Ahaaaa mme wa mtu sumu, nimekumbuka mdada alofiwa na sponsor. Alilia kwa uchungu alitinga msibani na timu yake mzima, mara gari la vinywaji na likafika, michele na mazagazaga kama yote.
Msibani watu wote macho kwa yule dada.sijawahi ona dada mwenye msimamo kama ule.
Alikuwa ni mchepuko ila wanaukoo wengi walikuwa wakimjua.
Yaan raha ya sponsor awe na hela, maana mchepuko ule ulitia pesa kila kitu chenye kasoro kilirekebishwa pale pale.
Marafiki wa marehemu nao walimpa nguvu mchepuko. Mafundi wa kujenga kaburi wakaletwa wapya. Watu wote walishika mdomo.
Mke mkubwa kimyaa hakusema chochote. Ile timu ta mchepuko na sare zao sasa mmmh.!!!!!!
Ni miezi 7 tangu mme wa mchepuko afe ila kila weekend mchepuko anaenda nyumbani kwa marehemu anasafisha kaburi, anapulizia perfume,maua na anaondoka.
Pesa ina nguvu nyie!!!!
Sema yeye hakuleta fujo.aligharamikia nsiba wote.kila kitu.