PLO Lumumba: Wazungu wanaichukulia Afrika kama Zoo. Hawajali utu wa watu wa Afrika

PLO Lumumba: Wazungu wanaichukulia Afrika kama Zoo. Hawajali utu wa watu wa Afrika

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
PLO Lumumba ambae ni Mwanaumajimui maarufu wa Afrika anasema wazungu wanatumia jitihada kubwa kutunza Ndovu,Sokwe, Chui na wanyama wengine ambao wamo kwenye mapori ya Afrika ili wapate mahala pa kuja kupumzika lakini hawajali lolote kuhusu maslahi ya Afrika.

Anasema hivi karibuni watatuzuia kwenda huko kwao kwa sababu ya hizi COVID 19 nk anasema ni vema tubaki Afrika na tuijenge Afrika.

Nipo namsikiliza hapa youtube akihojiwa na Sahara Online TV jamaa ni mzalendo wa kweli wa Afrika.

Anasema vijana wa Afrika wametopea kushabikia masuala yasiyo na maslahi kwao na badala yake wamekuwa mashabiki wa vitu vyepesi visivyoleta tija kwao ndio sababu hatuendelei hasa vijana wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

MY TAKE:

Vijana tuamke tujenge Afrika na nchi yetu/zetu. Afrika ijengwe na Waafrika.

Capture.PNG
 
Huyu ni muathirika wa elimu ya ujamaa ni watu waliosoma zamani akili zao zimefungwa awajui chochote kuhusu ulimwengu wa sasa. Walipandikizwa chuki dhidi ya wazungu juu ya matatizo yetu.Wameshindwa kujua sisi wenyewe ndio chanzo cha matatizo yetu.
Hana tofauti na Walter Rodney
 
PLO, mshauri Kenyatta angalau akija kuondoka madrakani Kenya iwe kama one of the scadinavian countries. Hivi wazungu wanawazuia kuwa kamama say Sweden kimaendeleo?
 
PLO, mshauri Kenyatta angalau akija kuondoka madrakani Kenya iwe kama one of the scadinavian countries. Hivi wazungu wanawazuia kuwa kamama say Sweden kimaendeleo?
Ushauri hutolewa. Ni shauri la mpewa ushauri kuuchukua au kutouchukua.

PLO anasema viongozi wengi wa Afrika wanagandia madarakani hawataki kung'atuka kwa sababu wanaiba sana. Wanaogopa siku wakiachia ngazi watakuwa prosecuted!!!

This man is an African indeed!!!
 
Huyu ni muathirika wa elimu ya ujamaa ni watu waliosoma zamani akili zao zimefungwa awajui chochote kuhusu ulimwengu wa Sasa.Walipandikizwa chuki dhidi ya wazungu juu ya matatizo yetu.Wameshindwa kujua sisi wenyewe ndio chanzo cha matatizo yetu.
Hana tofauti na Walter Rodney
Wazungu hawana msaada wowote kwa Afrika, PLO yuko sahihi. Fanya analysis vizuri utagundua anachokisimamia kina ukweli mwingi. Whites ndio waliochangia Afrika kushindwa kuendelea.

Wazungu ukiwauliza KWANINI AFRIKA NI MASKINI wanakupa sababu nyepesi eti sababu ya idadi kubwa ya watu(Mbona Eastern Countries kama China na India population ni kubwa na ziko developed,mbona hiyo USA yenyewe iko na population kubwa na iko developed?)

Wazungu ndio walioleta sera za kimataifa ambazo hazina urafiki na nchi maskini za Kiafrika...tazama masharti yao ya ushirikiano wa kiuchumi hayana nia njema mostly!!!
 
Watuache tumzike pombe wetu kwanza[emoji26][emoji26][emoji26]
 
Huyu ni muathirika wa elimu ya ujamaa ni watu waliosoma zamani akili zao zimefungwa awajui chochote kuhusu ulimwengu wa Sasa.Walipandikizwa chuki dhidi ya wazungu juu ya matatizo yetu.Wameshindwa kujua sisi wenyewe ndio chanzo cha matatizo yetu.
Hana tofauti na Walter Rodney
Walter Rodney na theory zake. Basi nimetambua kuwa PLO Lumumba ni opponent wa Neo-Marxism
 
Huyu jamaa namdharau sana. Sijui ni sifa gani za kijinga anatafutaga akiongeaga kile kiingereza.
Nadhani hujamfuatilia. PLO Lumumba anazungumza Kiingereza cha kawaida sana ingia kwenye postings zake zote Youtube utagundua unachokielewa ni kitu tofauti tu may be ni memes au parody social media pages ndo wanakudanganya. Watu walishaamini Mugabe anapost utopolo moja hivi kumbe ni vijana wa Ki-Afrika wamekaa nyuma ya devices zao wanaandika ujinga!
 
Tupia hiyo , bila ushaidi wa you tube ni tantalila tuu.
Ingia Sahara TV YouTube angalia.sio kila kitu hapa lazima tuweke reference. Kwenye thread nimeshakutajia na source ya opinion yangu; nenda huko na wewe ukafuatilie ili upate hoja za kuchangia nilichoweka hapa. Busara na Hekima ni kuleta mchango wako wa nilichoandika na sio kudai picha.
 
Halafu kuna mtindo wa wazee 'wazalendo' kulaumu vijana eti hawajitumi, siyo wazalendo, yada yada, lakini hawa wamepewa miaka zaidi ya sitini na wazungu wanaowalaumu na wameshindwa kututoa kwenye umaskini. Wameiba, wamemismanage, wamefanya ukabila na ufala mwingine wote wa dunia hii halafu wanalaumu vijana na wazungu.

Hakuna uzalendo bora kama kuitoa nchi yako kwenye umaskini, mengine ni porojo zisizo na maana.
 
Huyu ni muathirika wa elimu ya ujamaa ni watu waliosoma zamani akili zao zimefungwa awajui chochote kuhusu ulimwengu wa Sasa.Walipandikizwa chuki dhidi ya wazungu juu ya matatizo yetu.Wameshindwa kujua sisi wenyewe ndio chanzo cha matatizo yetu.
Hana tofauti na Walter Rodney
Kwahiyo ulimwengu wa sasa wazungu wanajali maslahi ya Africa?
 
Back
Top Bottom