Pinda: Zanzibar sio NCHI... Werema: Zanzibar ni NCHI (Serikali yao ni MOJA, RAIS wao ni MMOJA)

Pinda: Zanzibar sio NCHI... Werema: Zanzibar ni NCHI (Serikali yao ni MOJA, RAIS wao ni MMOJA)

Mwanzo nilikuwa nabisha lakini sasa nimeamini kwamba Zanzibar inatawaliwa na Tanganyika .

Hivi kwa dunia ya sasa inaruhusiwa kutawala nchi nyingine kwa mabavu ?

inaruhusiwa ikiwa nyinyi mnaotawaliwa ni waislamu lakini zanzibar ingalikuwa ni nchi ya kikiristo ingalishakuwa huru zamani
 
Imekuwa ikisemekana zanzibar ni nchi lakini hivi karibuni imegundulika sio nchi, wala dola, wala nchi iliyo huru bali ni sehemu ya Jamhuri ya muungano wa tanzania au unaweza kusema ni eneo la Tanzania au mkoa wa Tanzania au jimbo la tanzania

Hiyo bendera waliyonayo, wimbo walionao na rais wanaemchagua ni geresha tu

Wiki iliyopita wakati CAF wakiifutia zanzibar uanachama walihoji kama kuna nchi duniani inaitwa zanzibar inayojitegemea na mambo yake binafsi kama sudani kusini

Wakaangalia na ramani ya dunia kama kuna nchi inaitwa zanzibar hawakuiona bali waliishia kuiona Tanzania tu

So wale wanaosema zanzibar ni nchi hili wanalitoa wapi? Kama dunia haijui kuna nchi inaitwa zanzibar bali ni sehemu ya tanzania

Huu urais huko zanzibar
Na bendera waliyo nayo na wimbo walionao unawasaidiaje kuwa nchi inayotambulika?

Yangu macho
Namimi pia yangu macho,Warioba alitaka kuwapa Uhuru wao wenyewe wakaukataa wakiong'ozwa na balozi wao wa nyumba kumi sasa wanapiga kelele za mini wakati uraisi wenyewe wa Zanzibar unajulikana kwamba mwisho chumbe
 
Wa-Africa hatuna AKILI zipo za kushikiwa tu kwa kuikataa ZNZ kutambulika.


UNITED KINGDOM ni Nchi moja inayotokana na sehemu Tatu
1)England
2)Scotland
3)Wales

Na hizo zote zinajiwakilisha zenyewe ukija kwenye INTARNATIONAL CUP kama World cup na Euro Cup ..............
Hapo tofauti ikwapi na ZANZIBAR na Jamhuri ya muungano Tanzania .

Kwenye nyekundu ndio mdudu gani huyo


Zimwi likujualo......
 
NDONDI WANA RAIS
TFF WANA RAIS
SIMBA WANA RAIS
RIADHA WANA RAIS
ZANZIBAR WANA RAIS

Kuwa na Rais sio inshu kubwa, mnaweza kuwa na Rais na bado mkaendelea kuisoma namba tu.
Urais ni Mbwembwe tu
 
4b207367cb49f096c6ef442b061b156c.jpg


Soma article 1 ya Montevideo Convention on the rights and duties of state of 1933.

Zanzibar siyo nchi kwa sababu imekosa kipengele (d) capacity to inter into legal relation. Ili Zanzibar iingie mkataba wowote wa kimataifa lazima ipate kibali kutoka serikali ya muungano kwa hiyo haina capacity ya kujiamria kuingia kwenye mikataba.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zanzibar ni nchi ndani ya mipaka ya Tanzania na sio nchi ukiwa nje ya mipaka ya Tanzania. Ni nchi kwa kuwa ina mihimili yote. Inayotakikana kuwepo kutokana na jinsi huo mwungano ulivyotengenezwa. Ilitakuwa Iwe mkoa lakini walikubaliana ibaki kuwa nchi huru ndani ya mwungano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom