Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Chama cha kufanya michezo ya kihuni ni ccm, tunawakaribisha sana waje ccm ili tuwafundishe roho mbaya kumzidi shetwani.Huo ndio ukweli mchungu. Wakatafute chama cha kuchezea siyo chadema.
Kumfuta Uanachama Mtu ni mchakato wa Kisheria & Kikanuni pia
Mchakato huo ili ukamilike haushii kwenye Kamati Kuu ya Chama husika pekee bali unaenda hadi ngazi ya Mahakama ya Rufaa!
Hivyo Mdee na wenzake 18 bado ni kiuhalisia Wabunge hadi itakapoamuliwa vinginevyo
na mamlaka husika kupitia mchakato huo!
Mzee wetu amekuwa na haraka mno kutoa hitimisho kana kwamba mchakato ulipoishia Ilikuwa Halali Kisheria na kuwa suala hilo limehitimishwa!
Katiba ipo mahsusi kulinda haki za wote na sio maamuzi ya Uongozi Wa Chama pekeyake!
Tusubiri mchakato ukamilike Kabla ya kutoa hitimisho
Mbeleko ya spika ipo...Time will tell.
Tuone hili sakata litaisha vipi. Iam sick and tired of being sick and tired
Kwa mujibu wa katiba Yes
Ila.........let us give time to time. Yajayo.......
ila mwenye akili timamu anajiuliza kwa nini ccm haitaki kabisa kusikia katiba mpya na tume huru ya uchaguzi?!!!
Una umri gani?Lini Zitto alikuwa Mbunge wa Mahakama?
Job ndugai anasemaje uko?Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba mpaka sasa Halima Mdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa wabunge kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 28, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ilipotaka kufahamu kama sheria na taratibu za Bunge zinaruhusu mbunge asiyekuwa na chama kuendelea kushika nafasi hiyo, hii ni baada ya wabunge hao kufukuzwa uanachama na chama chao cha CHADEMA usiku wa kuamkia leo.
"Siyo sheria ya Bunge hiyo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasema kuwa mbunge akiacha kuwa mwanachama wa chama kilichompeleka Bungeni na ubunge wake unakwisha, Spika Ndugai, hapati ugumu wowote wanapoondolewa yeye ni mpokeaji tu, ni kama mganga wa hospitali anapokea wagonjwa akiwatibu wanaondoka na wakifa wanaondoka na hakuna anayeweza kuvunja katiba"- amesema Spika Mstaafu, Mzee Pius Msekwa.
Usiku wa kuamkia leo Novemba 28, 2020, kupitia kikao cha kamati kuu ya chama cha CHADEMA iliyoketi na kuongozwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, iliazimia kuwavua uanachama wanachama wake 19 waliokula kiapo cha ubunge bila ridhaa ya chama hicho.
Wanachama waliofukuzwa uanachama ni pamoja na Halima Mdee, Ester Bulaya, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Salome Makamba, Grace Tendega, Nusrat Hanje, Jesca Kishoa, Tunza Malapo na wengineo.
CHANZO: "Hakuna wa kuvunja katiba, hawana sifa"- Msekwa | East Africa Television
Swala la kufukuzwa uwanachama kina halima Sio la kujadiliwa na ndugai bungeni, Bali anapaswa kuwaondoa kina mdee bungeni Mara moja, hili ni takwa la kikatiba.Ndivyo Katiba ilivyo,cha ajabu ni jinsi tulivyokosa wasema kweli kukemea huo uhalifu.Siyo waasisi,Mahakama,Bunge,Chama chenye uwezo huo.Tumekuwa nchi ya One Man's Show,we are only allowed to Praise.
Tunasubiri kifanyike kitu gani ndipo tuchukue hatua?Watanzania tulisomeshwa na kuelimika kweli?Is forgery acceptable here?
Usihangaike na watu waliosoma Ds akili zao zinawaza mafuvu.Kichekesho cha asubuhi,
Akihojiwa na Azam FM Radio, Propesa Kitila Mkumbo amedai kuwa hata baada ya kuvuliwa uanachama, akina Halima watakuwa wabunge wa Jamhuri. Lakini huyohuyo pia kawataka kwenda mahakamani kudai uanachama wao.
Yaani unaiezi mitatu tu humu na watu huwajui unaleta ujuaji wewe taga,haya kachukue buku saba yakoUnaboa na visredi mbuzi. Subiri maana yajayo yanafurahisha. Hao ni wabunge hadi 2025. Anayeweza kuwaondolea ubunge ni Mwenyezi Mungu tu.
Hata katiba inasema hivi
Oath of
Members of
Parliament
Act No.15
of 1984,
Art.13
68. Every Member of Parliament shall be required to take and subscribe
before the National Assembly the oath of allegiance before commencing to take
part in the business of the National Assembly save that he may take part in the
election of Speaker before taking that oath.
Je wakati wanaapishwa ndicho kilichofanyika? [emoji28] [emoji28] [emoji28] Katiba bila vyombo vyenye nguvu kuisimamia ni maandishi tu
Ngoja akuanzishie uzi kukujibu, ila daah P sijui kawaje jamani, wamteue apoe! Mamlaka za uteuzi Mungu anawaona!@Pascal Mayalla umemsikia Mh Pius Msekwa
Vp kama CCM wakiwatosa hao COVID-19 na kutafuta njia mbadala, CDM inabidi iwe makini mana hapo CCM watakuwa hawana cha kupoteza lakini CDM itakuwa imepoteza wanachama wake walio kengeuka na kuwa COVID-19
Mimi napendekeza chadema iagize haraka nafasi zilizoachwa WAZI kujazwa, kisha waanze process za kuliagiza balaza la wanawake kuchakata na kupendekeza majina ya viti maalumu, ili yapelekwe kamati kuu kuchambuliwa, kisha mchakato uchukue muda mrefu hapo kweny kamati kuu. Kuwaacha warelax kabisa akina Halima na wenzie ni kuwapa nafasi kwenda mahakaman, ili wajue hata huko bungeni wanatakiwa waondoke basi chama kioneshe dhamira ya kupata viti maalumu waliofwata taaratibu za chama !
Hon Msekwa nailed it allSpika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba mpaka sasa Halima Mdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa wabunge kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 28, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ilipotaka kufahamu kama sheria na taratibu za Bunge zinaruhusu mbunge asiyekuwa na chama kuendelea kushika nafasi hiyo, hii ni baada ya wabunge hao kufukuzwa uanachama na chama chao cha CHADEMA usiku wa kuamkia leo.
"Siyo sheria ya Bunge hiyo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasema kuwa mbunge akiacha kuwa mwanachama wa chama kilichompeleka Bungeni na ubunge wake unakwisha, Spika Ndugai, hapati ugumu wowote wanapoondolewa yeye ni mpokeaji tu, ni kama mganga wa hospitali anapokea wagonjwa akiwatibu wanaondoka na wakifa wanaondoka na hakuna anayeweza kuvunja katiba"- amesema Spika Mstaafu, Mzee Pius Msekwa.
Usiku wa kuamkia leo Novemba 28, 2020, kupitia kikao cha kamati kuu ya chama cha CHADEMA iliyoketi na kuongozwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, iliazimia kuwavua uanachama wanachama wake 19 waliokula kiapo cha ubunge bila ridhaa ya chama hicho.
Wanachama waliofukuzwa uanachama ni pamoja na Halima Mdee, Ester Bulaya, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Salome Makamba, Grace Tendega, Nusrat Hanje, Jesca Kishoa, Tunza Malapo na wengineo.
CHANZO: "Hakuna wa kuvunja katiba, hawana sifa"- Msekwa | East Africa Television
Kwani kamaanisha yeye au ni vifungu vya katiba? Atapigwa biti kwani yeye ndio kaandika hiyo katiba? Hili ni suala la kikatiba uwe unataka au hutaki otherwise badilisha sheria.