PLO Lumumba: Wazungu wanaichukulia Afrika kama Zoo. Hawajali utu wa watu wa Afrika

Wewe uliyesoma sasa hivi, tupe njia nini kifanyike tujikwamue tulipo
 
PLO, mshauri Kenyatta angalau akija kuondoka madrakani Kenya iwe kama one of the scadinavian countries. Hivi wazungu wanawazuia kuwa kamama say Sweden kimaendeleo?
Mkuu kumbuka kuna external factors zinazotuzuia tusiendelee
 
Alijipendekeza kwa jiwe kumsifia na kumpamba akitegemea teuzi.
Ni msomi lakini hana tofauti na musiba mulaga
Huyu ni mkenya. Mtu akishakuwa mpenda ujamaa we jua tayari ni nusu dikteta na mwenye ufinyu wa mawazo hata asome vipi. Hawa kazi yao huwa ni kujificha kwenye uzalendo kurubuni wajinga wengi wanaowaongoza.
 
Mtu anaepingana na rushwa na wala rushwa hawezi kuwa rafiki wa Africans ruling elites. He's a real African. An African indeed!
Ndio maana huyu jamaa huwa anawapenda watanzania. Maanake akija Tz huwa anawazingua na maneno yake mengi kisha mnaingia box kiulaini sana. Tuulizeni sisi wakenya ambaye tunamfahamu vizuri.

Patrick Loch Odhiambo(PLO) Lumumba aliteuliwa mwaka wa 2011 na rais Mwai Kibaki kama mwenyekiti wa KACC(Kenya Anti-Corruption Commission), taasisi huru ya kupambana na ufisadi. Ambayo sasa hivi Inaitwa EACC na hakujakuwepo na mtu yeyote mwingine ovyo zaidi yake kwenye historia ya uongozi wa taasisi hio.

Kwa muda wote ambao Lumumba aliongoza KACC hakuna mwanasiasa hata mmoja ambaye alifunguliwa mashtaka ya ufisadi mahakamani kupitia shirika hilo. Mbaya zaidi ni kwamba wakenya walikuwa na matumaini makubwa kwamba atafanya jambo la maana na kuandikisha rekodi mpya kwenye vita dhidi ya ufisadi.

Ila walichokichopata kutoka kwake ni mipasho tu isiyokuwa na kikomo na ahadi hewa kila siku ya wiki. Bure kabisa huyo jamaa na tangu siku hiyo wakenya huwa hawapotezi muda mwingi na hizo lecture zake za kuuza sura.
 
Ndugu ww fanya yako uwezavyo ukipata nafasi ya kwenda nje nenda usiwasikilize hawa watu wana mameno matamu mdomoni mwao ila ni vinafiki hivi vibaraka wa wazungu
 
Tapeli wa siasa. Ni aibu hadi leo mtu hadi leo bado anawaza ukoloni tu na kuwasimanga wazungu alafu akipewa kazi inamshinda . Dunia haipo fair ukiwa laini utaliwa tu, tulianza na wazungu sasa hivi wapo wachina pia. Waafrika tunapenda sana kuonewa huruma kitu ambacho hakipo kwenye dunia halisi.
 
Huyu PLO ni mtu wa ovyo tu, anadhani kuonyesha chuki dhidi ya wazungu kutatufanya sisi waafrika tusonge mbele.

Ukimfuatilia utaona anatumia smart phone, yuko busy mtandaoni, anakwea pipa kuruka nchi na nchi, anaendesha ndinga kali, anamiliki Lap top ya kisasa, nyumbani kwake amefunga Tv ya kisasa, anatupia Suti za mamtoni, mkononi amevaa saa brand za mbele sana nk. Halafu anajifanya hawapendi wazungu.
 
Rafiki yake alietutoka huku Tanzania kwa miaka mingi alikuwa anaishi kwa hisani ya teknolojia ya mzungu lakini nae pia alikuwa anawachukia wazungu kupitia mlango wa uzalendo.
 
Unataka Msaada kutoka kwa Wazungu? swali fikirishi sana... Upumbavu huu unahitaji kupimwa Mkojo! Umuulize Mzungu kwanini wewe ni Masikini? hivi hapo ulipo upo sober au?

Tuache kuuliza maswali hadi mtu ajue huna akili au wewe ni Omba omba fanya kazi upate kipato bora uendelee
 
Wazungu na Ndovu wapi na wapi walishaacha kitambo sana anaogopa kuwasema Wachina? haya ndio yle aliyosema Lema Elimu bila akili...

Kama anawaonea gere wazungu kuja africa kulipa pesa kibao kutizama Ndovu basi aingie msituni akawauwe wote ili wazungu wakome kuja...
 
Soma aya ya mwisho ya mleta mada jamaa kasemea mtatizo yetu pia na mtoa mada akatoa maoni yake pia hapo mwishon

Mbona tunakuwa judgemental sana bila kusoma kwa umakini
 
Huwa nachukia hizi pumba za kulaumu wazungu, ukiwa mzembe utalaumu kila kitu.
Pambana bana, chakarika, ng'oa visiki, zibua, chimbua...nenda mbele kwa mbele...utaweza...utafaulu
 
Huyu profesa jana alikuwa uganda ktk mahojiano na Nbstv walikuwa na mada magufulificationn in E Africa ....
Sasa bwawa akatoa boko eti akadai M7 atumie ukongwe wake awaongoze viongoz wengine wa E africa kufikia SD ...ebwana eh twitter wa UG walimjia juu prof
 
Alijipendekeza kwa jiwe kumsifia na kumpamba akitegemea teuzi.
Ni msomi lakini hana tofauti na musiba mulaga

huyo mkenya na teuzi za magu wapi na wapi!!!

nyie ndio mnawahi stand tiketi mmefungia nyumbani.
 

nawewe ni zao lipi!!
 
huyo mkenya na teuzi za magu wapi na wapi!!!

nyie ndio mnawahi stand tiketi mmefungia nyumbani.
Magu ndie katiba ndie sheria ashindwi kitu vyoote vilivyomo ni mali yake,umpa amtakae.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…