Pishi la boga, nakosea wapi?

Pishi la boga, nakosea wapi?

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
70,916
Reaction score
141,437
Wapishi wa humu nawasalimu.

Napenda sana kula boga, ila upishi wangu unanikatisha tamaa, nikinunua boga kwenye migahawa huwa nakula linakua zuri linakua na unga unga kama kiazi kitamu.

Ishu sasa nije nilipike mimi, linakua lina maji maji, yani linanyonya maji sijui likiiva nikiliweka kwenye sahani linavuja maji tu (mchuzi maji)... hata halivutii tena kula linakata stimu. Nakosea wapi?

Huwa naandaa hivi: nalikata vipande namenya maganda, naweka kwa sufuria, chumvi kidogo na maji kidogo nachemsha.

Ila matokeo ndio hayo mimaji, kuna upishi mwingine? Au nakosea kuchagua boga? ( Siku zote sijui tu kuchagua mmh).
Niliwahi kusikia linatakiwa kuanikwa kabla ya kupika, ni kweli?
Naombeni ujuzi.
 
Mimi si mpishi ila nilikokulia maboga viazi karanga vilihusika naona uko sawa maji machache mvuke ndo unatumika zaidi ni kama kuchemsha viazi vitamu ila pia yaweza kuwa aina yanatofautiana hapo sijui
 
Wengine huanika ndio

Binafsi Sina tofauti nawewe Ila langu linakuwa tu Sawa
labda punguza maji usiweke mengi yakazidi ujazo wa maboga namaanisha boga liive zaidi na mvuke kuliko maji hii inasaidia boga kuiva wakati Sawa na maji yatakapoisha
Au likiiva kama bado Kuna maji basi litoe wakati huo huo kwenye sufuria usiliache kwenye maji

Labda yaweza saidia[emoji1745]
 
Unachemsha na maganda?
Maji unaweka kiasi gani?

Ukiona limekuwa boko mix na maziwa na kasukari kadogo usonge wape watoto wa enjoy
Hamna hata anaependa ni mimi peke angu
 
Unazungumzia pitiku wewe.

hiyo unatakiwa ukaange.

mboga ya mabogo maji maji huwa ni libaya kwangu
 
Ila haya maboga sijawahi yaelewa jamani
Kuna mdada aliwahi kunishangaa kuona napika maboga, akasema hapendi....

Akanambia aliendaga ukweni akapewa boga yani aliona kama ni dharau alichukia.
Mi nikienda ugenini nipewe boga itakua chakula cha kipekee, nalipenda ila boga halinipendi
 
Back
Top Bottom