PLO Lumumba: Tundu Lissu ni muongo, nimefika Chato Hayati Magufuli hana utajiri wa kumlinganisha na Mobutu Sese Seko

PLO Lumumba: Tundu Lissu ni muongo, nimefika Chato Hayati Magufuli hana utajiri wa kumlinganisha na Mobutu Sese Seko

Kuna mtu anafikiria kwa nini Legency ya Magufuli inajadiliwa na Kutetewa na ambaye huko Kwao Kenya kwa sasa anadharauliwa?
Hawa VOA watakuwa wamefikiri nini hasa kutafuta mtetezi wa Marehemu failure(jiwe) kutoka kwa failure anayeishi(Lumumba)?
Kweli msemo "wacha wafu wazike wafu wao" unamaana nzito sana.
Kwako mwalimu Mshana Jr , hiyo waliyocheza VOA tunaitaje katika soka la siasa?
 
Kwa wenye akili FINYU tu kama wewe Bwashee. Huyo mpuuzi alidhani kufika chato ndiyo atathibitisha utajiri au umaskini wa dikteta!? Mpuuzi kweli huyo Lumumba. Hajui chochote kuhusu kampuni yake ya Mayanga ambayo jiwe kaipa miradi mingi sana ya Serikali kinyemela tangu awamu ya tatu, hajui chochote kuhusu bank accounts zake ndani ya nchi na si ajabu nje ya nchi, hajui lolote kuhusu hotel yake kule chato inayodaiwa ni 4 Star hotel ambayo sasa itakuwa gofu tu kwani hakuna tena wageni wa kulipiwa na Serikali kwenye hiyo hotel ambao jiwe alikuwa akilazimisha kiaina waende chato ili hotel yake ipate wateja.
Mkuu hata wewe ukiwa Rais utajenga hoteli hizo hizo zenye Nyota. Ukiwa Rais lazima utapendelea kwenu na utafanya maendeleo mengine. Mimi sishangai mtu kupendelea kwao. Angalia amefanyia nini Taifa lake. Tukianza kufufua makaburi hata wewe utapatikana na makosa au utakuwa unaliibia taifa[emoji3][emoji23] eidha kwa kuttolipa kodi au mambo mengine.

Kila mmoja ni mwizi katika his own Risk. Tuacheni chuki
 
Hospitali zinaendana na population density na kabla hospitali aijapandishwa hadhi lazima iwe na vigezo kadhaa.

Juzi tu tumeona kwenye ziara ya Dr Gwajima ukerewe wana hospitali kubwa tu wanaomba wapandishiwe hadhi, why? Kwa sababu kuna privilege zake.

Kwa wilaya kuwa na hospitali yenye hadhi ya wilaya hiyo ni heshima kubwa wengine ndio kwanza wanajengewa.

Isitoshe kusema kuna wenye kubwa zaidi ni uongo Tanzania nzima hospitali za rufaa ni 28 tu mpaka sasa on average kila mkoa ina moja. Na zote hizo zinachangamoto za uhaba wa either a, b or c.

Chato wana hospitali ya wilaya so far tena wameipata juzi tu ndio vitu vya mwisho Magufuli kufungua, kulikuwa na mpango wa kuiongeza ije kuwa hospitali ya kanda. Lakini ni kwa sababu za kujipendekeza sio proposal za Magufuli kama wale waliotaka kujenga ofisi gani sijui Chato Magufuli akawaambia hapana.

Kwa sasa hayupo I don’t think that hospital project will go ahead (vinginevyo ntashangaa). Kwa sababu ya criteria za hospitali ya kanda in relation to being placed at epicentre of targeted population Chato isn’t.

Huyo bwana kadai hakuna miradi kabisa Handeni, kwa ivyo unakiri kuna miradi mikubwa ya maji; yes wakandarasi wameboronga sasa hilo ni tatizo la Magufuli au wasimamizi kama mkurugenzi na ma engineer wa miradi huko kwenye halmashauri?

Vipi kuhusu kuongezwa kwa shule na madarasa, Handeni ni moja ya wilaya yenye surplus ya madarasa Tanzania kwa sasa, vipi jengo la kisasa la halmashauri.

Kuna shule ya VETA inajengwa maeneo hayo sina uhakika ni wilaya gani kama sio Handeni basi jirani.

Hakuna wilaya ambayo Magufuli ajagusa si ajabu kuna zahanati zaidi ya mbili pia Handeni imepata na miradi mingine luluki.

Tuseme asante kwa Magufuli kajitahidi mno ndani ya muda mfupi.
 
Kuna mtu anafikiria kwa nini Legency ya Magufuli inajadiliwa na Kutetewa na ambaye huko Kwao Kenya kwa sasa anadharauliwa?
Hawa VOA watakuwa wamefikiri nini hasa kutafuta mtetezi wa Marehemu failure(jiwe) kutoka kwa failure anayeishi(Lumumba)?
Kweli msemo "wacha wafu wazike wafu wao" unamaana nzito sana.
Kwako mwalimu Mshana Jr , hiyo waliyocheza VOA tunaitaje katika soka la siasa?
Kabla hawajaanza majadiliano ya moja kwa moja hamkuleta hoja hizi. Ila baada ya Lisu kuburuzwa kwa hoja ndiyo mnakuja na hizi vioja vyenu. Je Tundu Lisu angemzidi kwa hoja mgekuja na hizi vioja?
 
Kabla hawajaanza majadiliano ya moja kwa moja hamkuleta hoja hizi. Ila baada ya Lisu kuburuzwa kwa hoja ndiyo mnakuja na hizi vioja vyenu. Je Tundu Lisu angemzidi kwa hoja mgekuja na hizi vioja?

Hebu oneni na mitazamo ya wenzenu kule Tweeter kuhusu majadiliano ya usiku huu.
Tatizo JF limegeuka jukwaa la kumtetea marehemu
 
Chato ya zamani ndo mnaongelea eeh.

Tena huyu Mheshimiwa the late alianza kujimilikisha mashamba ya miti, mbuga za wanyama ambavyo mwisho documents zitakuwa na majina yake.

Mwalimu Nyerere angekuwa na hiyo tabia angejimilikisha nusu ya Tanzania kama mzee Jomo Kenyatta alivyofanya huko Kenya.

Mara zote Mungu hakosei na tuwe tunamshukuru kila wakati.
 
Ahsante sana Mkuu..,
Nadhani hoja zako zimeegemea sana kwenye habari ulizosikia ama machapisho uliyosoma ila inaelekea Handeni kwenyewe hupafahamu vema.
Halmashauri ya Handeni Mji na Vijini ni miongoni mwa Halmashauri chache ambazo zina uhaba mkubwa wa Madarasa hususani kwa Shule za Msingi.
Hata ule ukarabati uliofanyika kwa baadhi ya Shule za Msingi katika Wilaya nyingine, Handeni haujafanyika na hadi kufikia sasa wastani wa darasa moja ni Watoto kati ya 100 hadi 120 huo ni Mkondo mmoja tu.

Kuhusu Jengo la Kisasa la Halmashauri ingawaje bado halijakamilika ila ukweli ni kwamba Halmashauri zote mpya zimepata hiyo Miradi na nyingi zimeshahamia katika Majengo hayo mapya!

Kuhusu Miradi ya Maji hakukuwa na umuhimu wa kutumia fedha nyingi kuchimba Mabwawa badala yake wangetumia fedha hizo kuboresha Mradi wa HTM Korogwe unaotoa Maji mto Ruvu kupeleka Handeni then Kilindi na swala la Maji lingekuwa historia ila vyovyote iwavyo ndio Miradi hiyo ya Mabwawa ilikuwepo!

Naaaam.., ni kweli hospitali zote za Mikoa zimekuwa za Rufaa na zile Kongwe zimeboreshwa kuwa za Kanda.
Eneo lile la Mkata panapojengwa Halmashauri mpya pia palipendekezwa kujengwa Hospital ya Rufaa kwasababu ya Majeruhi wengi kukosa huduma za haraka za Kibingwa kutokana na umbali uliopo kati ya KCMC, Bombo na Tumbi na eneo lilishatengwa ikichagizwa na uwepo wa Tetesi za kuugawa Mkoa wa Tanga maana yake vigezo vya kuwa na hospital ya Rufaa imekidhi, ila yote hayo bado yanabaki kwenye Makaratasi.
Ahsante kwa muda wako Mkuu..!
 




[emoji3516]Ina maana huyo afisa elimu wa wilaya muongo?

Kuhusu maswala ya hospitali kama nilivyokwambia zina criteria. Ndio maana hospitali ya rufaa ni Bombo na KCMC kwa maeneo hayo na zote zipo wilaya za mjini.

Hospitali zina vigezo ya rufaa inavitengo ambavyo huduma zake ni specialized zaidi na inagharimu hela nyingi kuiendesha bila ya kusahau kila aina ya wataalamu lazima wawepo ndio maana nichache nchi nyingi duniani sio Tanzania tu.

Halikadhalika hospitali ya wilaya lazima iwe na uwezo wa ku deal na accident and emergency; kama ni ajali wanauwezo wa ku-stabilise mgonjwa kabla ajapelekwa hospitali ya rufaa. Hiyo ni kwa Tanzania nzima sio Handeni tu. Hospitali aiwezi kupewa hadhi ya wilaya kama aina vigezo na sizungumzii majengo bali aina ya huduma za tiba inazotoa.

Swala la maji sio Magufuli anaeshauri na kuamua ni engineers wa maji ndio wanaangalia viability za vyanzo mbali mbali kutokana na design zao na kupendekeza.

Sasa wewe kama ni mmoja wapo sema hiyo proposal yako ulipeleka wapi ikakataliwa, vinginevyo laumu wahusika wa wilaya na wizara ya maji. Muhimu kwenye hoja miradi ya maji ililetewa hela nyingi tu Handeni, tofauti na uongo unaosemwa.
 
Kwanini wewe unamwanudu lisu halafu unauliza swali? Ni suala la muda tu siku moja wewe na lisu wako mtajilaumu kwa kitendo chenu cha kushambulia wananchi wa geita na kanda ya ziwa kwa ujmla. Mtu yeyote mwenye nia na doto za kutaka kuwa kiongozi hatakiwi kuwa mbaguzi.

Lisu nae ni mtu wa kuabudiwa? Hafai kuabudiwa. CCM mmekuwa ni watu wa kusifu na kuabudu Binadamu waziwazi kwa kumtaja kama shujaa wa Afrika kitu ambacho ni dhambi kuu. kwamba bila yeye wengine hawana uwezo wowote. Acheni mwenendo huo wa kuabudu Binadamu,ila wa kuabudu ni MUNGU PEKEE
 
Nae huyo angeomba Uraia kwa Jiwe ,mbona walikataa kurusha picha za makazi ya marehemu?
 
Huyu profesa si mgeni kwenye mijadala hapa Tanzania na mara zote amekuwa pro CCM. Tuchungulie mijadala iliyokuwa ikifanyika Udsm, ni mwanaharakati ambaye hakuwahi kujutia shambulio dhidi ya Tundu Lissu!
Hivi utajiri wa mtu huonekana nyumbani kwake? Mimi huamini utajiri wa mtu huwa kwenye akiba zake za benki hasa za nje ya nchi.
 
Inaonekana hujitambui.wewe unatoka mkoa gani tukupatie miradi iliyojengwa kipindi chake. Jpm hadi kafufua na njia za reli zilizotelekezwa tangu kipindi cha nyerere kama vile Dar hadi Arusha na kwenyewe ni chato? Furaha yako ni kuona wananchi wa chato hawana mradi hata mmoja?.

Wewe ndio empty set hapa tunazungumzia upendeleo wa miradi ya kipuuzi kujengwa chato!! Airport chato ina msaada gani? Dar-Arusha ilijengwa zamani kimkakati jopo la wataalam lilikaa likaona ni vyema ijengwe huko ila Chato Aiport jopo gani lililokaa zaidi ya JIWE na Dotto James?
 
NOOOOOOOOO usiniingize kwenye kundi la majizi na mafisadi. Mshahara wa Rais ni mkubwa mno kuanza kuingia tamaa ya kuliibia Taifa lako, mshahara ambao utakula wewe na vitukuu vyako bila ya kudokoa hata senti ya walipa kodi.
Mkuu hata wewe ukiwa Rais utajenga hoteli hizo hizo zenye Nyota. Ukiwa Rais lazima utapendelea kwenu na utafanya maendeleo mengine. Mimi sishangai mtu kupendelea kwao. Angalia amefanyia nini Taifa lake. Tukianza kufufua makaburi hata wewe utapatikana na makosa au utakuwa unaliibia taifa[emoji3][emoji23] eidha kwa kuttolipa kodi au mambo mengine.

Kila mmoja ni mwizi katika his own Risk. Tuacheni chuki
 
Kwa hiyo huo ni utajiri wa Magu?

Wewe unaujua utajiri wa Magu? Usilazimishe tusemseme wakati hana uwezo wa kuja humu JF kwa ID isiyojulikana kujitetea , PLO anavyosema ameenda Chato amekuta hakuna utajiri kama watu walivyokuwa wanavyosema kwani alitarajia chato patakuwa kama Paris?
 
Kwa nchi ya Tz kitendo cha Rais magufuli kukosa transparency katika matumizi ya pesa za umma ni wazi ameiba kuliko Mobutu kwani mifumo ya enzi za mobutu huwezi kulinganisha na sasa.

Lumumba alikuwa coward wa Magu na haambiliki pia alijaza watu wake ikulu ataachaje kuiba.Ukweli Lumumba hajitambui.

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
PLO alitegemea azikute Mali zinatembea mtaani? Si mpàka uzifanyie uchunguzi kujua ziko wapi. Mali huwa ni Siri inapowezekana
 
Back
Top Bottom