Mleta mada uko sahihi, Hawa akina Nyalandu na Msigwa kwa kutumia kichaka cha demokrasia wanataka kuchelewesha ndoto za Watanzania kumuondoa Jiwe Madarakani.
Sasa hivi tulipaswa tuwe tunaongea namna gani ya kumsaidia Lissu ashinde, siyo kujadili tutampata lini mgombea wa uraisi kupitia Chadema.
Na Chadema wajifunze, wasipompa Lissu tiketi ya kugombea kwa sababu zozote za kimagumashi basi chama kitapata pigo kubwa sana hata kuweza kuwatoa katika reli.
Mtu aliyesimama kuuchallenge utawala wa Magufuli, jasiri asiyeogopa ndiye anayepaswa kupewa tiketi ya kupambana na Magufuli.
Kusimamisha mtu legelege kupambana na Magufuli ni kuuza mechi