Xi Jinping
JF-Expert Member
- Jun 14, 2023
- 3,651
- 11,548
- Thread starter
-
- #41
Kinachotumaliza ni CCMWazee mbona hamsemi mikakati ipi ifanyike ili Tanzania nayo iwe levo za marekani?
Au nyie mnajua tu points za kuisaidia China,Japan na SK??
Yaah kweliYeah kiteknolojia bado wako vizuri sana
Kama Ujerumani ni economic powerhouse ya Ulaya mpaka sasa
NAKAZIAKuna kitu kinaitwa BRI hili ni bomu kubwa China alilounda miaka mingi kucounter magharibi na linawalipa
Kuna kitu kinaitwa Capital, hata mwalimu nyereree alikuwaa anakifahamu sana, hapa duniani wananchi wa kawaida wa marekani wana capital kubwaa sana na huwa inategemea wapi wameona kuna fursa. Kilichotokea Japan ni kwamba mabeberu wa marekani waliona fursa za kukuza mitaji yao kwa japani, kwa sababu japani na watu wake baada ya kupigwa na marekani walikuwa wepesi sana kukubali mikataba ya kiuwekezaji iliyolalia upande wa marekani. Pia japani ilikuwa tayari ina jamii yenye watu ambao wana ujuzi hivyo ilikuwa rahisi kuchakata mitaji naa kutengeneza faida.
Sasa baada ya japani kujiona yupo sawa zikanza vuta nikuvute na serikali, kitu kilichopelekea mabeberu wananchi wa marekani kuona hali si swari hivyo wakaanza kutoa mitaji yao, kwani raisi wao Nixoni tayari alikuwa kashapata Chaka jipya China.
Hivyo wazee wa mitaji wakaingia china na Japani akakosa pesaa. China wamarekani wamepiga sana pesa kwasababu kwanza wanainchi ni watiii sana wa serikali, wanaishi kama sisimizi, yani kwa maji na mkate anasurvive, hawalipwi mshahara mkubwa, na huwezi kuta maandamano ya kudai maslahi, sasa wanaichi china kama wana kamgomo baridi na Serikali yao, kwanza hawataki kuzaliana, pia wengine hawataki kabisa kufanya kazi, wanalala tu majumbani mwao. watu wengi walishituka sana baada ya kuona mazingira ya dormitory ya wafanyakazi waunda smartphone za Apple!
Sasa na China yupo kukimbiwa kutokana na choko choko zake, juzi tu nimemwona Xi yupo marekanaa anaomba vyuma vilegezwe. Na China mbadala wake ni India, Thailand na Vietnam. Mbaya zaidi china alikuwa haishi vizuri na majirani zake. Ndani ya miaka kumi china atakuwa kama puto lililotolewa upepo.
Uko sahihiChina wao wenyewe wafanyabiashara wanafungua viwanda nje ikiwemo hiyo Vietnam
Ujerumani ni economic powerhouse ya Ulaya mpaka sasa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila akil zakoMkataba wa Saudia na USA wa kuuza mafuta kwa dollar(petrodollar) unazishua nchi za far east na kuinyanyua Marekani.
Siku wakishtuka Marekani atakuwa sawa na South Sudan
Huu ni mdororo wa kiuchumi Eurozone, USA na Japan wanaupitia
waafrika mnashabikia bipolar world ila watesekaji wakubwa mtakuja kuwa nyiny , kwanza mnaongozwa na vipofu upigaj utakuja kuwa mwingi , ili uelew inabid niandike mengi ila tambua bipolar world itaifungua dunia na kuwafanya wenye nguvu kuwa huru zaid kuchagua mnyonge akiamin mataifa makubwa yatakaa kimya kuhofia kukuza mgogoro kama ilivyo Sudan kwa sasa hakuna atakaeingilia mpk mtu wamtoe moyo , huu ni mwanzo ila tutaona mengi kwenye hii bipolar word , mataifa dunia ya tatu yajipange kuteseka sana licha ya kuwa ss hv yanashabikia yakizan yatamkomoa mmarekan na mzunguWanaishi kwa historia kitu ambacho China alishakataa, anyway ila potential wanazo wangetakiwa kukaza kama China in short wao wamekubali watabaki kuwa nyuma ya Marekani miaka yao yote
Leo hii Japan imepigwa gap la kwenda na China katika soko la dunia kila kona iwe ni electronics, automobile, shipping industry n.k kwa sababu ya kutekeleza sera za Marekani
si kwel China ilipaswa kuwa superpower tangu zaman sema jamii yao ilikuwa haijamka kwa japan ni ngumu sana kuja kutawala dunia maana hana factors strong za kuliteka dunia , China ina wasomi na soko kubwa pia , hapo awali haikuwa na wasomi ila japan ina wasomi ia haikuwa na market ya kuivutia dunia , hivyo ilimpasa kuwa chawa wa USA ambae alikuwa kateka akili za wengi dunianiKihalisi position aliyopo leo China ilikuwa iwe ya Japan, ila kaamua kurusha kitaulo kwa sababu ya kutii sera za Marekani
Marekani ni taifa ambalo sikuzote linalinda sana position yake hataki atoe mguu uweke mguu
Asante kwa mchango wako chifuwaafrika mnashabikia bipolar world ila watesekaji wakubwa mtakuja kuwa nyiny , kwanza mnaongozwa na vipofu upigaj utakuja kuwa mwingi , ili uelew inabid niandike mengi ila tambua bipolar world itaifungua dunia na kuwafanya wenye nguvu kuwa huru zaid kuchagua mnyonge akiamin mataifa makubwa yatakaa kimya kuhofia kukuza mgogoro kama ilivyo Sudan kwa sasa hakuna atakaeingilia mpk mtu wamtoe moyo , huu ni mwanzo ila tutaona mengi kwenye hii bipolar word , mataifa dunia ya tatu yajipange kuteseka sana licha ya kuwa ss hv yanashabikia yakizan yatamkomoa mmarekan na mzungu
Mimi kama raia nimeelewa sana hapaJinsi tunavyoiona leo teknolojia na uchumi wa China ukipaa na kuitishia Marekani, ndivyo ambavyo Japan ilikuwa na uchumi unaokua kwa kasi na kiteknolojia karibu kuifikia Marekani miaka ya 1980.
Marekani akaja na mkataba ulioitwa PLAZA ACCORD. Mkataba huu Marekani alisaini na mataifa ya Japan, Uingereza, Ufaransa na West Germany. Wakati huo haya ndiyo yalikuwa mataifa yenye uchumi mkubwa duniani na kiviwanda.
Wakati huo dollar ya Marekani ilikuwa na thamani kubwa sana kiasi kwamba export (mauzo ya nje) ya bidhaa za Marekani ilipungua sana duniani, kwa sababu watu wengi duniani walishindwa kuhimili bei za bidhaa za Marekani.
Yen ya Japan ilikuwa na thamani ndogo ukilinganisha na dollar hivyo ilisaidia sana kwenye export ya bidhaa zake. Wakati huo makampuni ya Japan kama TOYOTA, TOSHIBA n.k yalitawala soko la dunia huku makampuni ya Marekani yakiwa na export ndogo, hii ilikuwa hatari kwa uchumi wa Marekani.
Kwa sababu ya kushuka sana kwa mauzo ya nje ilipelekea trade deficit kwa uchumi wa Marekani. (Trade deficit ni pale taifa linapotumia pesa nyingi kuagiza bidhaa kutoka nje kuliko mapato wanayopata kwa kuuza bidhaa nje. Sikuzote hii huwa ni sign mbaya kwa uchumi wa nchi)
Tarehe 22 September 1985 katika hoteli ya New York City's Plaza Hotel, chini Marekani mawaziri wa fedha wa nchi za Japan, Ufaransa, Uingereza, West Germany na mwenyeji Marekani wakakutana.
Marekani aliyashinikiza mataifa hayo manne yapandishe thamani ya sarafu zao dhidi ya dollar ya Marekani.
Mataifa hayo yakakubaliana na Marekani matokeo ni kwamba kwenye soko la dunia Marekani akaanza kuuza zaidi bidhaa zake kuliko mataifa mengine ya kiviwanda
Nchi hizo ziliathirika sana kiuchumi lakini hasahasa Japan kwa sababu exportation ya bidhaa zao katika soko la duniani zilipungua sana.
Nafikiri katika vitu ambavyo Wajapani hawatakuja kusahau ni kuingia mkataba huu wa kimangungo na Marekani na kuwashusha.
China imekataa kuwa kama Japan imekataa kutikiswa na Marekani anapigwa vikwazo lakini anakuja na mbinu mbadala. Kuna la kujifunza kutoka China tofauti na Japan.
Marekani ni kutunishiana naye misuli tu kibabe kama Urusi na China wanavyofanya sio watu wazuri.
Japan na EU wametepeta wamechagua kuwa chawa wa Marekani.
Kuna plant ya BYD EV ipo U.S.A wachina wamefunguaUko sahihi
BYD wamefungua kiwanda Vietnam
Changan wana kiwanda Thailand
Nio wameivenst Hungary
FAW wana kiwanda South Africa
Hiyo ni mifano michache tu
Level aliyofika China sasa hivi ni kubwa sana ya kimataifa
Yeah ile plant ya BYD ya mabasi ya umeme wiki hii imetimiza miaka 10 tangu ifunguliwe nchini MarekaniKuna plant ya BYD EV ipo U.S.A wachina wamefungua
Wapo vizuri BYD.Yeah ile plant ya BYD ya mabasi ya umeme wiki hii imetimiza miaka 10 tangu ifunguliwe nchini Marekani
Umesema vyemaNi kama marekani anaweka vikwazo sehemu ambayo China tayari ameweka mbadala toka muda.
Ujamaa ukoje kwenye nchi yetu?Kuna moja kati ya haya mawili, nchi iweke Sera ya wananchi wake kumiliki uchumi na manufaa yawaletee wananchi unafuu wa maisha hivyo kusababisha maisha ya mwananchi mmojammoja kuwa bora zaidi.
Au
Serikali kuodhi njia zote za uchumi ili wananchi wapate nafuu ya maisha kwa speed iliyo ndogo sana...hili litasababisha nchi kuonekana tajari sana ila maisha ya wananchi wake ni wastani kabisa.
Au
Kwenda navyo vyote kwa pamoja, kitu ambacho ni ngumu sana lazima uwe na pande zote kama Marekani yaani ndumelakuwili.
Tanzania tunashidwa kupiga hatua kwasababu tunajifanya wajamaa na wabepari kwa wakati mmoja.
Viongozi wanaleta unafiki kwa kujifanya wajamaa wakiogopa wapiga kura masikini huku wakitenda upepari kwa kificho wakiogopa pia wananchi wapiga kura masikini.