PLO Lumumba, kusema CCM ni chama kinachopigania kunyanyua maisha ya Watanzania maskini kwa kutumia vizuri rasilimali za Tanzania, unadanganya dunia

PLO Lumumba, kusema CCM ni chama kinachopigania kunyanyua maisha ya Watanzania maskini kwa kutumia vizuri rasilimali za Tanzania, unadanganya dunia

Magufuli alifany maisha ya wananchi yawe magumu zaidi kwa miradi yake ambayo mingi ilikuwa haina tija kama ununuz wa ndege,na miradi ya chato
 
Kama umesikiliza mjadala wote,huwezi andika kwa kuquote katikati,hizo ni chuki.

Ungeweka maelezo yake yote.mbona kataja madhaifu na mazuri
Hajataja dhaifu hata moja, ebu tuwekee hilo dhaifu alotaja
 
Yaani huyo professor uchwara , ayajue maisha ya watanzania kuliko watanzania wenyewe ? Masihara hayo kiss professor ? Yaani aijue CCM kuliko sisi watanzania ? Nilifikiri maprofesa uchwara Kama Kabudi wako Tanzania tu kumbe na Kenya wapo ? Aibu ya Karne .
 
Post toka kwa mmoja wa members wa Jf ambao ni wapuuzi kabisa.
Hebu Kidogo mkuu, usikimbilie hitimisho bila kuweka ushawishi juu ya hitimisho lako.

Mimi nilikuwa sijamsoma huyo jamaa RMC, hadi nilipokufikia wewe hapa na hitimisho lako hilo.

Ikanibidi nami nimsome nione upuuzi aliouweka.

Baada ya kumsoma, nikaona wewe ndiye "MPUUZI" mkubwa.

Mimi sio mtetezi wa Magufuli katika ujumla wake; na namlaani sana sana kwenye baadhi ya mambo makubwa sana ya msingi kwa maisha ya waTanzania.

Kwa hiyo nawe usianze kunipaka 'upuuzi' uliompaka huyo jamaa RMC., ambaye kaeleza tu njia za kupima umaskini mahali popote. Sioni 'upuuzi' katika hilo, hata kama takwimu za NBS ni maghumashi.

Ndiyo, hata kama sikumpenda Magufuli kwa mabaya yake mazito kabisa aliyowatendea waTanzania, kuna maeneo aliyoipigania Tanzania, hata kama mapigano yake yalikuwa ya njia zisizo nzuri.
Katika mapigano hayo ninayokubaliana naye ni hilo la kulinda mali za taifa hili ili ziwaletee waTanzania manufaa kuliko yaliyokuwa yanapatikana huko nyuma.

Tuwe watu wa kutumia akili kupambanua mambo.

Tusisukumwe tu na kumshabikia mtu au chama. Tuishabikie Tanzania.
 
Nimemsikiliza huyu Prof nguli wa sheria toka nchini Kenya akizungumzia juu ya uzalendo wa hayati JPM juu ya kuwa kiongozi aliyekuwa kada wa CCM. Na kwa mujibu wa Prof Lumumba anadai CCM ni chama kinamchomuenzi hayati Julius Nyerere ndio maana kinakuwa kinahakikisha kuwa rasilimali za taifa la Tanzania zinatumika kunyanyua na kuendeleza maisha ya Watanzania.

Hivyo Prof Lumumba anadai kuwa sababu hayati JPM alikuwa mwanaCCM ndio maana alimuenzi hayati Nyerere kwa kuhakikisha anatumia rasilimali za taifa letu kuinua maisha ya Watanzania.

Jambo ambalo nimegundua kuwa huyu Prof Lumumba ameongea kwa kuangalia sarafu upande mmoja, huku akiwa haijui vizuri Tanzania. Maana kama anaijua vizuri Tanzania asingeongea pumba kama hizi.

Kwa haya maisha duni wanaoishi Watanzania ndio aseme CCM kwa miaka hiyo yote tangu itawale imeinua maisha ya watanzania masikini? Hata hayati JPM alipokuwa madarakani mbona umasikini umekuwa mkubwa? Mama lishe na wenye maduka wamefunga, ajira zilisimama, wafanyakazi hawajaongezwa mishahara. Huku ndio kuinua maisha ya wananchi? Mbona 80% wanamaisha duni? Au Prof. Lumumba na usomi wake anaona kununua ndege na kujenga Ubungo interchange ndio kuinua maisha ya watu!
View attachment 1740504
Ni mjinga sana huyu jamaa anaijua sana nchi yetu. Aongelee Mambo ya kwao ni shabiki wa CCM
 
Hawa maprof wa zama hizi ni wa kupuuzwa tu! Wameacha taaluma zao kwa ajili ya kujipendekeza tu
 
Back
Top Bottom