LGE2024 Pius Msekwa aeleza kutofurahia ushindi wa 99% wa CCM, asema anafurahia tu pale uchaguzi unapomalizika na pande zote zinaridhika

LGE2024 Pius Msekwa aeleza kutofurahia ushindi wa 99% wa CCM, asema anafurahia tu pale uchaguzi unapomalizika na pande zote zinaridhika

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Mchengerwa alitaka kumfuraisha mama mkwe, kwamba yeye na Chama Chake anakubalika kitu ambacho si kweli
 
Kwa hiyo unakiri kuwa ulikuwa UFISADI kwa kutumia katiba?
Shida yangu ni kwamba hata hao wanaolaumu sasa hivi wanajua na walikuwa wanajua kwamba huko mbele ya safari kutakuja kutokea sintofahamu kama wanazoziona wao sasa hivi na bado haitoonekana popote pale kwamba Katiba labda imevunjwa !

Maana yake ni kwamba kipindi kile wao wakiwa madarakani walikuwa wakiona sawa lakini sasa wao hawapo madarakani wanaona si sawa !

Najaribu kutafakari kama katika kipindi chao ni nani alivunja Katiba katika masuala ya Uchaguzi ?!
Sioni yeyote aliyevunja Katiba !
Je na sasa yanayofanyika kwenye Uchaguzi ni kinyume na Katiba ??!
Au ni kwa sababu yapo mapungufu mengi ndani ya Katiba yanatakiwa kutolewa Ufafanuzi ???!
Itapendeza kama Mzee Msekwa au Mzee Warioba wakitoa ufafanuzi juu ya hili Suala !!
Lawama bila Ufafanuzi wa kwa sababu gani haya yanatokea inazidisha sintofahamu tu !!
Au nasema uongo ndugu zanguni ?! 🙏
 
Tusubili tuone kama huyu nae atakuja Kusema Wazee Mnawashwa washwa
 
Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Pius Msekwa amesema hafurahii ushindi wa 99% wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika kwani kuna mapungufu mengi. Pia amesema mtu mwenye akili timamu hawezi kufurahia ushindi huo.

Spika mstaafu ameyasema hayo leo alipohojiwa na Sauti ya Kiswahili ya Ujerumani. Spika amevitaka vyombo vya uchaguzi kuondokana na kasoro ikiwa ni pamoja na matumizi ya nguvu na kuwaengua wapinzani ambapo amesema hilo halikuwahi kutokea hapo zamani kwanini linatokea sana siku hizi? Amehoji Spika Mstaafu.

---------

View attachment 3170482
chawa wa mama kwa kuwa akili zao zimehamia kwenye matumbo yao, watapinga busara za wazee.
 
Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Pius Msekwa amesema hafurahii ushindi wa 99% wa CCM katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliomalizika kwani kuna mapungufu mengi. Pia amesema mtu mwenye akili timamu hawezi kufurahia ushindi huo.

Spika mstaafu ameyasema hayo leo alipohojiwa na Sauti ya Kiswahili ya Ujerumani. Spika amevitaka vyombo vya uchaguzi kuondokana na kasoro ikiwa ni pamoja na matumizi ya nguvu na kuwaengua wapinzani ambapo amesema hilo halikuwahi kutokea hapo zamani kwanini linatokea sana siku hizi? Amehoji Spika Mstaafu.

---------

View attachment 3170482
Wazee wenye hekima, busara pamoja na kujielewa ni lazima wakemee upuuzi unaofanywa na watawala wa sasa. Viongozi wa kidini ambao wanajielewa tumeshuhudia nao pia wameonyesha kutokuridhishwa na uchafuzi uliofanyika.

Magufuli alipanda magugu mengi ndani ya shamba zuri la ngano. Sasa magugu haya yameota na hata mimea yote ya ngano imefifishwa . Viongozi wa CCM wana nia ovu na shamba la ngano, na pia wanafaidika kwa uwepo wa magugu yaliyopo shambani.

Ni muda sahihi wa kuanza kuuweka ukweli wote kuhusu uwepo wa magugu shambani, na pia kumtambua hila mbaya za adui mwenye kunufaika na uwepo wa magugu hayo, ndipo jitihada za kuweza kulisafisha shamba zofanyike ile Watanzania wapate mavuno mazuri ya ngano.
 
Ukimtoa Wasira,Musiba,Bashite,Mafwele na Kangi Lugola Watu wengine woote wa Lake Zone tunaipenda Tanganyika.
Sinde,Msekwa,
Yaani kwa akili yako unadhani nitamuacha Mpina kweli!
Nami nimo kwenye mkeka,cha msingi anza kuwaondoa nilioanza nao.
 
Mwasisi wa ujinga wote huu ni Magufuri itatuchukua muda nchi kukaa sawa labda waliok huko juu waanze kufarakana na kuuana.
Magufuli yupo , anakusikia. Magufuli hayupo tulikuwa na Nyerere hayupo, Mwinyi hayupo, Mkapa hayupo kazi ya kiongozi yeyote ni kuendeleza mazuri aliyoyakuta na kuacha mabaya Sasa kwanini tihangaike na Magufuli
 
Shida yangu ni kwamba hata hao wanaolaumu sasa hivi wanajua na walikuwa wanajua kwamba huko mbele ya safari kutakuja kutokea sintofahamu kama wanazoziona wao sasa hivi na bado haitoonekana popote pale kwamba Katiba labda imevunjwa !

Maana yake ni kwamba kipindi kile wao wakiwa madarakani walikuwa wakiona sawa lakini sasa wao hawapo madarakani wanaona si sawa !

Najaribu kutafakari kama katika kipindi chao ni nani alivunja Katiba katika masuala ya Uchaguzi ?!
Sioni yeyote aliyevunja Katiba !
Je na sasa yanayofanyika kwenye Uchaguzi ni kinyume na Katiba ??!
Au ni kwa sababu yapo mapungufu mengi ndani ya Katiba yanatakiwa kutolewa Ufafanuzi ???!
Itapendeza kama Mzee Msekwa au Mzee Warioba wakitoa ufafanuzi juu ya hili Suala !!
Lawama bila Ufafanuzi wa kwa sababu gani haya yanatokea inazidisha sintofahamu tu !!
Au nasema uongo ndugu zanguni ?! 🙏
Hawa wazee ndo waasisi wa mambo yote ya hovyo serikalini. Nawaashangaa sana wanalaumu upuuzi. Warioba ni nguli wa sheria lakini hakumshauri Mwalimu wakati anataifisha mali za watu enzi hizo.. hadi leo kuna watu wanalipwa fidia. Huyu Msekwa akiwa spika ndo mikataba inayoumiza taifa hadi leo ilisainiwa. Hawa wangekaa tu kimya maana sio wasafi. Wanalazimisha kuvunjiwa heshima.
 
UVCCM na Viongozi wa CCM watapelekwa mahakama ya ICC The Hague ikiwa hawatasikiliza usia wa Mzee Pius Msekwa kama huyu Jamaa Ntaganda case: Appeals Judgment on Reparations, 1 November 2024 (SWAHILI)

UTETEZI WA NTAGANDA MBELE YA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA ICC THE HAGUE ALIOUTOA KWA LUGHA YA KISWAHILI KUHUSU MADAI YA FIDIA

View: https://m.youtube.com/watch?v=_gjWNG2K28E

1733502083874.jpeg

Bosco Ntaganda

Mnamo tarehe 8 Julai 2019, Mahakama ya ICC ilimpata Bosco Ntaganda na hatia, bila shaka yoyote, ya makosa 18 ya uhalifu wa kivita na...

Maombi ya fidia​

Watu ambao wamepata madhara kutokana na uhalifu wowote ambao Bw Bosco Ntaganda ametiwa hatiani katika ICC na wanaotaka kuwasilisha maombi ya fidia wanaweza kufanya hivyo kwa kujaza fomu ya maombi ya fidia mahususi kwa kesi ya Ntaganda ( tazama kiungo hapa chini ). Fomu ya maombi imeundwa kukusanya taarifa zote muhimu zinazohitajika ili ombi lichukuliwe kuwa limekamilika. Mara baada ya VPRS kupokea maombi, VPRS itasajili taarifa zote katika hifadhidata yake na kuhifadhi nyaraka kwa usalama na kwa siri. Itachanganua yaliyomo na kubaini ustahiki wa mwombaji kwa fidia. Majaji watachukua uamuzi wa mwisho juu ya kustahiki kwa kila mwombaji.

Fomu ya maombi ya fidia kwa watu binafsi katika kesi ya Ntaganda inapatikana hapa
 
Wazee wenye hekima, busara pamoja na kujielewa ni lazima wakemee upuuzi unaofanywa na watawala wa sasa. Viongozi wa kidini ambao wanajielewa tumeshuhudia nao pia wameonyesha kutokuridhishwa na uchafuzi uliofanyika.

Magufuli alipanda magugu mengi ndani ya shamba zuri la ngano. Sasa magugu haya yameota na hata mimea yote ya ngano imefifishwa . Viongozi wa CCM wana nia ovu na shamba la ngano, na pia wanafaidika kwa uwepo wa magugu yaliyopo shambani.

Ni muda sahihi wa kuanza kuuweka ukweli wote kuhusu uwepo wa magugu shambani, na pia kumtambua hila mbaya za adui mwenye kunufaika na uwepo wa magugu hayo, ndipo jitihada za kuweza kulisafisha shamba zofanyike ile Watanzania wapate mavuno mazuri ya ngano.
Tuna kazi nyingine ya kutafuta uhuru wetu kutoka CCM.
 
Back
Top Bottom