Pole sana mtani, ila iga busara za Uamsho walipoachiwa huru

Pole sana mtani, ila iga busara za Uamsho walipoachiwa huru

Kama alivyokuwa anafanya jiwe
Huyu ni mwanasiasa, kwahiyo kila jambo lazima alipeleke kisiasa. Anatumia kifungo chake kama njia ya kuwarubuni watu ili aongeze wanachama zaidi, na muda sio mrefu ataanza kuomba michango ya chama ili aende zake Dubai akapumzishe akili na familia yake, huku akiwaacha wachangaji wakilia kuhusu ugumu wa maisha nk. Jamaa anajua kucheza na akili za watu, ndio maana amefanikiwa kukusanya akili za mamilioni ya wafuasi wake na kutembea nazo mfukoni kwake.

Sent from my SM-J400F using JamiiForums mobile app
 
Kama siasa za kina jiwe, bashiru na polepole
Ushauri mzuri sana ila Mbowe asivyokuwa na hekima nakuhakikishia atarudi jela. Hata yeye angekuwa na serikali wala asingekubali drama na tena yeye angekuwa muuaji na mfunga watu midomo maana kama tu uenyekiti hataki kuachia na kila mwenye dalili za kuonesha anamuua, je angepewa mamlaka?

Nadhani kizazi cha mbowe inapindi kiondoke kwenye siasa kije kizazi kingine chenye kuendesha siasa za kimkakati na kuheshimu utu wa mtanzania

Sent from my SM-J400F using JamiiForums mobile app
 
Miezi 8 si haba. Lakini wako UAMSHO walikaa miaka 9. Kwa hiyo kama kuumia mtani hujawafikia UAMSHO.

Ningefurahi ukawaiga UAMSHO. Hakika wameonesha hekima kubwa toka waachiwe huru. Wamejirudi.

La muhimu ni namna walivyo "behave" walipoachiliwa. Hatukuwasikia wakituambia unayotuambia mtani. Unafikia hata kumuudhi aliyekusamehe! Kwamba hakuna aliyekuhurumia bali umetoka kwa nguvu ya umma? Really? Ipi? Ni nguvu ipi ya umma unafanya kazi kwenye kutoa watu jela lakini inashindwa kuzuia watu wasiende jela? Mtaniii?

Mtani ushakuwa mtu mzima na uzee ushabisha hodi. Haipendezi kila siku uwe wa vituo vya polisi, jela na mahakamani ! Mtani kuna marafiki wa kweli na kuna wapambe! Hebu tusikilize marafiki wa kweli.

Achana na siasa fanya biashara. Na kama siasa ndio biashara yako basi acha siasa za kibabe. Hazilipi kwa kuwa sifa ya ubabe ni sifa ya serikali zoote duniani. Hakuna chombo au mtu anaweza kuwa mbabe kuliko serikali.

Dai chochote kwa kistaarabu utaeleweka. Serikali kuiambia hupoi, mpaka kieleweke, una kiberiti, utafanya nchi iwe Libya, n. k. haifai. Serikali ina uwezo wa kufanya hicho kibiriti kikuchome mwenyewe! Serikali ina uwezo wa kufanya wéwé peke yako uishi kama uko Libya!

Mtani hakuna sifa ya mtu kutembelewa na watu wengi gerezani, Sawa na mgonjwa ajisifie kutembelewa na watu wengi kitandani akiwa wodini It's an illusion! Haimfanyi awe mgonjwa bora kuliko wagonjwa wengine!

Mtani miaka inasonga hairudi nyuma. Na ukweli ni kuwa bado hauna hiyo "nguvu ya umma". Wenye nguvu ya umma hawakamatwi usiku, wakasafirishwa usiku, wakakaa ndani miezi 8 Huku wenzake wanachomudu ni kuvaa t-shirt zenye hukumu!

Sikupenda walichofanya UAMSHO lakini nimependa busara zao baada ya kuachiwa. Ukiziiga utakuwa salama. Ukifuata wapambe basi utatembelewa tena jela. Na hao wapambe watalala na kula makwao wewe ukilia njaa. Jela hakujawahi kuwa kuzuri hivyo sio mahali pakupenda kwenda.

Wenzako wanaokupa moyo Mtani kina Godbless Lema na Tundu Lissu wapo ughaibuni wanakula maisha na kuendesha shughuli zao huku wakilipwa madola kila mwezi. Usiwe mjinga, jua limezama shtuka!

Umelia kwa uchungu sana Mtani kila uliposimulia miezi yako 8 jela, itoshe kusema imekufunza. Ogopa mwanaume kulia kwa kiwango kile tena mbele ya umati akiwa na mke wake kando yake.

Anyway, akili ni nywele!
View attachment 2144111
Nguvu ya uma si tu watu kuandamana mitaani, serikali ilipata shinikizo kubwa zaidi ya maandamano ya machinga ambayo yangezimwa kwa virungu na washa washa.
 
Dah Chacha Wangwe kadhulumiwa uhai wake kama masihara. Kitendo cha kujaribu kum beep bwana mkubwa kimeyagharimu maisha yake na familia yake. RIP Chacha Wangwe Mungu ataendelea kuwanyima amani wote waliohusika na dhulma ya maisha yako.

Inakuwaje serikali na polisi wake wanaendelea kucheka na muuaji wa Wangwe? Nao wameamua kumuachia Mungu?
 
Bosi Mbowe kesi bado anayo. Yaani ni kama ilivyokuwa kwa Sabaya tu. Sabaya walivyomuachia akasema ataitisha presa conference aseme yote, mhhhh nikajisemea moyoni huyu kaisha. Sasa mshaurini huyu Mwenyekiti wenu wa kikundi cha ngo ajitafakari

Fact ni serikali iliogopa kuendelea kuaibika na kesi iliyoitunga kijinga Rais akaamua kuifutilia mbali na kumuita Mbowe Ikulu “kuweka mambo sawa”. Hiyo kesi ndiyo imeisha. Hakuna mwenye akili anayeweza kuirejea. Ni aibu.

Mbowe ni level nyingine. Kumlinganisha na Sabaya ni kujipa maumivu yasiyo na sababu.
 
Ana haki ya kuongea yote na kuwashukuru wote walionyesha utu kwake ni haki yake. Yule asiye na shukrani kwa walionyesha utu wakati wa shida huyo ni sawa na punda tu. Ni shetani tu anayefurahia shida ya mtu mwingine
Mbona kama umemtukana Mudawote
 
Hilo ni sikio la kufa huwa halisikii dawa kamwe. Pia umeongea jambo la msingi kukaa jela sio sifa wala sio ujanja sababu kunyimwa uhuru sio jambo la kujivunia sababu hapo mahakamani akina kibatala wanatokwa jasho kukutetea muda ukiisha we unarudi lupango kwa kalandinga na kwenda kula dona maharage wenzio wanapanda VX wanaenda kula vyuku.

Wanatoka out na familia zao,usiku wana gegeda kwenye vitanda vizuri wakati we saa kumi jioni ushaingizwa kulala selo halafu mtu anajiona mjanja na pia umesomewa mashitaka na kukutwa na kosa la kujibu bado ataona mzaha ngoja akutane na ving'ang'anizi mtaani utapasikia siku unatoka utakuta Dar inafanana na Newyork City.
Kwa mawazo haya na akili hizi nakushauri ujiunge ccm mkuu
 
Uamsho baada ya kuachiwa waliitwa ikulu?
Miezi 8 si haba. Lakini wako UAMSHO walikaa miaka 9. Kwa hiyo kama kuumia mtani hujawafikia UAMSHO.

Ningefurahi ukawaiga UAMSHO. Hakika wameonesha hekima kubwa toka waachiwe huru. Wamejirudi.

La muhimu ni namna walivyo "behave" walipoachiliwa. Hatukuwasikia wakituambia unayotuambia mtani. Unafikia hata kumuudhi aliyekusamehe! Kwamba hakuna aliyekuhurumia bali umetoka kwa nguvu ya umma? Really? Ipi? Ni nguvu ipi ya umma unafanya kazi kwenye kutoa watu jela lakini inashindwa kuzuia watu wasiende jela? Mtaniii?

Mtani ushakuwa mtu mzima na uzee ushabisha hodi. Haipendezi kila siku uwe wa vituo vya polisi, jela na mahakamani ! Mtani kuna marafiki wa kweli na kuna wapambe! Hebu tusikilize marafiki wa kweli.

Achana na siasa fanya biashara. Na kama siasa ndio biashara yako basi acha siasa za kibabe. Hazilipi kwa kuwa sifa ya ubabe ni sifa ya serikali zoote duniani. Hakuna chombo au mtu anaweza kuwa mbabe kuliko serikali.

Dai chochote kwa kistaarabu utaeleweka. Serikali kuiambia hupoi, mpaka kieleweke, una kiberiti, utafanya nchi iwe Libya, n. k. haifai. Serikali ina uwezo wa kufanya hicho kibiriti kikuchome mwenyewe! Serikali ina uwezo wa kufanya wéwé peke yako uishi kama uko Libya!

Mtani hakuna sifa ya mtu kutembelewa na watu wengi gerezani, Sawa na mgonjwa ajisifie kutembelewa na watu wengi kitandani akiwa wodini It's an illusion! Haimfanyi awe mgonjwa bora kuliko wagonjwa wengine!

Mtani miaka inasonga hairudi nyuma. Na ukweli ni kuwa bado hauna hiyo "nguvu ya umma". Wenye nguvu ya umma hawakamatwi usiku, wakasafirishwa usiku, wakakaa ndani miezi 8 Huku wenzake wanachomudu ni kuvaa t-shirt zenye hukumu!

Sikupenda walichofanya UAMSHO lakini nimependa busara zao baada ya kuachiwa. Ukiziiga utakuwa salama. Ukifuata wapambe basi utatembelewa tena jela. Na hao wapambe watalala na kula makwao wewe ukilia njaa. Jela hakujawahi kuwa kuzuri hivyo sio mahali pakupenda kwenda.

Wenzako wanaokupa moyo Mtani kina Godbless Lema na Tundu Lissu wapo ughaibuni wanakula maisha na kuendesha shughuli zao huku wakilipwa madola kila mwezi. Usiwe mjinga, jua limezama shtuka!

Umelia kwa uchungu sana Mtani kila uliposimulia miezi yako 8 jela, itoshe kusema imekufunza. Ogopa mwanaume kulia kwa kiwango kile tena mbele ya umati akiwa na mke wake kando yake.

Anyway, akili ni nywele!
View attachment 2144111
 
Bosi Mbowe kesi bado anayo. Yaani ni kama ilivyokuwa kwa Sabaya tu. Sabaya walivyomuachia akasema ataitisha presa conference aseme yote, mhhhh nikajisemea moyoni huyu kaisha. Sasa mshaurini huyu Mwenyekiti wenu wa kikundi cha ngo ajitafakari
Mungu angeumba mtanzania tu duniani hii dunia ingenuka Mavi maana hata akili ya kuchimba choo isingepatikana. Mbowe anyamanze ili aabudu watesi? Watu mnawaonea na bado mnataka wanyamaze. Hata Lisu mlipompiga risasi mkataka anyamaze aabudu watesi wake. Kuna watu muelewe Mungu kawaumba na hawataabudu binadamu kamwe. Wewe uliyezoea kuabudu watu endelea na usitake wengine waabudu watu Kama wewe.
 
Mleta mada Uamsho sio viongozi wa chama cha Siasa kama Mbowe.
Suala la Mbowe kurudi tena jela sio issue maana kwenye moyo wake "nothing to loose"
Usimfundishe uoga kama kwako uoga ndio Kinga yako ya kubaki uraiani na kuishi vyema waachie na wengine waamue namna wanavyotaka kuishi.
 
Back
Top Bottom