PLO Lumumba: Tundu Lissu ni muongo, nimefika Chato Hayati Magufuli hana utajiri wa kumlinganisha na Mobutu Sese Seko


Rwanda ni taifa la washenzi sio Tanzania, hapa Mungu hajakubali utawala wa mtu muovu. Wapinzani wa Kagame tunawaona wanapelekwa mahakamani kwa kesi za kubambikiwa, kama ilivyokuwa kwa Lisu hapa nyumbani. Magu alimuachia Lisu akiamini Lisu hatakuwa na watu kutokana na propaganda alizoendesha kwenye utawala wake. Alichokiona kwenye kampeni za Lisu kilimpa msongo wa mawazo, ndio maana akaagiza uchaguzi unajisiwe nchi nzima. Lisu aliondoka kwa msaada wa mabalozi wa ulaya na sio kwa ruhusa ya jiwe. Na angebaki hapa angeagiza amri zake za awali zikamilishwe. Hapo tofauti na Kagame itoke wapi labda?
 
Kwani nyinyi watanzania nani aliyewaroga hivi hiyo mbuga ya wanyama ni ya magu au ni ya hifadhi za taifa.mbona ilo pori lilikuwepo na ilikuwa hifadhi ya majambazi?sasa kuligeuza hifadhi ya taifa ndo limekuwa lake?mi nadhan mnaompinga magu mna lenu jampo na hamwezi kufanikiwa
 
Hivi Mbuga mpya Burigi iko wapi?
Chato hakijajengwa chuo kikubwa cha kanda cha VETA?
Hotel ya TANAPA ya nyota 3 wameshaimalizia?
Shamba kubwa la miti Tanzania lilizinduliwa na nani?
Kuna sehemu yoyote Tanzania waliwahi kupelekewa pesa za miradi ya maendeleo zaidi ya zile walizoomba?
Uwanja mkubwa kabisa wa mpira utaendelea kujengwa?
Chato kule hamna kitu, ni chuki Tu za watu, kule cha maana zaidi ni hospital
 
Huko Kenya PLO Lumumba ni mganga njaa tu
 
Watengenezeeni platform tupige kura tuone nani anakubalika zaidi
 
Yeye huyo Pro Lumumba anaishi Tz? Amewahi kupigwa Risasi ngapi?
Kwani wasiopigwa risasi tu ndiyo wanatoka tz na ndiyo wanaopaswa kuzungumza tu?

Je nyie huwa hamuongelei mambo ya nchi nyingine?
 
Huyo alishikwa wizi TBC na matumizi mabaya kiofisi, manunuzi hewa yasio fuata taratibu za kisheria, ni sawa na kakoko alivyo banwa TPA una dhani ata Muongea Samia vizuri maishani mwake? unadhani wafuasi wa kakoko watamuongea vizuri samia?, huyo ni former CEO wa TBC lakini mahali kuna shida ndio maana anatumia kila njia kuponda Magufuli kuhalalisha maovu yake yaleeee
 
Inaonesha Mungu anaipenda sana Tanzania kama hajaondoa watawala wakorofi katika mataifa mengine isipokuwa Tanzania tu basi ni wazi hayo mapenzi ya wazi ya Mungu kwetu na ndio maana hata Magufuli kwa kulijua hilo alikuwa anatuhimiza tuombe tu ili kwa ajili ya corona pamoja na kuwa dunia kote kuna corona alijua Tanzania si kama hayo mataifa mengine ya kishenzi Tanzania ni taifa linalopendwa na Mungu.

Kabla hata ya Magufuli miaka yote hakujawahi kuwa na uchaguzi uliyofanyika katika mazingira ya haki na siku zote tunasema ccm hawezi kuliruhusu hilo,sasa Magufuli kapita humo humo hivyo hata asingekuwa Magufuli bado isingefanya Lissu ashinde ule uchaguzi kivyovyote vile. Masuala ya watu kwenye kampeni ni kwamba walikuwepo pande zote hata kwa Magufuli kulikuwa na nyomi la watu na nyomi hilohilo tumeliona hata wakati wa kufa kwake ila hilo nyomi la Lissu ambalo aliliambia liingie barabarani kuandamana ila halikuonekana ni wazi lilikuwa linaenda kumshangaa tu Lissu kwa sababu ya kupigwa risasi basi.
 

Hilo nyomi la Magufuli subiri siku itokee kuna vita kisha waambie waende bila silaha ndio ulete mrejesho.
 
Tundu Lissu muongo sana na hafai kuwa kiongozi
 
Hilo nyomi la Magufuli subiri siku itokee kuna vita kisha waambie waende bila silaha ndio ulete mrejesho.
Hapa hatuzungumzii vita mkuu Tanzania ni nchi ya Amani.
 
Hapa hatuzungumzii vita mkuu Tanzania ni nchi ya Amani.

Siku ile Lisu aliyosema watu waingie barabarani wangeishia kuuwawa. Na ibilisi kwakuwa alijua anakaribia kufa alitaka afe na wengi, bahati nzuri Mungu wa watu wema alituepusha na yule muovu.
 
Siku ile Lisu aliyosema watu waingie barabarani wangeishia kuuwawa. Na ibilisi kwakuwa alijua anakaribia kufa alitaka afe na wengi, bahati nzuri Mungu wa watu wema alituepusha na yule muovu.
Hayo ni maelezo baada ya habari tu,tatizo sio hawakuingia barabarani tu bali hawakuwa hata na hilo wazo kabisa huko mitaani yani ni kama hawakumsikia Lissu,kiufupi Lissu hana ushawishi kabisa.
 
Hayo ni maelezo baada ya habari tu,tatizo sio hawakuingia barabarani tu bali hawakuwa hata na hilo wazo kabisa huko mitaani yani ni kama hawakumsikia Lissu,kiufupi Lissu hana ushawishi kabisa.

Ni kweli, je zile kura za kwenye mabeg zilikuwa za nini ili ibilisi atangazwe mshindi?
 
Wizi wa kura umeanza kufanywa na ccm kabla hata ya Magufuli.

Ule ulivuka viwango vya wizi, bali alinajisi uchaguzi. Ule ulikuwa ni uhayawani wazi ulioletwa na kiburi cha madaraka.
 
Kwa hiyo , alieanzisha mjadala hakufanya sahihi ? Kama aliweka mtu mmoja mwenye credibility na mwingine hana , maana yake nini? Hizo ndio dalili za tindo liso kushindwa vibaya kabisa na prof Lumumba , maana mnaanza kumcritisize Lumumba badala ya kuichambua mada. @no Lockdown in 🇬🇧
 
Ni kweli, je zile kura za kwenye mabeg zilikuwa za nini ili ibilisi atangazwe mshindi?
Zile kura za kwenye mabegi alizileta nani pale kwenye kituo? Aliezishika kituoni yupo wapi sasa ? Drama on the move🤣🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…