180,000 (Net) wakati visiwani ni 120,000 (net).

2. Nesi akiajiriwa bara 250,000 (net) wakati Visiwani ni 120,000 (net).

3. Daktari 1st appointment Bara 700,000..viswani 250,000


Wakati Nesi, daktari na Mwalimu anamhudumia Mtanzania huyo2!

Je huu ni uungwana??

Na tunasema tuko ktk nchi moja??

Thanks for the info mkuu. Je hizo ajira za ualimu na unesi/udaktari kwa upande wa Z'bar zina shugulikiwa na serikali ya Muungano au SMZ?
 
SALIM SAID SALIM
BINADAMU si malaika. Kuna kipindi huteleza na kufanya makosa. Anapofanya hivyo binadamu wenzake wenye utu, wema na hisani hutakiwa kumuonea huruma mwenzao aliyeanguka kwani kila mmoja wao huenda siku moja naye akateleza.
Waswahili wanasema mwenzako akianguka msaidie kumuokota aweze kusimama, ili nawe utapoanguka upate kiumbe wa kukuokota.
Lakini pale unapoona mtu anajiangusha kwa makusudi, basi ni vyema ukamueleza waziwazi kuchoshwa kwako na kumuokota, kwa vile kuna kipindi nguvu za kufanya hivyo zitakusekana na utakapojitahidi misuli huenda ikagoma kufanya kile unachokitaka.
Hivi karibuni limekuwa ni jambo la kawaida au mara kwa mara kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuteleza, kuanguka au kujiangusha labda akiamini kila mizegwe anaweza kufanya kwa kutoa kauli za ajabu ambazo mimi ninavyoziona hazina kichwa wala miguu.
Baadhi ya wakati hujiuliza hivyo kweli huyu Waziri Mkuu wetu ni Mtanzania? Au ndiyo anauruka ukweli kwa kuwa anatoka Rukwa? Au ndiyo ni katika jitihada zake za kupindisha mambo ili mizengwe ionekane kweli?
Nimekuwa karibu na viongozi wengi wa nchi hii, wa Bara na Visiwani, kwa miaka mingi, tangu Waziri Mkuu akiwa shule. Tumezungumza mengi na nimewasikia wakizungumza mengi, baadhi yao ya siri. Lakini kama yupo kiongozi anayenishangaza ni huyu Mizengo Pinda ambaye ninaona anafanya mizengwe na kupindisha mambo.
Hivi karibuni amejibu hoja za Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi waliokuwa wakisema hawataki tena kuona suala la mafuta kuwa la Muungano. Kauli hii haikumfurahisha na kuwaeleza waliotamka hayo kuwa wanafanya chokochoko.
Si hayo tu, Mizengo Pinda alifanya mizengwe ya aina yake na kutoa kauli ambayo hata siku moja sijawahi kuisikia kutoka kwa kiongozi yeyote wa juu wa nchi hii. Nayo ni kusema Muungano ukivunjika Zanzibar ndiyo itakayopata hasara. Wapi alipata ujabari wa kutoa kauli hii, sijui. Kama alifanya utafiti ni vema pia akatueleza.
Masikini Pinda anapindisha mambo. Suala hapa ni kwa Zanzibar kukataa mafuta kuwa suala la Muungano na kudai kuwa liliingizwa katika orodha ya mambo ya Muungano kinyemela. Kama madai haya ni sahihi au upotoshaji ni suala la mjadala na kujengewa hoja yenye maelezo ya kina.
Ni vema tukaambiwa kuwa Wawakilishi wa Zanzibar hawana haki kusema hayo kikatiba. Kama ndiyo hivyo Pinda aeleze kuwa Wazanzibari, pamoja na Wawakilishi wao hawana haki ya kutoa maamuzi juu ya masuala ya Muungano.
Anachoamini Pinda - sijui kapata wapi takwimu za kutoa kauli hiyo - kuwa Zanzibar ndiyo inayofaidika zaidi kwa kuwapo kwa Muungano na ukivunjika hasara kubwa itawaendea watu wa visiwani.
Naamini Pinda ndiye aliyepata hasara kwa vile hazijui hisia za Wazanzibari juu ya namna Muungano unavyoendeshwa. Kwa taarifa yake Wazanzibari hawakushirikishwa (hajashauriwa) ulipoundwa.
Kwa taarifa yake Wazanzibari wengi, bila kujali kama ni wanachama wa CCM au CUF, hawaridhiki na shughuli za Muungano zinavyoendeshwa. Wapo wanaoamini kwamba Muungano, hasa wa vyama vya ASP na TANU, ndiyo uliowaletea balaa kwa vile hata viongozi wana-CCM wa visiwani huona wanafaa kuongoza Zanzibar huwekwa upande na Bara kuwachagulia watu wa Visiwani viongozi wa kuongoza.
Ni vizuri kama Pinda hajui mambo yanavyopindishwa kufikia hali hii, apitie kumbukumbu za vikao vya CCM, hasa wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi.
Suala la mafuta na hizo chokochoko za Muungano ambazo Pinda anazizungumzia hazitoi taswira yoyote ile nyingine isipokuwa uwepo wa mgogoro wa katiba. Wazanzibari wanataka suala hili liwe chini ya mamlaka yao kama ilivyo kwa dhahabu na almasi kwa Bara, na hili ndio ningelimtarajia Waziri Mkuu kulizungumzia na si kupindisha mambo.
Kama walichofanya Wawakilishi ni dhambi, kwa nini haikuwa dhambi kwa Bara kufanya madini yake si ya Muungano? Au Zanzibar haina haki kudai kumiliki mafuta yaliyopo kwenye ardhi na bahari yake?
Kutaka mafuta yawe chini ya mamlaka ya Zanzibar ni kutaka kuvunja Muungano, lakini kwa dhahabu na almasi kuwa ya Bara si kuvunja bali kuimarisha Muungano. Makubwa haya, labda kama kule Rukwa ndivyo wanavyoelewa mantiki ya aina hii.
Hili Pinda analazimika kulitolea maelezo na si kupindisha mambo na kutufanyia mizengwe kwa kutoa kauli za vitisho na kusimanga (kunyanyapaa) watu. Wazanzibari hawataki kuabudiwa, lakini wanataka kuheshimiwa. Wao ni wadau wa Muungano na wanayo haki ya kutoa mawazo na maamuzi.
Suala la nani anafaidika zaidi na Muungano ni zito, refu na pana. Jawabu lake halipatikani kwa mizengwe, propaganda, kwa kauli au kupindisha mambo. Ni suala linalohitaji utafiti wa kina.
Lilio muhimu ni kukubali kwamba Muungano sasa unapanda mwamba na ukifanyiwa mchezo utazama. Hii ni kwa sababu Wazanzibari wanaamini hisia zao na maamuzi yao hayatiliwi maanani na watu kama Mizengo Pinda. Badala yake wanasukumiwa makombora na kushutumiwa kuwa wachochezi kama vile hawana haki ya kutoa maoni au kufanya maamuzi juu ya mwenendo wa Muungano.
Wakati umefika kwa kila upande wa Muungano kuheshimu kauli na mawazo ya upande wa pili. Wazanzibari wamesema si mara moja wala mbili, hawataki suala la mafuta liwe la Muungano kama ilivyo kwa almasi na dhahabu na madini mengine.
Kwa nini ionekane kuwa nongwa na kufuru? Kama kuvunjika kwa Muungano kutakuwa na hasara zaidi kwa Zanzibar kwa nini tusianzie basi na hasara kuonekana kwa hili suala mafuta ili tuone hasara itayopata Zanzibar?
Tukitaka au tusitake huu Muungano una matatizo na hata Pinda akijaribu kuupindisha ukweli matataizo yataendelea kujitokeza. Njia pekee ya kupata ahueni ni kwanza kukubali ukweli kwamba upo mgogoro na sio kutoa kauli za kutishana.
Zama za kutishana zilishapita, sasa ni zama za ukweli na uwazi, Pinda hata atumie vitisho vya aina gani hawezi kulipindisha kwani wakati wa kufanya hivyo umepita.
Watanzania tuamke. Muungano wetu una matatizo na wakubwa wanaonekana hawataki kuyaona. Tuwafumbue macho na tuwatoe tongo zinazowaziba macho, kama si kwa mikono basi kwa kuwafanyia upasuaji.
Jahazi letu linakwenda mrama na tuliowapa unahodha wa kuliongoza katika safari yetu, ambayo sasa imekumbwa na dhoruba wanaonekana hawataki au hawana ustadi wa kulivusha jahazi hili salama katika dhoruba hii.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi, Idumu CUF. Idumu CHADEMA. Idumu NCCR-Mageuzi. Idumu TLP na vidumu vyama vingine vyote vya siasa. Wadumu wa Tanzania - waliopo Bara na wale wa Visiwani. Tanzania ni moja lakini ni sehemu mbili – Bara na Visiwani - fikra nyingi na vyama vingi vya siasa. Tuache kupindisha mambo na badala yake tujitahidi kuyaweka sawa kwa hekima na busara na sio vitisho kama vya Mizengo Pinda.

SOURCE: TANZANIA DAIMA
 
Back
Top Bottom