Pisi kali - Nini maana yake?

Sibonike

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Posts
17,296
Reaction score
18,027
Pisi kali lina trend sana sasa hivi. Nini hasa maana yake? Mwanamke mzuri? Huenda kila mtu anaelewa kivyake.

Ingawa kuna wadada wanajiita na kujisifu kuwa wao ni Pisi kali, kuna wengine wanaona kuwaita Pisi kali ni kuwadharau na kuwadhalilisha

Wewe una maoni gani?
 
MIMI NI CCM DAMU-----MIMI NI YANGA DAMU-----MIMI NI TANZANIA DAMU----MIMI NI TEAM MAGUFULI DAMU---- MIMI NASEMA KWA KAULI MOJA "BAADA YA MITANO TENA, KAZI IANZE"
kwaiyo we ndio PISI???

(KUNA WACHINA FLAN MBWA WAO ALIITWA PISI ni hukoooo KZ camp)
 
Pisi maana yake ni kipande.

Hii kauli ilianziaga kwa wahudumu wa mabasi na baadae mtaan,kipind hicho mtu anakuuliza vp leo tunapata wapi pisi akimanisha tunapata wapi mademu.

Mara nyingi pisi ilikua ni mwanamke unaekutana nae siku moja hakujui humjui mnaenda banduana kila mmoja anaunga na zake.

Siku hizi et pisi ni demu mkali na mademu wakiitwa pisi wanasikia burudani Kama vile wapo edeni[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mwanamke akiwa na mahusiano na tajiri anaitwa pisi Kali

Mwanamke akiwa na mahusiano na wenye kipato cha kati anaitwa mdangaji

Mwanamke akiwa na mahusiano na masikini anaitwa Malaya

Hapo kazi kwako kuelewa
Yaani hapo ni kama mpangilio wa hela anayopata kuanzia juu hadi chini kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…