PNA: Makamo wa Rais Dr Nchimbi, atamsaidia sana Rais Samia na Taifa, Ni Mkweli Anayeweza Kumweleza Rais Ukweli!. Ili Kumsaidia Aomba Rais Aombewe!

PNA: Makamo wa Rais Dr Nchimbi, atamsaidia sana Rais Samia na Taifa, Ni Mkweli Anayeweza Kumweleza Rais Ukweli!. Ili Kumsaidia Aomba Rais Aombewe!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi,

Hii ni safu yangu mpya inayoitwa PNA, kirefu chake ni PPR News Analysis. Tamka (P.N.A)

Hapa nitakuwa nawawekea News Analysis ya habari kubwa yoyote yenye maslahi kwa taifa.

PNA ni kufuatia kuwepo kwa gaps za kutokuwepo kabisa uchambuzi wa habari kwenye media zetu,hukuna any serious or critical analysis ya news kwenye media zetu, kuanzia magazeti, radio, TV na online media, hakuna uchambuzi wowote wa kina wa habari on serious issues zinazolikabili taifa letu.

Kufuatia my long experience ya uzoefu wa muda mrefu,wa zaidi ya miaka 30 newsroom, nina uwezo wa kufanya News analysis ya habari yoyote.

Kwenye News analysis yangu
  1. Kwanza nitakuwekea News yenyewe
  2. Kisha nitakuchambulia kilichosemwa au kuripotiwa kwenye News hiyo nikieleza what does it mean
  3. Mwisho nitamalizia kwa opinion yangu kuhusu umuhimu wa taarifa hiyo kwa Taifa letu na kwa maslahi ya taifa.
Habari ya kwanza kwa PNA kwenye bandiko hili ni jinsi Makamo wa Rais Dr Emmanuel Nchimbi, atakavyo msaidia sana Rais Samia, na kulisaidia Taifa, kwasababu huyu ni mtu mkweli asiye papasa wala kumungunya maneno, kwa maoni yangu, ukimuondoa Balozi Humphrey Polepole,huyu ndiye kiongozi pekee anayeweza kumsaidia Rais Samia kwa kumweleza ukweli kuhusu mapungufu yake as a human being, hakuna mkamilifu !.

Katika kumsaidia Rais Samia, Dr Nchimbi amenote madhaifu fulani, hivyo amewaomba viongozi wa dini, wamuombee Rais Samia.

Isikilize hii clip ili ujue VP Dr. Nchimbi ametaka Rais Samia aombewe nini
View: https://youtu.be/-eNen3NlaMc?si=6RgS59my73NLdLwg

Alichosema Makamu wa Rais, Balozi Dr. Emmanuel Nchimbi, anatoa wito kwa viongozi wa dini kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kwa mambo yafuatayo:
  • Afya na Maisha Marefu: Anawaomba waendelee kumuombea Rais ili Mungu amjalie afya njema na maisha marefu ya kuliongoza taifa [00:39].
  • Busara na Hekima: Ni muhimu kumuombea ili aendelee kupata busara na hekima katika maamuzi yake ya kila siku [00:47].
  • Wasaidizi Waaminifu: Anasisitiza umuhimu wa kumuombea Rais apate wasaidizi ambao ni waaminifu, wakweli, na wanaoipenda nchi kwa dhati, wenye nia ya kuona maendeleo ya kweli [01:03]. Hii maana yake ni Dr Nchimbi, ame note mapungufu kwa baadhi ya wasaidizi wa Rais Samia, sio waaminifu, sio wakweli!. Hili la wasaidizi wa Rais niliwahi kulizungumza humu Wasaidizi wa Magufuli walimuogopa hadi kushindwa kumsaidia, Je Wasaidizi wa Samia wanamsaidia kwa kumweleza ukweli au nao wanamuogopa? Tumsaidie au..?
    Screenshot_20240721-055430_Rifaly.jpg
  • Ulinzi dhidi ya Watu Wabaya: Anaomba Mungu ampe Rais "macho ya tai" ili aweze kuwatambua watu wabaya, wachonganishi, mafitini, waongo, na wezi [01:20]. Japo Rais Samia aliwahi kujinasibu kuwa japo macho yake yameregea lakini anaona sana,
    View: https://youtu.be/TaaXyzqd9bQ?si=Y6UjlEzMRUzzNL-w
  • hapa Dr Nchimbi amenote mapungufu ya hayo macho malegevu ya Rais Samia, kuna vitu hayana uwezo wa kuviona au kuwabaini na kuwatambua watu wabaya, wachonganishi, mafitini, waongo, na wezi na mafisadi, hivyo ameomba Rais Samia aombewe Mungu ampe jicho la Tai, hili ni jicho la tatu.
  • Usalama wa Ikulu: Dr. Nchimbi anaomba maombi yasaidie "kufunga mageti ya Ikulu" dhidi ya watu wenye nia mbaya, ubadhirifu, au wenye mawazo ya kumwaga damu, (wasiojulikana)ili wasiweze hata kusogea karibu na Rais [01:49]. Hapa Dr Nchimbi anamaanisha pale ikulu kuna watu wenye nia mbaya, wabadhirifu, na wenye mawazo ya kumwaga damu huwa wanaingia hivyo ameomba Mungu alinde geti la Ikulu, watu hao, wasikaribie Ikulu yetu, Mfano lile Bonge Nyanya la Zimbabwe, limwaga minoti ya doleri, limekuja mara 6 pale patakatifu petu na kupiga mapicha na mtu wetu, huku mapicha mengine ni very compromising positions, huku hakuna taarifa yoyote kutoka popote, linakuja kufanya nini au kwa issue gani!, na siku linaondoka, linamwaga minoti ya dala 💯 💯 airport nzima!, wafanyakazi wa eapoti wanapanga foleni kupokea bakhashish!. Watu wa type hii wasikaribie kabisa lango la patakatifu petu!.

Video hii inasisitiza kuwa utulivu wa nchi unategemea sana utulivu na usalama wa Rais [00:30]. Ukimtikisa rais ni umeitikisa nchi!

What does this mean
Rais Samia ni binadamu, ana mapungufu yake, tunapaswa kumuomba Mungu amsaidie na kuisaidia nchi yetu.

My Take,
Japo Makamu Rais Balozi Dr Nchimbi amewaomba viongozi wa dini ndio wamuombee Rais, mimi Pascal Mayalla naongezea
kwa kusema, Rais Samia, sio tuu aombewe na viongozi wa dini tuu, bali nashauri ni aombewe na Watanzania wote Wazalendo wa ukweli wa taifa letu, Tumuombee Rais Samia.

Mungu Mbariki Rais Samia

Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali
 
Aombewe dhidi ya nani? Yaani mtu mwenye uwezo wa kujilinda na kuzuia kile alichokiita mapinduzi unadhani hana huo uwezo wa kujilinda mpaka ategemee kuombewa?, au mashaka na hofu zimemjaa juu ya wale aliowaulia ndugu zao kuwa wanaweza kutaka kulipiza visasi juu yake na uongozi wake?, au ana hofu ya nguvu za mataifa makubwa kumshughulikia?.

Hivi kama mahakama na sheria ziliundwa kuwashughulikia watu wote kiusawa why yeye ahepuke kikombe hiki?, kujificha na kujifanya haoni machungu ya aliowaumiza haiondoi ukweli kuwa atalipa, na atalipa hakika hata Mumuombe Mungu wa Anga zipi.

Tutaanza kuona matokeo mdogo mdogo kuanzia watumishi wake mpaka yeye mwenyewe, na uzuri ni kwamba machungu yakiwazidi huwa hawafichi vilio, wanawatumaga wapambe wao kujisemesha kwa raia.

Samia anachokipitia sio siri na hakifichiki, hayupo sawa na hatowai kuwa sawa haijalishi anajitahidi kubadili mambo vipi na kutumia pesa kusawazisha... NCHI imemkataa.

Acheni kujichosha hayo maombi muwaombee ndugu zenu sio huyo jambazi
 
Wanabodi,

Hii ni safu yangu mpya inayoitwa PMNA, kirefu chake ni Pasco Mayalla News Analysis. Tamka (Piemeniei)

Hapa nitakuwa nawawekea News Analysis ya habari kubwa yoyote yenye maslahi kwa taifa.

PMNA ni kufuatia kuwepo kwa gaps kwenye media zetu, kuanzia mageti, radio, TV na online media, hakuna uchambuzi wa habari on serious issues zinazolikabili taifa letu.

Kufuatia uzoefu wangu wa long experience ya zaidi ya miaka 30 newsroom, nina uwezo wa kufanya News analysis ya habari yoyote.

Kwenye News analysis yangu
  1. Kwanza nitakuwekea News yenyewe
  2. Kisha nitakuchambulia kilichosemwa au kuripotiwa kwenye News hiyo
  3. Nitakuchambulia what does it mean
  4. Mwisho nitamalizia umuhimu wake kwa maslahi ya taifa.
Habari ya kwanza kwa PMNA kwenye bandiko hili ni jinsi Makamo wa Rais Dr Emmanuel Nchimbi, atakavyo msaidia sana Rais Samia, na kulisaidia Taifa, kwasababu huyu ni mtu mkweli asiye papasa wala kumungunya maneno, kwa maoni yangu, huyu ndiye kiongozi pekee anayeweza kumsaidia Rais Samia kwa kumweleza ukweli kuhusu mapungufu yake as a human being, hakuna mkamilifu !.

Katika kumsaidia Rais Samia, Dr Nchimbi amenote madhaifu fulani, hivyo amewaomba viongozi wa dini, wamuombee Rais Samia.

Isikilize hii clip ili ujue VP Dr. Nchimbi ametaka Rais Samia aombewe nini
View: https://youtu.be/-eNen3NlaMc?si=6RgS59my73NLdLwg

Alichosema Makamu wa Rais, Balozi Dr. Emmanuel Nchimbi, anatoa wito kwa viongozi wa dini kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kwa mambo yafuatayo:
  • Afya na Maisha Marefu: Anawaomba waendelee kumuombea Rais ili Mungu amjalie afya njema na maisha marefu ya kuliongoza taifa [00:39].
  • Busara na Hekima: Ni muhimu kumuombea ili aendelee kupata busara na hekima katika maamuzi yake ya kila siku [00:47].
  • Wasaidizi Waaminifu: Anasisitiza umuhimu wa kumuombea Rais apate wasaidizi ambao ni waaminifu, wakweli, na wanaoipenda nchi kwa dhati, wenye nia ya kuona maendeleo ya kweli [01:03]. Hii maana yake ni Dr Nchimbi, ame note mapungufu kwa baadhi ya wasaidizi wa Rais Samia, sio waaminifu, sio wakweli!. Hili la wasaidizi wa Rais niliwahi kulizungumza humu Wasaidizi wa Magufuli walimuogopa hadi kushindwa kumsaidia, Je Wasaidizi wa Samia wanamsaidia kwa kumweleza ukweli au nao wanamuogopa? Tumsaidie au..? View attachment 3540846
  • Ulinzi dhidi ya Watu Wabaya: Anaomba Mungu ampe Rais "macho ya tai" ili aweze kuwatambua watu wabaya, wachonganishi, mafitini, waongo, na wezi [01:20].
  • Usalama wa Ikulu: Dr. Nchimbi anaomba maombi yasaidie "kufunga mageti ya Ikulu" dhidi ya watu wenye nia mbaya, ubadhirifu, au mawazo ya kumwaga damu, ili wasiweze hata kusogea karibu na Rais [01:49].

Video hii inasisitiza kuwa utulivu wa nchi unategemea sana utulivu na usalama wa Rais [00:30].


Analysis inafuata.

Paskali

Teuzi enthusiast.
 
Kama hakujitenga na mauaji yaliyotokea wakati wa uchaguzi sidhani kama anamsaidia lolote.
Kama hakumkemea kitendo cha kuteua mtoto wake, mpwa wake, mkwe wake, shemeji yake na mshenga wake kwenye vyeo vya uwaziri hawezi kumsaidia chochote,.
Kama hamwambii aache kupora rasilimali za Tanganyika hawezi kumsaidia chochote.
Kama hakumwambia aache kuteka , kufanya mauaji na kuwapa kesi wanaomkosoa hawezi kumsaidia lolote.
Kama hawezi kumwambia aache kutumia wakatoliki feki hizo zitakuwa porojo.
 
Back
Top Bottom