Angel Nylon
JF-Expert Member
- Jul 26, 2011
- 9,164
- 18,402
Nimetoka kupika biriani. Yaani huwezi amini Majangaaaa
- Mchele ulivyopakuliwa umetoka mweusiiiiiiiii sitanii yaani rangi nyeusi na kijani hata weupe hauonekani
- Kwenye mchuzi ma Karot yamegoma kuiva sijui kwa kuwa hukusema na mimi nikaweka makubwa makubwa. Maana karot zinawekwa mwisho.
- Ma pilipili hoho pia nayo yanatafunika kama mabichi vile.
- Hiii Giligilani inaelea tu juu yaani inaonekana kama mboga za majani zimetiwa mwishoni, inatafunika lakini imeleta sura mbayaaaa kichizi.
- Ninavyokula kuna ladha ya pilipili na mimi sikuweka sa sijuiii zimetoka wapi.
Kiufupi amu umenisaidia nimepata idea lakini next time sema na Quantity ya viungo. Mfano Currypowder nimemiminia pakti yoote matokeo yake imezidi ile mbaya.
Hukusema ni wakati gani unaweka Royco Mchuzi mix ingawa umeitaja.
Pia badala ya mtindi naweza kuweka kitu kingine? Ladha ya mchuzi imepotea kabisaa nadhani ni kwa sababu ya huo mtindi.
Ha ha haaaaa. Mbavu zangu jamani. Unataka mwalimu awepo apo apo