Makala nzuri ingawa ni ndefu ila hakuna jinsi. Makala kama hii lazima iwe ndefu. Mengi uliyoandika nilikuwa nayafahamu ila siyo too deep kama ulivyoandika. Hongera na asante kwa muda wako kuamua kuweka hii makala.
Ila jambo moja ambalo nililitegemea utaliweka na la muhimu sana ni uhusiano wa CIA na hawa akina Escobar na Noriega Rais wa Nicaragua aliyetekwa nyumbani kwake na wanajeshi wa USA na kufichwa huko USA. Nafikiri hili Escober alilijua na ndiyo maana akawa hataki kabisa kupelekwa USA na akaona heri afe.
Ukitaka kuujuwa ukweli huu ni kufuatilia Mzee wa Crack Cocaine USA aliyeitwa RICK ROSS, the real Rick Ross (
Richard Donnell "
Freeway Rick"
Ross). Mwanzo aliletewa real cocaine aiuze kwa watu weusi na weusi wakamwambia ile ni ghali na wanatumia matajiri tu ambao ni WEUPE. Ndipo akaja kuletewa Crack ambayo imemaliza sana watu weusi US.
Baada ya miaka mingi kupita ndiyo akaja kujua kwamba aliyekuwa akimpa Crack na kumtonya mapema POLICE wakija kumfanyia msako alikuwa ni BOSS wa CIA.
Rick Ross mwanamuziki alikuja kuchukua jina la Rick Ross na kuwa ni Nick name yake ya kimuziki.
Wengine ni hawa Demetrius and Terry Flenory brothers na kundi lao wakijiita Black Mafia Family au BMF. Rick Ross alikuja pia kuimba wimbo na kuuita BMF ingawa anaimba Blowing Money Fast. Sijui kesi na ndugu wa Flenory brothers iliishaje.
Black Mafia Family na wao walitesa sana mitaa ya Atlanta na huku wakiuza Unga kama hawana akili nzuri. Police kila wakipanga kuwavamia na kuwakamata, jamaa walipewa sign mapema na kujisafisha na Police walipofika kwenye majengo yao walikuta hayana Madawa wala silaha.
Jamaa wamesaidia Wanamuziki wengi sana wa Atlanta kuwa maarufu kwani walipenda sana Hip Hop na kuwekeza fedha zao au kutupatupa fedha zao huko (Blowing Money Fast).
Hao nao walikuja kugundua baadaye kuwa aliyekuwa akiwapa mzigo na kuwatonya wajiandae na msako wa Police alikuwa ni jamaa wa CIA. CIA hawa jamaa badala ya kulinda wananchi, walihakikisha magereza yanajaa na hasa watu weusi kwa kuwapa kila aina ya madawa ili walewe na wafanye ujinga uliowatia kirahisi magerezani. Magereza USA ambayo ni Private yalikuwa na mkataba na serikali kuwa ni lazima yawe yamejaa. MTV nayo ikaja kunogeza tu wajinga hao.
Kuna Video ya Real Rick Ross akilalamika alivyotumiwa na CIA kuwa-CRACK watu weusi wa USA. Kwa ufupi hizi biashara ilikuwa huwezi kuzifanya bila idhini ya WAKUBWA. Kwamba USA huwa wanapenda kujiumiza wenyewe time to time ni kuangalia jinsi walivyoanzisha Al Qaida na ISIS ambayo sasa wanatumia fedha nyingi ili kuitekekeza.
Nashukuru sana Mkuu! I will look into that..