Pole Sana Mama Janeth Magufuli pokea upendo na faraja ya umma wa Watanzania hata milele

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
36,197
Reaction score
29,717
Hawa ndio wanadamu!

Kipenzi chako na baba wa familia alikesha na mafaili wizarani na baadae ikulu na pengine aliwasahau kama wanafamilia kutokana na kujitoa kwake kama sadaka ya watanzania!

Hakika usifadhaike ,usilie,usijute bali muombe Mungu sana.

Wanadamu wabaya ndivyo walivyo...hawapendi anayefanikiwa haswa aliyeanzia katika magumu.

Piga konde moyo ...umma uliopata maji,barabara,vituo vya huduma vya afya na wanyonge wote waliopata ahueni wataombea baraka roho ya marehemu ipumzike kwa amani ya milele.

Usilipe ubaya kwa ubaya bali endeleza wema wa baba yetu aliyetangulia.

Tuliokunywa maji salama huku vijijini na tuliopata barabara ya kufika hospitali kwa wakati na tukakuta vifaa vya matibabu kamwe hatuwezi kusahau na kuacha kusali na kumuombea mema THE LATE ,THE LEGEND JOHN POMBE MAGUFULI.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
..msiwasahau Ben Saanane, Azory Gwanda, na wengine waliopotezwa ktk awamu ya 5.

..Magufuli died naturally, lakini hao wengine wamedhulumiwa uhai wao.
Hivi tukiamua kufikiri kwa muktadha wa kitabu ina maana kabendera alipanga kisasi dhidi ya Magufuli??Je alifikia hatua ipi ya kisasi??nani yupo nyuma yake kwenye kisasi??nani alimuwezesha kulipa kisasi??
Hapa narudi kwenye msemo wetu muhimu...tumuachie Mungu!!
 
..kwanini tumuachie Mungu? Haki lazima itendeke.

..uchunguzi wa haki, na kweli, ufanyike tujue nini kilichojiri watu wasio na hatia wakapotea.

..kibinadamu ulipaswa kuwa na uchungu na huruma zaidi kwa mama yake Ben Saanane, Azory Gwanda, Akwilina, na wengine waliodhulumiwa uhai wao.
 
mwandishi huyu kama anao ukweli alipaswa kuufikisha kwa familia za Azory na Saanane...hiyo ndio huruma ya kweli
 
..kwanini tumuachie Mungu? Haki lazima itendeke.

..uchunguzi wa haki, na kweli, ufanyike tujue nini kilichojiri watu wasio na hatia wakapotea.

..kibinadamu ulipaswa kuwa na uchungu na huruma zaidi kwa mama yake Ben Saanane, Azory Gwanda, Akwilina, na wengine waliodhulumiwa uhai wao.
Huna huruma kwa familia ya Magufuli na pia huna huruma kwa Taifa linapohujumiwa na mabeberu wakiwatumia vibaraka wao kama kabendera
 
kuna kikundi ovu mtandaoni kinaratibu mapandikizi ya chuki kwa watanzania

kila kukicha kimekua kikitoa mada na michango isiyo na heshima kwa viongozi wa nchi
 
Hawa ndio wanadamu!

Kipenzi chako na baba wa familia alikesha na mafaili wizarani na baadae ikulu na pengine aliwasahau kama wanafamilia kutokana na kujitoa kwake kama sadaka ya watanzania!

Hakika usifadhaike ,usilie,usijute bali muombe Mungu sana.

Wanadamu wabaya ndivyo walivyo...hawapendi anayefanikiwa haswa aliyeanzia katika magumu.

Piga konde moyo ...umma uliopata maji,barabara,vituo vya huduma vya afya na wanyonge wote waliopata ahueni wataombea baraka roho ya marehemu ipumzike kwa amani ya milele.

Usilipe ubaya kwa ubaya bali endeleza wema wa baba yetu aliyetangulia.

Tuliokunywa maji salama huku vijijini na tuliopata barabara ya kufika hospitali kwa wakati na tukakuta vifaa vya matibabu kamwe hatuwezi kusahau na kuacha kusali na kumuombea mema THE LATE ,THE LEGEND JOHN POMBE MAGUFULI.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
Naunga mkono hoja Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani
P
 
Hivi mbona utekaji na mauaji ya wapinzani hayajakoma hata baada ya JPM kufariki?

..Tulipinga utekaji, na mauaji, wakati wa Magufuli.

..Tunapinga utekaji, na mauaji, wakati wa Samia.

..Ndio maana tunasisitiza iundwe Tume Huru kuchunguza nini kilitokea, na nani alihusika.

..Tusipofanya hivyo wahusika watajisikia wako huru kufanya udhalimu wao.

..TANZANIA ISIYO NA UKATILI WA VYOMBO VYA DOLA INAWEZEKANA.
 
Back
Top Bottom