Evelyn Salt
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 70,916
- 141,437
Wapishi wa humu nawasalimu.
Napenda sana kula boga, ila upishi wangu unanikatisha tamaa, nikinunua boga kwenye migahawa huwa nakula linakua zuri linakua na unga unga kama kiazi kitamu.
Ishu sasa nije nilipike mimi, linakua lina maji maji, yani linanyonya maji sijui likiiva nikiliweka kwenye sahani linavuja maji tu (mchuzi maji)... hata halivutii tena kula linakata stimu. Nakosea wapi?
Huwa naandaa hivi: nalikata vipande namenya maganda, naweka kwa sufuria, chumvi kidogo na maji kidogo nachemsha.
Ila matokeo ndio hayo mimaji, kuna upishi mwingine? Au nakosea kuchagua boga? ( Siku zote sijui tu kuchagua mmh).
Niliwahi kusikia linatakiwa kuanikwa kabla ya kupika, ni kweli?
Naombeni ujuzi.