Pole Prof. Adolf Mkenda kwa ugumu wa mazingira ya kazi

😂😂😂😂😂😂
 
Kwa nchi kama Tanzania unatakiwa ugeuke shawa moja kwa moja ili ule mema mm ningekuwa ndio waziri wa elimu bwana mkenda sifanyi kitu kila kitu namuuliza kwanza naibu wangu na tena namuita kabisa mwanangu.
😂😂😂😂😂
 
Kazi mojawapo ya waziri au naibu, ni kutunga falsafa inayoongoza wizara na Taifa kwa ujumla.
Sasa mtu ukiwa na elimu ya hapa na pale utatunga falsafa gani ya maana?.
 
Kwani huyo waziri, zaidi ya kulalamika lalamikia, ameifanyia nini cha maana hiyo wizara
 
Kwa nchi kama Tanzania unatakiwa ugeuke shawa moja kwa moja ili ule mema mm ningekuwa ndio waziri wa elimu bwana mkenda sifanyi kitu kila kitu namuuliza kwanza naibu wangu na tena namuita kabisa mwanangu.
Daaah🤣🤣🤣🤣..yani unajifanya huelewi lolote na kwamba miongozo yote unapewa na naibu 🤣🤣
 
Elimu ya hapa na pale ndo ikoje yaani??

Unafeli la saba, unaenda shule ya kulipia, unafeli form two, unarudia form two. Tia maji, tia maji unaunga mpaka form four, unapata division four ya 26, D na F kibao, unaambulia ka credit kamoja au tuwili, unaenda kutafuta credit ya tatu, ili uende forms six. Unapata ka credit hapo hapo hapo unapiga pepa la form six, unapata division three ya pointi 13. Unaomba vyuo unakosa, au unapata kwa mbinde sana.

Unamaliza chuo unapata ka GPA ka 2.9, unatafutiwa mchongo, unapata kibarua chako kwa nguvu ya wazee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…