Wanabodi,
Hii ni safu yangu mpya inayoitwa PMNA, kirefu chake ni Pasco Mayalla News Analysis. Tamka (Piemeniei)
Hapa nitakuwa nawawekea News Analysis ya habari kubwa yoyote yenye maslahi kwa taifa.
PMNA ni kufuatia kuwepo kwa gaps kwenye media zetu, kuanzia mageti, radio, TV na online media, hakuna uchambuzi wa habari on serious issues zinazolikabili taifa letu.
Kufuatia uzoefu wangu wa long experience ya zaidi ya miaka 30 newsroom, nina uwezo wa kufanya News analysis ya habari yoyote.
Kwenye News analysis yangu
Habari ya kwanza kwa PMNA kwenye bandiko hili ni jinsi Makamo wa Rais Dr Emmanuel Nchimbi, atakavyo msaidia sana Rais Samia, na kulisaidia Taifa, kwasababu huyu ni mtu mkweli asiye papasa wala kumungunya maneno, kwa maoni yangu, huyu ndiye kiongozi pekee anayeweza kumsaidia Rais Samia kwa kumweleza ukweli kuhusu mapungufu yake as a human being, hakuna mkamilifu !.
- Kwanza nitakuwekea News yenyewe
- Kisha nitakuchambulia kilichosemwa au kuripotiwa kwenye News hiyo
- Nitakuchambulia what does it mean
- Mwisho nitamalizia umuhimu wake kwa maslahi ya taifa.
Katika kumsaidia Rais Samia, Dr Nchimbi amenote madhaifu fulani, hivyo amewaomba viongozi wa dini, wamuombee Rais Samia.
Isikilize hii clip ili ujue VP Dr. Nchimbi ametaka Rais Samia aombewe nini
View: https://youtu.be/-eNen3NlaMc?si=6RgS59my73NLdLwg
Alichosema Makamu wa Rais, Balozi Dr. Emmanuel Nchimbi, anatoa wito kwa viongozi wa dini kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kwa mambo yafuatayo:
- Afya na Maisha Marefu: Anawaomba waendelee kumuombea Rais ili Mungu amjalie afya njema na maisha marefu ya kuliongoza taifa [00:39].
- Busara na Hekima: Ni muhimu kumuombea ili aendelee kupata busara na hekima katika maamuzi yake ya kila siku [00:47].
- Wasaidizi Waaminifu: Anasisitiza umuhimu wa kumuombea Rais apate wasaidizi ambao ni waaminifu, wakweli, na wanaoipenda nchi kwa dhati, wenye nia ya kuona maendeleo ya kweli [01:03]. Hii maana yake ni Dr Nchimbi, ame note mapungufu kwa baadhi ya wasaidizi wa Rais Samia, sio waaminifu, sio wakweli!. Hili la wasaidizi wa Rais niliwahi kulizungumza humu Wasaidizi wa Magufuli walimuogopa hadi kushindwa kumsaidia, Je Wasaidizi wa Samia wanamsaidia kwa kumweleza ukweli au nao wanamuogopa? Tumsaidie au..? View attachment 3540846
- Ulinzi dhidi ya Watu Wabaya: Anaomba Mungu ampe Rais "macho ya tai" ili aweze kuwatambua watu wabaya, wachonganishi, mafitini, waongo, na wezi [01:20]. Japo Rais Samia aliwahi kujinasibu kuwa japo macho yake yameregea lakini anaona sana,
View: https://youtu.be/TaaXyzqd9bQ?si=Y6UjlEzMRUzzNL-w- hapa Dr Nchimbi amenote mapungufu ya hayo macho malegevu Rais Samia, hayana uwezo wa kuwabaini na kuwatambua watu wabaya, wachonganishi, mafitini, waongo, na wezi na mafisadi, hivyo ameomba Rais Samia aombewe Mungu ampe jicho la Tai, hili ni jicho la tatu.
- Usalama wa Ikulu: Dr. Nchimbi anaomba maombi yasaidie "kufunga mageti ya Ikulu" dhidi ya watu wenye nia mbaya, ubadhirifu, au mawazo ya kumwaga damu, ili wasiweze hata kusogea karibu na Rais [01:49]. Hapa Dr Nchimbi anamaanisha pale ikulu kuna watu wenye nia mbaya, ubadhirifu, au mawazo ya kumwaga damu huwa wanaingia hivyo ameomba Mungu alinde geti la Ikulu, watu hao, wasikaribie Ikulu yetu, Mfano lile Bonge Nyanya limwaga minoti ya doleri, limekuja mara 4 pale patakatifu petu na kupiga mapicha na mtu wetu, huku mapicha mengine ni very compromising positions, huku hakuna taarifa yoyote kutoka popote, linakuja kufanya nini au kwa issue gani!, na siku linaondoka, linamwaga minoti ya dala 💯 💯 airport nzima!, wafanyakazi wa eapoti wanapanga foleni kupokea bakhashish. Watu wa type hii wasikaribie kabisa lango la patakatifu petu.
Video hii inasisitiza kuwa utulivu wa nchi unategemea sana utulivu na usalama wa Rais [00:30]. Ukimtikisa rais ni umeitikisa nchi!
What does this mean
Rais Samia ni binadamu, ana mapungufu yake, tunapaswa kumuomba Mungu amsaidie na kuisaidia nchi yetu.
My Take,
Japo Makamu Rais Balozi Dr Nchimbi amewaomba viongozi wa dini ndio wamuombee Rais, mimi Pascal Mayalla nasema ni Watanzania wote Wazalendo wa ukweli wa taifa letu, Tumuombee Rais Samia.
Mungu Mbariki Rais Samia
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
Nchimbi ni MAFIA MKUBWA , NI COBRA ; NA NI MAMBA HATARI SANA . NDIYE KIPENZI CHA GODFATHER KIKWETE NA GENGE LAKE. YAANI SHETANI anaomba eti watu wa dini waombe dua ?? Umeiona wapi hii Pascal ??