Pinda: Zanzibar sio NCHI... Werema: Zanzibar ni NCHI (Serikali yao ni MOJA, RAIS wao ni MMOJA)

Mwanzo nilikuwa nabisha lakini sasa nimeamini kwamba Zanzibar inatawaliwa na Tanganyika .

Hivi kwa dunia ya sasa inaruhusiwa kutawala nchi nyingine kwa mabavu ?

inaruhusiwa ikiwa nyinyi mnaotawaliwa ni waislamu lakini zanzibar ingalikuwa ni nchi ya kikiristo ingalishakuwa huru zamani
 
Namimi pia yangu macho,Warioba alitaka kuwapa Uhuru wao wenyewe wakaukataa wakiong'ozwa na balozi wao wa nyumba kumi sasa wanapiga kelele za mini wakati uraisi wenyewe wa Zanzibar unajulikana kwamba mwisho chumbe
 
 
NDONDI WANA RAIS
TFF WANA RAIS
SIMBA WANA RAIS
RIADHA WANA RAIS
ZANZIBAR WANA RAIS

Kuwa na Rais sio inshu kubwa, mnaweza kuwa na Rais na bado mkaendelea kuisoma namba tu.
Urais ni Mbwembwe tu
 


Soma article 1 ya Montevideo Convention on the rights and duties of state of 1933.

Zanzibar siyo nchi kwa sababu imekosa kipengele (d) capacity to inter into legal relation. Ili Zanzibar iingie mkataba wowote wa kimataifa lazima ipate kibali kutoka serikali ya muungano kwa hiyo haina capacity ya kujiamria kuingia kwenye mikataba.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zanzibar ni nchi ndani ya mipaka ya Tanzania na sio nchi ukiwa nje ya mipaka ya Tanzania. Ni nchi kwa kuwa ina mihimili yote. Inayotakikana kuwepo kutokana na jinsi huo mwungano ulivyotengenezwa. Ilitakuwa Iwe mkoa lakini walikubaliana ibaki kuwa nchi huru ndani ya mwungano

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…