PLAZA ACCORD-Mkataba uliotumiwa na Marekani kuishusha Japan kiuchumi miaka ya 1980

PLAZA ACCORD-Mkataba uliotumiwa na Marekani kuishusha Japan kiuchumi miaka ya 1980

Wazee mbona hamsemi mikakati ipi ifanyike ili Tanzania nayo iwe levo za marekani?
Au nyie mnajua tu points za kuisaidia China,Japan na SK??
Kinachotumaliza ni CCM

China iko imara kwa sababu chama cha kikomunisti cha China CPC kina watu makini kinasimamia rasilimali za taifa, hawacheki na mafisadi na wala rushwa

Mafanikio ya China hayakuwa overnight process ukisoma na kufuatilia documentaries za historia ya China tangu kipindi cha Mwenyekiti Mao, comrade Deng Xiaoping, Jiang Zemin, Hu Jintao mpaka Xi Jinping utaelewa
 
Kule puerto rico ni kampeni na teua ,tengua na mkalitizame hili. Habari za ku curb trade deficit walaa!
 
Kuna kitu kinaitwa Capital, hata mwalimu nyereree alikuwaa anakifahamu sana, hapa duniani wananchi wa kawaida wa marekani wana capital kubwaa sana na huwa inategemea wapi wameona kuna fursa. Kilichotokea Japan ni kwamba mabeberu wa marekani waliona fursa za kukuza mitaji yao kwa japani, kwa sababu japani na watu wake baada ya kupigwa na marekani walikuwa wepesi sana kukubali mikataba ya kiuwekezaji iliyolalia upande wa marekani. Pia japani ilikuwa tayari ina jamii yenye watu ambao wana ujuzi hivyo ilikuwa rahisi kuchakata mitaji naa kutengeneza faida.

Sasa baada ya japani kujiona yupo sawa zikanza vuta nikuvute na serikali, kitu kilichopelekea mabeberu wananchi wa marekani kuona hali si swari hivyo wakaanza kutoa mitaji yao, kwani raisi wao Nixoni tayari alikuwa kashapata Chaka jipya China.

Hivyo wazee wa mitaji wakaingia china na Japani akakosa pesaa. China wamarekani wamepiga sana pesa kwasababu kwanza wanainchi ni watiii sana wa serikali, wanaishi kama sisimizi, yani kwa maji na mkate anasurvive, hawalipwi mshahara mkubwa, na huwezi kuta maandamano ya kudai maslahi, sasa wanaichi china kama wana kamgomo baridi na Serikali yao, kwanza hawataki kuzaliana, pia wengine hawataki kabisa kufanya kazi, wanalala tu majumbani mwao. watu wengi walishituka sana baada ya kuona mazingira ya dormitory ya wafanyakazi waunda smartphone za Apple!

Sasa na China yupo kukimbiwa kutokana na choko choko zake, juzi tu nimemwona Xi yupo marekanaa anaomba vyuma vilegezwe. Na China mbadala wake ni India, Thailand na Vietnam. Mbaya zaidi china alikuwa haishi vizuri na majirani zake. Ndani ya miaka kumi china atakuwa kama puto lililotolewa upepo.

Unataka tu kuonesha mahaba yako Kwa Marekani, kabla yavita ya Pili ya dunia japani alikuwa mbali sana
 
Ujerumani ni economic powerhouse ya Ulaya mpaka sasa
Screenshot_20230525-182741.png
 
Mkataba wa Saudia na USA wa kuuza mafuta kwa dollar(petrodollar) unazishua nchi za far east na kuinyanyua Marekani.

Siku wakishtuka Marekani atakuwa sawa na South Sudan
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila akil zako
 
Wanaishi kwa historia kitu ambacho China alishakataa, anyway ila potential wanazo wangetakiwa kukaza kama China in short wao wamekubali watabaki kuwa nyuma ya Marekani miaka yao yote

Leo hii Japan imepigwa gap la kwenda na China katika soko la dunia kila kona iwe ni electronics, automobile, shipping industry n.k kwa sababu ya kutekeleza sera za Marekani
waafrika mnashabikia bipolar world ila watesekaji wakubwa mtakuja kuwa nyiny , kwanza mnaongozwa na vipofu upigaj utakuja kuwa mwingi , ili uelew inabid niandike mengi ila tambua bipolar world itaifungua dunia na kuwafanya wenye nguvu kuwa huru zaid kuchagua mnyonge akiamin mataifa makubwa yatakaa kimya kuhofia kukuza mgogoro kama ilivyo Sudan kwa sasa hakuna atakaeingilia mpk mtu wamtoe moyo , huu ni mwanzo ila tutaona mengi kwenye hii bipolar word , mataifa dunia ya tatu yajipange kuteseka sana licha ya kuwa ss hv yanashabikia yakizan yatamkomoa mmarekan na mzungu
 
Kihalisi position aliyopo leo China ilikuwa iwe ya Japan, ila kaamua kurusha kitaulo kwa sababu ya kutii sera za Marekani

Marekani ni taifa ambalo sikuzote linalinda sana position yake hataki atoe mguu uweke mguu
si kwel China ilipaswa kuwa superpower tangu zaman sema jamii yao ilikuwa haijamka kwa japan ni ngumu sana kuja kutawala dunia maana hana factors strong za kuliteka dunia , China ina wasomi na soko kubwa pia , hapo awali haikuwa na wasomi ila japan ina wasomi ia haikuwa na market ya kuivutia dunia , hivyo ilimpasa kuwa chawa wa USA ambae alikuwa kateka akili za wengi duniani
 
waafrika mnashabikia bipolar world ila watesekaji wakubwa mtakuja kuwa nyiny , kwanza mnaongozwa na vipofu upigaj utakuja kuwa mwingi , ili uelew inabid niandike mengi ila tambua bipolar world itaifungua dunia na kuwafanya wenye nguvu kuwa huru zaid kuchagua mnyonge akiamin mataifa makubwa yatakaa kimya kuhofia kukuza mgogoro kama ilivyo Sudan kwa sasa hakuna atakaeingilia mpk mtu wamtoe moyo , huu ni mwanzo ila tutaona mengi kwenye hii bipolar word , mataifa dunia ya tatu yajipange kuteseka sana licha ya kuwa ss hv yanashabikia yakizan yatamkomoa mmarekan na mzungu
Asante kwa mchango wako chifu
 
Jinsi tunavyoiona leo teknolojia na uchumi wa China ukipaa na kuitishia Marekani, ndivyo ambavyo Japan ilikuwa na uchumi unaokua kwa kasi na kiteknolojia karibu kuifikia Marekani miaka ya 1980.

Marekani akaja na mkataba ulioitwa PLAZA ACCORD. Mkataba huu Marekani alisaini na mataifa ya Japan, Uingereza, Ufaransa na West Germany. Wakati huo haya ndiyo yalikuwa mataifa yenye uchumi mkubwa duniani na kiviwanda.

Wakati huo dollar ya Marekani ilikuwa na thamani kubwa sana kiasi kwamba export (mauzo ya nje) ya bidhaa za Marekani ilipungua sana duniani, kwa sababu watu wengi duniani walishindwa kuhimili bei za bidhaa za Marekani.

Yen ya Japan ilikuwa na thamani ndogo ukilinganisha na dollar hivyo ilisaidia sana kwenye export ya bidhaa zake. Wakati huo makampuni ya Japan kama TOYOTA, TOSHIBA n.k yalitawala soko la dunia huku makampuni ya Marekani yakiwa na export ndogo, hii ilikuwa hatari kwa uchumi wa Marekani.

Kwa sababu ya kushuka sana kwa mauzo ya nje ilipelekea trade deficit kwa uchumi wa Marekani. (Trade deficit ni pale taifa linapotumia pesa nyingi kuagiza bidhaa kutoka nje kuliko mapato wanayopata kwa kuuza bidhaa nje. Sikuzote hii huwa ni sign mbaya kwa uchumi wa nchi)

Tarehe 22 September 1985 katika hoteli ya New York City's Plaza Hotel, chini Marekani mawaziri wa fedha wa nchi za Japan, Ufaransa, Uingereza, West Germany na mwenyeji Marekani wakakutana.

Marekani aliyashinikiza mataifa hayo manne yapandishe thamani ya sarafu zao dhidi ya dollar ya Marekani.

Mataifa hayo yakakubaliana na Marekani matokeo ni kwamba kwenye soko la dunia Marekani akaanza kuuza zaidi bidhaa zake kuliko mataifa mengine ya kiviwanda

Nchi hizo ziliathirika sana kiuchumi lakini hasahasa Japan kwa sababu exportation ya bidhaa zao katika soko la duniani zilipungua sana.

Nafikiri katika vitu ambavyo Wajapani hawatakuja kusahau ni kuingia mkataba huu wa kimangungo na Marekani na kuwashusha.

China imekataa kuwa kama Japan imekataa kutikiswa na Marekani anapigwa vikwazo lakini anakuja na mbinu mbadala. Kuna la kujifunza kutoka China tofauti na Japan.

Marekani ni kutunishiana naye misuli tu kibabe kama Urusi na China wanavyofanya sio watu wazuri.

Japan na EU wametepeta wamechagua kuwa chawa wa Marekani.
Mimi kama raia nimeelewa sana hapa
Lakini wale wahuni kule Hazina na Mipango wapo bize kutunga tozo za kuwadidimiza wananchi kouchumi
 
Kuna moja kati ya haya mawili, nchi iweke Sera ya wananchi wake kumiliki uchumi na manufaa yawaletee wananchi unafuu wa maisha hivyo kusababisha maisha ya mwananchi mmojammoja kuwa bora zaidi.
Au
Serikali kuodhi njia zote za uchumi ili wananchi wapate nafuu ya maisha kwa speed iliyo ndogo sana...hili litasababisha nchi kuonekana tajari sana ila maisha ya wananchi wake ni wastani kabisa.
Au
Kwenda navyo vyote kwa pamoja, kitu ambacho ni ngumu sana lazima uwe na pande zote kama Marekani yaani ndumelakuwili.
Tanzania tunashidwa kupiga hatua kwasababu tunajifanya wajamaa na wabepari kwa wakati mmoja.
Viongozi wanaleta unafiki kwa kujifanya wajamaa wakiogopa wapiga kura masikini huku wakitenda upepari kwa kificho wakiogopa pia wananchi wapiga kura masikini.
Ujamaa ukoje kwenye nchi yetu?
 
Back
Top Bottom