Poland imewazuia walinzi wa Ramaphosa kwenda Ukraine

Poland imewazuia walinzi wa Ramaphosa kwenda Ukraine

Ingekuwa mie ndiye Ramaphosa, kabla hata sijafika SA, hao walinzi wote kazi hawana. Sasa wanalinda nzi? Rais wao akiuawa, watajibu nini? Shame! Mnazuiwaje kwa mfano?

Wametudhalilisha sana Afrika. It means hawakuzungumza wakaelewana before waanze safari? Kwa nini Poland isione kwamba huo ujumbe wa Afrika ni kwa ajili ya maslahi na usalama wa Ukraine na Ulaya nzima?

Unadhani wanazuiwa Kwa mikono,la ashaa,ni ndege ndio inanyimwa Mawasiliano
 
Anaenda kuwasuluisha wazungu,matokeo yake unabaguliwa haha,,,ngozi nyeusi hazijifunzi toka kwenye msiba wa malkia hampendwi,wapo na nyie kwakua wanataka vitu kwenu,kwanza Afrika ina matatizo kibao badala yakukaa nchini kwako ujue jinsi gani ucontrol uuzwaji holela wa madawa na risasi maana ndivyo vinawaua raia wengi wa South Africa eti unaenda kuzurula nchi za walioamua kuharibu nchi zao wenyewe smh!
 
Unadhani wanazuiwa Kwa mikono,la ashaa,ni ndege ndio inanyimwa Mawasiliano
Huo ndio ushamba wenyewe, mkuu. Mimi nikajua walikwidwa, then wakapigwa mitama, mihindi na michina! Kumbe walitishwa kwa maneno tu?

Walitakiwa kutumia nguvu kama ambavyo gaidi Marekani alitumia nguvu kuingia anga ya wenyewe kwenye Kisiwa cha Taiwan, Mchina akamsamehe bure hadi hapo baadaye.
 
Walinzi 100 ni wengi sana, huenda Poland wamehisi kuna wabeba unga miongoni mwao. Africa Kusini limekuwa taifa la hovyo sana.
Akili na mawazo haya ni aibu kwa Waafrika na uafrika achilia mbali ubantu.

Ni jitu jeusi ila software sio yenyewe
Aibu
 
Mzozo wa kidiplomasia umeibuka baina ya nchi ya Poland na Afrika Kusini kwa kile kinachodaiwa ubaguzi wa rangi na mkuu wa kitengo cha ulinzi wa Rais Ramaphosa.

Kundi la walinzi zaidi ya 100 wa Rais Ramaphosa wakiwa kwenye ndege ya shirika la SAA wamezuliwa isivyotarajiwa na Mamlaka za Poland kuendelea na safari.

"...wametuzuia hapa hakika wanahatarisha usalama wa Rais ( Ramaphosa). Nataka muone walivyo wabaguzi wa rangi!"

Ramaphosa yupo Ukraine bila ulinzi mahsusi.

BBC
Walinzi mia moja wa nini, hao wakae hapo mwisho wa siku warudi nyumbani. Hakuna mwenye nia ovu na Ramaphosa.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Toka kule asee! Russia hajawahi kununua wala kuazima silaha kutoka kokote. Wake up! Anachofanya yeye ni kujenga na kuimarisha urafiki na mataifa mbalimbali ambayo Marekani amewatisha muda mrefu.

Anatumia muda huo ku-test mitambo na silaha za nchi husika, then washamba wanadai kwamba ameuziwa au amepewa msaada.
Drones za Shaheed zinatoka wapi?

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Wewe umepimaje hilo?
Toka apogee Urais, uchumi wa SA haujawahi kukua zaidi ya 2%,unemployment rate almost 38%,crime rate hasa mauaji, scams, yameongezeka mno, uhusiano wake na nchi za kiafrika umeathirika mno, SA inayumba mno kibiashara including AGOA ,zar against top currencies duniani ipo kwenye free falling
 
Back
Top Bottom