Pindi Chana: Nimesitisha usafirishaji wa wanyamapori mpaka nitakapopata taarifa kamili

Pindi Chana: Nimesitisha usafirishaji wa wanyamapori mpaka nitakapopata taarifa kamili

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Waziri wa Maliasili na utalii Mh Pindi Chana amesema kuna tangazo limekuwa likizunguka kwenye mitandao kuhusu usafirishaji wa wanyamapori ambalo lilizua taharuki toka jana.

Hivyo kwakuwa yeye ni Waziri mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii ametangaza kusitisha mara moja usafirishaji wa wanyamapori na Maliasili mpaka hapo atakapopata taarifa kamili na kutoa maamuzi.

Kwa maelezo yangu haya hakuna tena usafirishaji wa wanyama pori hao kama jinsi ambavyo tangazo hilo la jana limetolewa na hiyo taasisi" amesisitiza Balozi Pindi Chana.

Chanzo: EATV

N:B Ni wazi ndani ya Serikali hakuna mawasiliano kabisa hivi inawezekanaje waziri wa maliasili na utalii asiwe na taarifa na tangazo kubwa na nyeti kama lile?

Ni kweli waziri hakuwa na taarifa la na tangazo lile? Ni kweli waziri hakuambiwa kuhusu tangazo?
 
Untitled-1_2.jpg
Waziri Chana ametoa kauli hiyo kufuatia taarifa zilizokuwa zinasambaa mitandaoni kuwa baadhi ya taasisi zimeanza kusafirisha wanyama hao kwenda nje ya nchi

Akizungumza na wanahabari Jijini Arusha Waziri Chana amesema zoezi la usafirishaji wa wanyama pori nchini limesitishwa mara moja hadi hapo serikali itakapopata taarifa rasmi na serikali kuamua vinginevyo

"Kwa maelezo yangu haya hakuna tena usafirishaji wa wanyama pori hao kama jinsi ambavyo tangazo hilo la jana limetolewa na hiyo taasisi" amesisitiza Balozi Pindi Chana
 
Ina maana waziri alikuwa hajapata taarifa kamili kuhusu usafirishaji wa wanyama pori....

Anyway kelele zimesaidia

Ova
Ni vigumu tangazo kama like kusambaa na waziri akose taarifa kamili, wanatuzuga tu hao vigogo.

Naona kelele za mitandaoni zimesikika, japo kuna wakati husema hawafanyii kazi mambo ya mitandaoni.
 
Waziri wa Maliasili na utalii Mh Pindi Chana amesema kuna tangazo limekuwa likizunguka kwenye mitandao kuhusu usafirishaji wa wanyamapori ambalo lilizua taharuki toka jana ! Hivyo kwakuwa yeye ni waziri mwenye dhamana ya Maliasili na utalii ametangaza kusitisha mara moja usafirishaji wa wanyamapori na maliasili yeyote mpaka hapo atakapo pata taarifa kamili na kutoa maamuzi!

N:B Ni wazi ndani ya serikali hakuna mawasiliano kabisa hivi inawezekanaje waziri wa maliasili na utalii asiwe na taarifa na tangazo kubwa na nyeti kama lile?

Ni kweli waziri hakuwa na taarifa la na tangazo lile? Ni kweli waziri hakuambiwa kuhusu tangazo?

Source :EATV
Kuna wajinga walitetea uuzwaji wanyama pori nje ya nchi,sijui sasa wanajisikiaje?
 
Kama mama amezuia huo mpango basi hapo ameupiga mwingi, tuwe na huruma na nchiyetu jamani.
 
Waziri wa Maliasili na utalii Mh Pindi Chana amesema kuna tangazo limekuwa likizunguka kwenye mitandao kuhusu usafirishaji wa wanyamapori ambalo lilizua taharuki toka jana ! Hivyo kwakuwa yeye ni waziri mwenye dhamana ya Maliasili na utalii ametangaza kusitisha mara moja usafirishaji wa wanyamapori na maliasili yeyote mpaka hapo atakapo pata taarifa kamili na kutoa maamuzi!

N:B Ni wazi ndani ya serikali hakuna mawasiliano kabisa hivi inawezekanaje waziri wa maliasili na utalii asiwe na taarifa na tangazo kubwa na nyeti kama lile?

Ni kweli waziri hakuwa na taarifa la na tangazo lile? Ni kweli waziri hakuambiwa kuhusu tangazo?

Source :EATV
Hangaya alishawahi kusema hachezi ngoma za mitandaoni. Ila kinyume chake mitandao inampeleka puta kuliko hata mtangulizi wake.
 
Back
Top Bottom