Hivi ni wewe, Marcus JUNIUS Brutus, uliyemsaliti Julius Caesar aliyekupenda kama mwanae hasa ukizingatia uhusiano wake na mama yako Servilia Caepionis? Au ni wewe Francis Bacon, Attorney General aliyemtosa rafiki yake kipenzi Robert Devereux, Earl wa Essex katika kutaka kujikomba kwa Malkia Elizabeth?
Leo hii unaubeza Muungano ambao serikali ya Zanzibar na Pemba iliingia kwa hiari yake? Unamlaumu Nyerere ambae ndiye pekee aliyempokea na kumpa hifadhi Sayyid Sir Jamshid Bin Abdullah Al Said na waziri mkuu wake Muhammad Shamte Hamadi alipokimbia kwenye meli yake iliyoitwa Seyyid Khalifa? Huyo huyo Nyerere aliyewaondolea John Okello ( raia wa Uganda ambae alitokea Pemba wakati wa Mapinduzi na alikuwa mwanachama wa ASP) ambae alitaka kuendeleza mtindo wa chinja chinja? Leo kweli mnambeza?
Unasahau kuwa hiyo nchi iliyoingia kwenye muungano na Tanganyika ni Jamhuri ya Zanziba na Pemba (sio Zanziba kama unavyotaka kutuambia) na kuunda serikali ya Tanganyika na Zanziba ambayo miezi sita baadae ikajiita Jamhuri ya Muungano ya Tanzania! Unasahau kuwa wakati mnapigiwa ving'ora, mnalazimishwa kuolewa na weusi wa huko kwenu mlipokewa na kupewa hifadhi huko mnakokulaani hivi sasa? Hata pale mlipomuua Rais wenu wa kwanza ni Nyerere huyo huyo aliyekataa kuwakabidhi wakina Abdurahman Babu akijua mlichotaka kuwafanyia. Ni Nyerere huyo huyo aliyewapatia mwokozi wenu Jumbe ambae hakuwa na ufuasi mkubwa katika Baraza la mapinduzi.
Mnasema hamkuridhia Muungano na ati Nyerere aliwarubuni! Unasahau ni Rais wenu ( ambae hakuenda shule) ndiye aliyempa likizo ya wiki moja Attorney General wake Wolfgang Dourado na kufuata ushauri wa mganda Dan Nabudere badala yake? Mwenzake alimtumia AG wake Roland Brown kuhakikisha maslahi ya upande wake. Hapa nani alaumiwe? Na ni Nyerere huyo aliyekataa Muungano wa jumla akisisitiza kuwa identity ya Zanzibar ni lazima ilindwe! Leo amekuwa muovu? Mnasahau pia kuwa kikatiba za nchi zao wakati huo, hao marais wawili walikuwa na haki kuingiza nchi zao katika mkataba wowote. Mnadai Baraza la Mapinduzi halikuridhia Muungano? Mbona Babu na Khamis Abdallah Ameir wamekiri kuwa ulijadiliwa katika Baraza na kukubalika baada ya Abdallah Kassim Hanga kuutetea kwa nguvu zake zote? Hanga huyo huyo mliokuja mnyonga baadae! Mnasahau kuwa mlikuwa na chama chenu cha ASP na ni kwa ridhaa yenu wenyewe mkakitosa na kukubali kuungana na TANU kuunda CCM mwaka wa 1977. Leo mnadai kubururwa na CCM, hamkuona hilo mlipoimba ngonjera kufurahia kifo cha ASP? Mnasahau kuwa hata katika kamati ya Nyalali, kwenye suala la Muungano ni wazanzibari watatu tu katika 11 waliotaka muundo wa serikali tatu na saba walitaka muundo uliopo uendelee. Wakati huo, watanganyika 9 kati ya 11 walitaka serikali 3 na ni wawili tu walitaka muundo wa sasa uendelee. Hao wenzenu si walijua maslahi wanayopata kutokana na muundo wa sasa na kama alivyosema Pinda, hasara mtakayopata ukivunjika ( na kila mmoja anajua kuwa muundo serikali tatu ni kituo tu katika safari ya kuvunja Muungano)!
Uvumilivu una mwisho na Pinda amewaambia msichotaka kusikia. Kama hamna haja na Muungano si heri mseme wazi badala ya kuendeleza malumbano yasiyo na tija. Si mna uwakilishi katika Bunge? Kwa nini maneno haya msiyasemee huko badala ya kubakia ambako hao mnaowabeza hawako?
Shule kweli muhimu. Msome hapa Profesa Othman aliyosema kuhusu huu Muungano http://www.kongoi.com/forty-years-of-the-union-is-it-withering-away-by-prof.-haroub-othman-2.html .
Na yeye hakuwatakia mema?
Nilikuwapo.
Amandla................
I am not of such inhuman characters.
"
I was the justest judge that was in England these last fifty years. When the book of all hearts is opened, I trust I shall not be found to have the troubled fountain of a corrupt heart. I know I have clean hands and a clean heart. I am as innocent of bribes as any born on St Innocents Day." Sir Francis Bacon.
Unaposema "iliingia kwa hiari yake" sina hakika kama neno la kiswahili "hiari" lina maana pana kama neno kama hilo katika lugha yako ya kwanza ya kikabila.
Hakuna popote katika kumbukumbu za Baraza la Mapinduzi lilipokaa na kupitisha kauli za kuridhia Muungano. Hata Mh. Jumbe ambaye alikuwa ndo mshauri mkuu wa Karume hakuwa na habari ya maafikiano kati ya Karume na Nyerere, kwa kauli yake mwenywe Jumbe (yupo na aitwe aulizwe au maandiko yake yaletwe hapa kwa rejea) anasema wakati anarudi katia ziara ya kikazi kutoka Pemba alikutana na Karume Ikulu na kumhabarisha kuwa yeye Karume ameshakubaliana na Rais Wa tanganyika kuunganisha nchi zao kuwa jamhuri, na kumtaka yeye Jumbe akubali, Hapa pana Baraza gani la Mapinduzi lililokaa ambalo Jumbe asihusike katika kupitisha uamuzi mzito kama huo.
Tena Jumbe anaendelea kusimulia kuwa wakati anatoka uwanja wa ndege anakwenda kisiwandui aliwakuta akina Bhoke Munanka, Rashidi Kawawa na timu yao, ndo kwanza wanamaliza mazungumzo na karume, na wao kumtaka Jumbe akikutana na Mzee Karume asiache kusisitiza akubali mipango yao ya kuungana, hili ndo unaliita ww baraza la Mapinduzi?
Nyerere kwa kauli yake mwenyewe anasema kuwa alipomwendea Karume kwa shauri la kuunganisha nchi, Karume alikubali bila kufikiri na kama utakumbuka hotuba ile (J.Chisano alikuwapo wakati Mwalimu akisema hivyo) alimalizia akasema kuwa
"...Karume mwanamme bwana..."
Ridhaa ya wazanzibar ilivyotafutwa na kumbukumbu zipo ni mkutano wa hadhara alioutisha Karume katika viwanja vya Maisara Suleiman, na kuwauliza wananchi aliowaita yeye kuwa
"..wanawakilisha mikoa yote ya Zanzibar..." kuwa kama wapo tayari Jamhuri ya Zanzibar iungane na tanganyika na watu woote hapo wakaitikia ndiyooo, nani angebisha?? Hilo ndiyo unaloliita baraza la Mapinduzi???
Hakuna
" hansard" wala
"minutes" za kikao cha Baraza la Mapinduzi zinazoonyesha wajumbe walikutana wapi, wangapi, agenda, maazimio,kura, waliokubali, waliokataa n.k kwako ww hiii ndo ridhaa????
Yaliyotokea ni akina Mfaranyaki na Twala, akiwamo na Okello kumbishia Karume asifanye pupa la kuunganisha nchi kwanza. Mfaranyaki alipoleta kubisha zaidi akaambiwa kwanza Zanzibar si kwao akiendelea kidomo domo atarejeshwa kwao unengerekoni, akaufyata, kadhalika na Okello, nawenzake n.k na kilichowakuta watu hawa kinajuulikana katika historia ya muungano.
Na kama unavyotaka watu waamini kuwa kuungana huku hakuna hila basi kwanini Karume amfukuze Dourado katika wakati ambao anahitajika na kwanini Nyerere akamfukuza Bashir Swanzy katika wakati ambao uhalali wa muungano unatafutwa?
Kama Jumbe alijuwa kuwa muungano huo una ridhaa ya baraza la Mapinduzi kwa nini alimfukuza Damian Lubuva{mwanasheria mamluki aliyeletwa na Nyerere Zanzibar} na kumrejesha tanganyika na Jumbe kuandika "petition" katika mahakama ya katiba kuhoji uhalali wa Muungano, si angekuja na makubaliano ya baraza la mapinduzi tu kuweka sawa palipokosewa kama walivyokubaliana, je hapa hapotoshi kuthibitisha kuwa Muungano huu ni wa kichochoroni, kati ya Nyerere na Karume tu?
Kama Nyerere hakuwaburuza wazanzibar katika muungano kwanini hakukubali kuwapa fursa kuhoji uhalali wake ili wananchi wajiridhishe kuwa kinachofanyika ni sahihi kwa ridhaa zao na taratibu zao, na badala yake akatengeneza majasusi wakaipora "petition" ya Jumbe kabla hata kufika kwa mrajis wa Mahakama kuu, na kumfikia yye Nyerere. Kwanini hili isiwe hoja kuwa Nyerere aliwan'ga'ngania wazanzibar kwa kuwakataza hata kuhoji muungano na kufukuza rais wao, mbona hakuwataka warudi Baraza la mapinduzi kupitisha shauri la kumuondoa rais ambaye baraza hilo ndilo lililomteua.
Hapa unatwambia uwongo wako kuwa eti Nyerere alishinikiza Jumbe achaguliwe kwa kuwa hakuwa akikubalika na Baraza la Mapinduzi, kumbukumbu zipo kuwa baaada ya Karume Kutangazwa amefariki, Baraza la Mapinduzi lilikutana na kumteuwa Jumbe ambaye alikuwa msaidizi nambari moja wa Mzee Karume na ndiye aliyetoa tangazo la serikali rasmi kuhusu kifo cha Mzee Karume na uamuzi wa Baraza la Mapinduzi kumteua yye rais kwa muda, wakati gani Nyerere alifanya mchakato wa ushawishi katika hali tete kama hiyo. Huo ni uwongo.
Nani kachangia mauwaji holela na kumpa kichwa cha kufanya atakavyo karume kama si Nyerere? Karume alipokuwa akiwashughulikia anaowaita
maadui wa Muungano, niNyerere unaedai hakulazimisha muungano aleinyamaza kimya bila kuhoji kitu, kwakuwa ushetani wake ulikuwa unalindwa kwa mkono wa chuma, iweje Makamo wa rais wa Jamhuri anauwa watu ww bosi wake uwe hujuwi au usiwe dhamana na hili(On the same principle of vicarious liability that the act of the servant is the act of the master) na ndo yeye Nyerere bila ya aibu, utu, huruma wala soni kwa Mungu wake, aliyewakabidhi Hanga na Mzee wetu Othaman Shariff wakauliwa Zanzibar(assessory after the fact) nayeye Nyerere pia muuwaji.
Leo unaniletea hadithi za
white paper ndugu yangu mm nilishiriki mwaka 1998 kisiwandui na katika matawi mbalimbli ya chama, kuandika maoni ya kubuni kwa niaba ya CCM kujidai kuwa Muungano wa serikali mbili uendelee bila kujuwa kuwa natumiwa kulinda maslahi ya wachache. (Naujutia muda ule mpaka leo na maisha nitakuwa mpinzani kulipa dhulma ile). Takwimu hizi bandia za nini kuzitegemea ww???
Nani kashawishi ASP na TANU ziungane? unajuwa jinsi Mzee Thabit Kombo Jesha alivyolia kwa kwi kwi kama mtoto mdogo ASP ilipouliwa kwa
"ushawihsi wa kibabe" wa Nyerere na
"ulevi" wa Jumbe tu?
Unanambia Mar. Prof. Haroub Othman kasema na kama na yeye hakuwa katutakia mema. Kusema ndugu kila mtu anasema ni uhuru wake kusema, kuandika, lakini Othmnan alikuwa Prof. hakuwa
Mtume au
Nabii kuwa alichokisema na kuandika ndo
maagano na amri za lazima kufata, hayo yalikuwa ni mawazo yake, na tulikuwa tukitofautiana kistaarabu pale kituoni kwake siku hizo na yeye wakati mwengine hukiri kuwa kuna mambo yamekosewa na yanaleta matatizo sasa. Hii haimaanishi kuwa msimamo wa wazanzibar wote kuwa na muungano wa haki siyo sahihi!
Bado tutaendelea kudai kuwa Muungano huu wa dhulmau urekebishwe na kama haiwezekani kurekebishwa tusiumizane vichwa wala tusitishane kila upande utazame maslahi yake bas.
J,