Pita hapa, tupate elimu ndogo kuhusu kampuni

MASWALI
1. Inahitajika kiasi gani kuanzisha kampuni?
2. Kodi Kwa hiyo 30% ni Kwa makampuni hata madogo?
3. Ni zipi athari za kufungua kampuni bila ya kusajili?
4. Kuna tofauti gani kati ya usajili wa biashara na usajili wa kampuni?
 
MASWALI
1. Inahitajika kiasi gani kuanzisha kampuni?
2. Kodi Kwa hiyo 30% ni Kwa makampuni hata madogo?
3. Ni zipi athari za kufungua kampuni bila ya kusajili?
4. Kuna tofauti gani kati ya usajili wa biashara na usajili wa kampeni?
Nasubiri jibu
 
MASWALI
1. Inahitajika kiasi gani kuanzisha kampuni?
2. Kodi Kwa hiyo 30% ni Kwa makampuni hata madogo?
3. Ni zipi athari za kufungua kampuni bila ya kusajili?
4. Kuna tofauti gani kati ya usajili wa biashara na usajili wa kampuni?
1. Kiasi kinachohitajika kuanzisha kampuni Tanzania kinaweza kutofautiana kulingana na aina ya kampuni na mtaji wa kuanzisha.
gharama za brela zinaangalia mtaji
usiozidi 1m ni 167k
usiozidi 5m ni 247k
usiozidi 20m ni 322k
usiozidi 50m ni 362k
50m and above ni 512k


2.Kodi ya 30% Kwa profit ni kwa kampuni zote za ndani


3. Kufungua kampuni bila usajili kunaweza kuwa na athari mbaya, kama vile kushindwa kupata ulinzi wa kisheria na mikataba, kukosa fursa za kibiashara, na kuwekwa katika hatari ya kisheria. Kusajili kampuni kunahakikisha kwamba biashara yako inazingatia sheria na inalindwa kisheria.


4. Jina la biashara linaweza kutumika na wafanyabiashara binafsi au wamiliki wa biashara ndogo.
Hili ni jina ambalo unalitumia kuitambulisha biashara yako.
Linaweza kuwa jina lako binafsi au jina unalolichagua kwa biashara yako.
Inaweza kusajiliwa katika ofisi ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ili kuilinda na kuitambulisha kisheria.
Kampuni (Company)

Kampuni ni aina ya biashara inayojitegemea kisheria na inayoshiriki katika shughuli za biashara kwa niaba ya wamiliki wake.
Ina taratibu na wajibu wa kisheria unaohitaji usajili rasmi kwa BRELA..
Kampuni ina utambulisho wake wa kisheria na inaweza kujitegemea kifedha na kisheria kutoka kwa wamiliki wake.
Kwa ufupi, jina la biashara linaweza kutumika na wafanyabiashara binafsi au biashara ndogo, wakati kampuni ni aina ya biashara inayojitegemea kisheria na inahitaji usajili rasmi.
 
babukatunz
 
fungua ya 2mil uliyo nayo mkuu, hiyo ya 50m itakuongezea liability kubwa sana kwa nyie wamiliki mambo yakienda kushoto, sababu kiuhalisia hauna, anza mdogo mdogo kampuni hukua boss ukiipata hiyo 60m utaupdate TU brela
Mfano ipo iyo 2M na tupo watu wawili tunaotaka kufungua company ni taratibu zipi tunatakiwa kuzifata?
na nasikia kuna limited sijui na nini kingine yaani twaweza kupata elimu kidogo kuhusiana na haya maswala
 
Habari, kampuni ni mjumuiko wa watu wawili au zaidi wenye nia ya kufanya biashara halali na kuusajili mjumuiko huo chini ya Sheria ya kampuni, aina za kampuni kampuni inaweza kuwa kampuni ya kigeni,kampuni binafsi au kampuni ya umma, kwa upande wa jina la biashara ni utambulisho wa biashara fulani inayofanywa na mtu au kikundi cha watu, hivyo mtu mmoja au kikundi cha watu wasiozidi 20 wanaweza kusajili jina la biashara, mfano wa majina ya biashara ni Ali Entreprises, Rose Beauty Salon au John Urassa Investments. Baada ya kukamilisha usajili utatakiwa kufanya maombi ya leseni ya biashara kutokana na aina ya biashara ambayo unahitaji kufanya.
 
Asante Kwa Ufafanuzi
 
Kama nilisajiri kampuni na likatelekezwa na kuwa na malimbikizo ya Kodi,je naweza kuzuiwa kufungua kampuni nyingine,Asante.
 

Attachments

Ahsante nawe pia, karibu tena.
1. Kwenye kusajili kampuni hatua ya mwanzo oabisa inatakiwa TIN ila kwenye tin naona pako blank nafanyaje?

NB: Nishaweka taarifa za NIDA.

2. Name reservation inafanyake kazi?

3. Name similarity inatakiwa iwe ngapi ili ikubalike? 30% 10% au?

4. Kampuni inagakiwa iwe na director wawili, je mmoja wa hao madirector anaweza kuwa secretary?
 
1. Hiyo nafasi ya Tin haijazwi sasa, brela wao wenyewe wata assign number ya usajili wa kampuni Yako baada ya maombi hiyo pia ndo itakuwa tin Yako ya kampuni

2. Reservation ya jina hufanywa kwamalipo ya 50,000 na hureserviwa kwa siku 60

3. similarity unasaidia TU kujua uwepo wa jina lako kulinganishwa nayale ya kwenye mfumo, lkn haikupi uhakika wa jina lako kuwa na nafasi maana mengine hayapo kwenye mfumo, generally similarity inatakiwa iwe chini

4.ndiyo mmoja wa directors anawezakuwa secretary
 
Kwa ushauri na msaada kuhusiana na masuala yote ya usajili wa biashara usulisite kuwasiliana nasi kupitia 0629706263
 
Kwa Asiye na uraia wa Tanzania process z inakuwaje?
process ni zile zile kama anasajili local company sema atatumia passport ,.lkn kama anasajili foreign company ndiyo kunamanadiliko ya procedure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…