bahati93
JF-Expert Member
- Aug 6, 2015
- 1,334
- 2,463
Kuna kitu kinaitwa Capital, hata mwalimu nyereree alikuwaa anakifahamu sana, hapa duniani wananchi wa kawaida wa marekani wana capital kubwaa sana na huwa inategemea wapi wameona kuna fursa. Kilichotokea Japan ni kwamba mabeberu wa marekani waliona fursa za kukuza mitaji yao kwa japani, kwa sababu japani na watu wake baada ya kupigwa na marekani walikuwa wepesi sana kukubali mikataba ya kiuwekezaji iliyolalia upande wa marekani. Pia japani ilikuwa tayari ina jamii yenye watu ambao wana ujuzi hivyo ilikuwa rahisi kuchakata mitaji naa kutengeneza faida.
Sasa baada ya japani kujiona yupo sawa zikanza vuta nikuvute na serikali, kitu kilichopelekea mabeberu wananchi wa marekani kuona hali si swari hivyo wakaanza kutoa mitaji yao, kwani raisi wao Nixoni tayari alikuwa kashapata Chaka jipya China.
Hivyo wazee wa mitaji wakaingia china na Japani akakosa pesaa. China wamarekani wamepiga sana pesa kwasababu kwanza wanainchi ni watiii sana wa serikali, wanaishi kama sisimizi, yani kwa maji na mkate anasurvive, hawalipwi mshahara mkubwa, na huwezi kuta maandamano ya kudai maslahi, sasa wanaichi china kama wana kamgomo baridi na Serikali yao, kwanza hawataki kuzaliana, pia wengine hawataki kabisa kufanya kazi, wanalala tu majumbani mwao. watu wengi walishituka sana baada ya kuona mazingira ya dormitory ya wafanyakazi waunda smartphone za Apple!
Sasa na China yupo kukimbiwa kutokana na choko choko zake, juzi tu nimemwona Xi yupo marekanaa anaomba vyuma vilegezwe. Na China mbadala wake ni India, Thailand na Vietnam. Mbaya zaidi china alikuwa haishi vizuri na majirani zake. Ndani ya miaka kumi china atakuwa kama puto lililotolewa upepo.