Pius Msekwa: Kwa mujibu wa Katiba, mpaka sasa Halima Mdee na wenzake hawana sifa za kuwa Wabunge

Pius Msekwa: Kwa mujibu wa Katiba, mpaka sasa Halima Mdee na wenzake hawana sifa za kuwa Wabunge

Zitto hajawahi kuwa mbunge wa mahakama, alipovuliwa uanachama alijitoa bungeni.
 
Waombe radhi tuu kiishe na heshima ibaki. Mdee ndio kama atajichora sana na hili saga na alivyomwepesi kulia!
 
CCM mnachekesha kweli. Mtaendelea kutawala kwa mapenzi ya polisi/JW/TISS tu. Mlivyomfukuza Membe, mlisubiri mpaka Mahakama ya Rufaa iamue? Kama maamumzi ya vyama yanawachukiza hivyo, futeni vyama vingi ili turudi enzi ya Nyerere. Yaani mnataka kufanya maamzi kwa niaba ya Kamati kuu ya CHADEMA. You should be ashamed of yourselves!
Kumfuta Uanachama Mtu ni mchakato wa Kisheria & Kikanuni pia

Mchakato huo ili ukamilike haushii kwenye Kamati Kuu ya Chama husika pekee bali unaenda hadi ngazi ya Mahakama ya Rufaa!

Hivyo Mdee na wenzake 18 bado ni kiuhalisia Wabunge hadi itakapoamuliwa vinginevyo
na mamlaka husika kupitia mchakato huo!

Mzee wetu amekuwa na haraka mno kutoa hitimisho kana kwamba mchakato ulipoishia Ilikuwa Halali Kisheria na kuwa suala hilo limehitimishwa!

Katiba ipo mahsusi kulinda haki za wote na sio maamuzi ya Uongozi Wa Chama pekeyake!

Tusubiri mchakato ukamilike Kabla ya kutoa hitimisho
 
Time will tell.

Tuone hili sakata litaisha vipi. Iam sick and tired of being sick and tired

Kwa mujibu wa katiba Yes

Ila.........let us give time to time. Yajayo.......
Mbeleko ya spika ipo...
Usiogope.
 
Wanajua hawawezi kutoboa. 2020 walikataliwa kabisa. Ndio maana wakateka wagombea wa upinzani ili wapite bila kupingwa, kura za kupigiwa nje ya vituo na kuingizwa vituoni kwa mtutu wa bunduki, nk. Wangekuwa wanajua kuwa wanapendwa, wasingefanya hayo.
ila mwenye akili timamu anajiuliza kwa nini ccm haitaki kabisa kusikia katiba mpya na tume huru ya uchaguzi?!!!
 
Du kweli mtu anakupokonya tonge mdomon,. Kirahis namna hiyo
 
Katika nchi hakuna mda wa kupumzika na siasa, yaan mfumo wetu wa maisha ni siasa tupu
 
Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba mpaka sasa Halima Mdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa wabunge kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 28, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ilipotaka kufahamu kama sheria na taratibu za Bunge zinaruhusu mbunge asiyekuwa na chama kuendelea kushika nafasi hiyo, hii ni baada ya wabunge hao kufukuzwa uanachama na chama chao cha CHADEMA usiku wa kuamkia leo.

"Siyo sheria ya Bunge hiyo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasema kuwa mbunge akiacha kuwa mwanachama wa chama kilichompeleka Bungeni na ubunge wake unakwisha, Spika Ndugai, hapati ugumu wowote wanapoondolewa yeye ni mpokeaji tu, ni kama mganga wa hospitali anapokea wagonjwa akiwatibu wanaondoka na wakifa wanaondoka na hakuna anayeweza kuvunja katiba"- amesema Spika Mstaafu, Mzee Pius Msekwa.

Usiku wa kuamkia leo Novemba 28, 2020, kupitia kikao cha kamati kuu ya chama cha CHADEMA iliyoketi na kuongozwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, iliazimia kuwavua uanachama wanachama wake 19 waliokula kiapo cha ubunge bila ridhaa ya chama hicho.

Wanachama waliofukuzwa uanachama ni pamoja na Halima Mdee, Ester Bulaya, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Salome Makamba, Grace Tendega, Nusrat Hanje, Jesca Kishoa, Tunza Malapo na wengineo.

CHANZO: "Hakuna wa kuvunja katiba, hawana sifa"- Msekwa | East Africa Television
Job ndugai anasemaje uko?
 
Ndivyo Katiba ilivyo,cha ajabu ni jinsi tulivyokosa wasema kweli kukemea huo uhalifu.Siyo waasisi,Mahakama,Bunge,Chama chenye uwezo huo.Tumekuwa nchi ya One Man's Show,we are only allowed to Praise.
Tunasubiri kifanyike kitu gani ndipo tuchukue hatua?Watanzania tulisomeshwa na kuelimika kweli?Is forgery acceptable here?
Swala la kufukuzwa uwanachama kina halima Sio la kujadiliwa na ndugai bungeni, Bali anapaswa kuwaondoa kina mdee bungeni Mara moja, hili ni takwa la kikatiba.
 
Kichekesho cha asubuhi,
Akihojiwa na Azam FM Radio, Propesa Kitila Mkumbo amedai kuwa hata baada ya kuvuliwa uanachama, akina Halima watakuwa wabunge wa Jamhuri. Lakini huyohuyo pia kawataka kwenda mahakamani kudai uanachama wao.
Usihangaike na watu waliosoma Ds akili zao zinawaza mafuvu.
 
Unaboa na visredi mbuzi. Subiri maana yajayo yanafurahisha. Hao ni wabunge hadi 2025. Anayeweza kuwaondolea ubunge ni Mwenyezi Mungu tu.
Yaani unaiezi mitatu tu humu na watu huwajui unaleta ujuaji wewe taga,haya kachukue buku saba yako
 
Hata katiba inasema hivi

Oath of
Members of
Parliament
Act No.15
of 1984,
Art.13
68. Every Member of Parliament shall be required to take and subscribe
before the National Assembly the oath of allegiance before commencing to take
part in the business of the National Assembly save that he may take part in the
election of Speaker before taking that oath.

Je wakati wanaapishwa ndicho kilichofanyika? [emoji28] [emoji28] [emoji28] Katiba bila vyombo vyenye nguvu kuisimamia ni maandishi tu

Hicho kifungu ndugai amekikanyagakanyaga na viatu vyake kama vile siyo yeye aliyeapishwa kuilinda hiyo katiba anatakiwa kufunguliwa kesi ya kukiuka katiba ya nchi mawakili tusaidieni katika hili ili huku mbele asitokee mwengine akafanya hayo mauchafuzi
 
@Pascal Mayalla umemsikia Mh Pius Msekwa
Ngoja akuanzishie uzi kukujibu, ila daah P sijui kawaje jamani, wamteue apoe! Mamlaka za uteuzi Mungu anawaona!

P apewe hata ukatibu tarafa huko Ushirombo!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Vp kama CCM wakiwatosa hao COVID-19 na kutafuta njia mbadala, CDM inabidi iwe makini mana hapo CCM watakuwa hawana cha kupoteza lakini CDM itakuwa imepoteza wanachama wake walio kengeuka na kuwa COVID-19

Tanzania ina watu zaidi ya milioni 50 CHADEMA haiwezi kuhangaika na hao nguchilo 19 wahamie huko CCM kama wanawaona ni wengi. Hiyo imeshaisha hakuna makombo
 
Mimi napendekeza chadema iagize haraka nafasi zilizoachwa WAZI kujazwa, kisha waanze process za kuliagiza balaza la wanawake kuchakata na kupendekeza majina ya viti maalumu, ili yapelekwe kamati kuu kuchambuliwa, kisha mchakato uchukue muda mrefu hapo kweny kamati kuu. Kuwaacha warelax kabisa akina Halima na wenzie ni kuwapa nafasi kwenda mahakaman, ili wajue hata huko bungeni wanatakiwa waondoke basi chama kioneshe dhamira ya kupata viti maalumu waliofwata taaratibu za chama !

CHADEMA haiwezi kuwa sehemu ya huo uchafuzi uliofanyika kama wanahitajika sasa wawakilishi si wachukuliwe wanawake mitaani huko waende CHADEMA haihitaji kuwa sehemu huo uchafuzi uliofanyika. Walipokuwa wanavuruga uchaguzi walisahau kuwa kuna trilioni 2 za msaada. Watakoma na ujinga wao sasa. CHADEMA umeshamaliza kazi inaendelea na ujenzi wa chama bila kutambua kama kuna seriakali
 
Spika Mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa, amesema kwa mujibu wa katiba mpaka sasa Halima Mdee na wenzake 18, hawana tena sifa za kuwa wabunge kwa kuwa hawana chama kilichowapeleka Bungeni na hata wakihamia chama kingine hawawezi kupata nafasi hizo, labda mpaka uchaguzi ujao.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba 28, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ilipotaka kufahamu kama sheria na taratibu za Bunge zinaruhusu mbunge asiyekuwa na chama kuendelea kushika nafasi hiyo, hii ni baada ya wabunge hao kufukuzwa uanachama na chama chao cha CHADEMA usiku wa kuamkia leo.

"Siyo sheria ya Bunge hiyo ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inasema kuwa mbunge akiacha kuwa mwanachama wa chama kilichompeleka Bungeni na ubunge wake unakwisha, Spika Ndugai, hapati ugumu wowote wanapoondolewa yeye ni mpokeaji tu, ni kama mganga wa hospitali anapokea wagonjwa akiwatibu wanaondoka na wakifa wanaondoka na hakuna anayeweza kuvunja katiba"- amesema Spika Mstaafu, Mzee Pius Msekwa.

Usiku wa kuamkia leo Novemba 28, 2020, kupitia kikao cha kamati kuu ya chama cha CHADEMA iliyoketi na kuongozwa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, iliazimia kuwavua uanachama wanachama wake 19 waliokula kiapo cha ubunge bila ridhaa ya chama hicho.

Wanachama waliofukuzwa uanachama ni pamoja na Halima Mdee, Ester Bulaya, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Salome Makamba, Grace Tendega, Nusrat Hanje, Jesca Kishoa, Tunza Malapo na wengineo.

CHANZO: "Hakuna wa kuvunja katiba, hawana sifa"- Msekwa | East Africa Television
Hon Msekwa nailed it all
 
Kwani kamaanisha yeye au ni vifungu vya katiba? Atapigwa biti kwani yeye ndio kaandika hiyo katiba? Hili ni suala la kikatiba uwe unataka au hutaki otherwise badilisha sheria.

Mkuu uko sahihi, lakini Magufuli haheshimu katiba. Cecil Mwambe alijiondoa cdm akajiunga ccm kabisa, kisha akaitwa na spika kuendelea na bunge. Wabunge wa ccm walipomuuliza yuko bungeni kwa uwakilishi wa chama kipi, alisema ameitwa na spika. Na kweli akaendelea kuwa mbunge!
 
Back
Top Bottom