Pindi Chana: Nimesitisha usafirishaji wa wanyamapori mpaka nitakapopata taarifa kamili

Pindi Chana: Nimesitisha usafirishaji wa wanyamapori mpaka nitakapopata taarifa kamili

Waziri wa Maliasili na utalii Mh Pindi Chana amesema kuna tangazo limekuwa likizunguka kwenye mitandao kuhusu usafirishaji wa wanyamapori ambalo lilizua taharuki toka jana !

Hivyo kwakuwa yeye ni Waziri mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii ametangaza kusitisha mara moja usafirishaji wa wanyamapori na Maliasili mpaka hapo atakapopata taarifa kamili na kutoa maamuzi!

Kwa maelezo yangu haya hakuna tena usafirishaji wa wanyama pori hao kama jinsi ambavyo tangazo hilo la jana limetolewa na hiyo taasisi" amesisitiza Balozi Pindi Chana

Chanzo: EATV


N:B Ni wazi ndani ya serikali hakuna mawasiliano kabisa hivi inawezekanaje waziri wa maliasili na utalii asiwe na taarifa na tangazo kubwa na nyeti kama lile?

Ni kweli waziri hakuwa na taarifa la na tangazo lile? Ni kweli waziri hakuambiwa kuhusu tangazo?
Ili tujue kwamba hatuzugi basi na yeye atoe maandiko siyo mdomo mtupu. haiwezekani bandiko ni la Wizara halafu yeye asijue!

Sent from my TECNO PR651H using JamiiForums mobile app
 
View attachment 2251418Waziri Chana ametoa kauli hiyo kufuatia taarifa zilizokuwa zinasambaa mitandaoni kuwa baadhi ya taasisi zimeanza kusafirisha wanyama hao kwenda nje ya nchi

Akizungumza na wanahabari Jijini Arusha Waziri Chana amesema zoezi la usafirishaji wa wanyama pori nchini limesitishwa mara moja hadi hapo serikali itakapopata taarifa rasmi na serikali kuamua vinginevyo

"Kwa maelezo yangu haya hakuna tena usafirishaji wa wanyama pori hao kama jinsi ambavyo tangazo hilo la jana limetolewa na hiyo taasisi" amesisitiza Balozi Pindi Chana
Yaani Serikali ilikuwa haina taarifa!!? Basi kuna tatizo kubwa sana!! Wakati Serikali ndio iliyositisha usafirishaji huo mwaka 2016.
 
huyu waziri mm naona hafai pia mkurugenzi wa taasisi waliotangaza hafai ishu sensitive kama hii waziri ujui n shida
 
Hivyo kwakuwa yeye ni Waziri mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii ametangaza kusitisha mara moja usafirishaji wa wanyamapori na Maliasili mpaka hapo atakapopata taarifa kamili na kutoa maamuzi!
Yaani Waziri alikuwa hana habari na mambo yanayofanyika wizarani kwake hadi yanafika mitandaoni?

Hii ni serikali?
 
Back
Top Bottom