Pole sana mtani, ila iga busara za Uamsho walipoachiwa huru


Unafahamu maana ya nguvu ya umma?. Mbowe ametetewa kuanzia vyama vya siasa, Viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla. Hakuna aliyemtoa Mbowe zaidi ya nguvu ya Umma. Maana kila mmoja aliona uonevu aliofanyiwa.

Halafu huna uhalali wa kumshauri Mh Mbowe maana wakati anapitia kadhia hiyo wewe binafsi ulimuita Gaidi.
 

Naomba nikueleweshe, Mh Mbowe alikuwa Rumande sio kifungoni. Alikuwa Rumande maana kesi yake ilikuwa haina dhamana.
 

Kizazi chako ndio kinatakiwa kuondoka. Unapangiaje watu nini cha kuongea na nini sio cha kuongea. Wewe ukipangiwa Cha kusema utakubali?.

Kama udikteta upo ccm, juzi tu hapa Speaker Ndugai katoa maoni yake mkamshambulia hadi akaomba msamaha. Pamoja na kuomba msamaha hamkumsamehe mpaka akajiuzuru.
Ilifikia kipindi hata kujua hali ya afya ya Rais Ni kosa la jinai.

Pia, usitumie jela Kama tishio la kupokonya haki ya mtu ya kuongea. Mh Mbowe alikuwa tayari kujitetea ndipo nolle prosequi ya kufuta kesi ikaja. Kama Mbowe alikuwa tayari kujitetea na alikuwa na mashahidi wengi, iweje umtishie kwamba utamrudisha jela?.

Halafu kesi haindelei maana imefutwa Bali inaanza upya, trial de novo.
 

Please heshimu familia ya Mbowe, usifanye siasa ikakuondolea upendo na uhalisia. Kuna maisha baada ya siasa. Nani amekwambia Mh Mbowe anashida ya pesa?. Kama angekuwa na shida ya pesa asingefungiwa akaunti zake na pesa kuchukuliwa.

Let's change, don't let politics create hatred in you.
 
Eti tufanye nchi isitawalike. Wee..!! Unaijua dola wewe!!??? Saivi hali shwari sijaona anayeweza kuleta fyokofyoko..!!
 
Naomba nikueleweshe, Mh Mbowe alikuwa Rumande sio kifungoni. Alikuwa Rumande maana kesi yake ilikuwa haina dhamana.
Ndio maana tunapiga kelele kufumuliwa mfumo wa elimu yetu unakuta huyu ni form 4/6 ila anakosa uelewa was mambo ya kawaida kama haya , halafu wenyewe wanaona wanajua yote, hata pale wanapoelimishwa hawataki.
 
Soma vizuri nilichoandika. Inawezekana vipi uchukue hela umpe mtu akale bata na familia yake, afu wewe urudi kwako ukilia njaa. Kwanini hizo hela ulizomchangia mtu usizitumie kwa biashara au mambo mengine ya kimaisha!

Mbona serikali ya CCM imeibia watanzania pesa nyingi kwa ufisadi na bado unaishabikia?. Richmond, Dowans, EPA, Kagoda, Twin Towers, Rada ya Uingereza na Sasa pesa za uviko na tozo. Tofautisha michango wa hiari na ufisadi kwenye tozo au pesa za uviko ambazo Ni less za wananchi wote.
 
Eti tufanye nchi isitawalike. Wee..!! Unaijua dola wewe!!??? Saivi hali shwari sijaona anayeweza kuleta fyokofyoko..!!
لا تعاند من إذا قال فعل

Usimbishie yule anaposema hufanya



Tuishi humo tutafurahia maisha
 
Dah Chacha Wangwe kadhulumiwa uhai wake kama masihara. Kitendo cha kujaribu kum beep bwana mkubwa kimeyagharimu maisha yake na familia yake. RIP Chacha Wangwe Mungu ataendelea kuwanyima amani wote waliohusika na dhulma ya maisha yako.

Chacha wangwe kamalizwa na serikali ya CCM . Hivi unajua yupo wapi yule kijana waliye kuwa naye ndani ya gari? Uliwahi kumsikia Tena baada ya kuachiwa kwa msamaha wa Rais kikwete?. Tatizo tuna macho lakini tunajifanya vipofu.
 
Wapumbavu kama wewe nchi hii bado ni wengi! Wacha wenzako wapiganie haki wewe baki kulamba nyayo za hao unaowaabudu!
 

Mchakato gani CCM walianzisha?. Mchakato wa katiba mpya umeanzishwa na upinzani sio CCM kuanzia mwaka 1992, mpka ulipopata nguvu mwaka 2011, kwa makongamano pale UDSM. Ndipo Rais kikwete alipokubali na kuteua time ya Warioba. Ila CCM hao hao ndio wakaja wakauharibu mchakato mzima mpaka leo hatuna katiba mpya hata rasimu yao ya change wameitupa.
 

Punguza dharau mkuu. Usiongee kana kwamba hii dunia umeimaliza. Kosa la Mh Mbowe ni lipi? Kubambikiwa kesi na kuwekwa mahabusu?. Yani ulitaka Mbowe asiseme chochote akae kimya?.

Dunia Ni mzunguko, kuna watu walijiona wanaimiliki Tanzania lakini siku yao ya taabu walikuwa wanaomba msaada hakuna wa kuwasaidia na wakafa kifo Cha Siri. Tuheshimiane Kama watanzania sio kwa vyama.
 
Huu Ushauri haufai Kabisa..., Mimi ni Muumini wa watu wenye Misimamo na wanasimamia wanachokiamini (Kukaa kimya au kufanya kile ambacho hutaki kufanya sababu ya fulani is like being dead)....;

Kwa reasoning yako watu wangeendelea hata kutokupinga Utumwa sababu ilikuwa ni mamlaka ya kipindi kile kwamba Utumwa its all good ?

Na hii italeta precedence gani ?, Kwamba ukiwa mbishi unafungwa ila ukisamehewa unaunga mkono ? (Mbona tunajenga tabia mbovu ya kutetea vitu vya ajabu) Yaani Sheria inatoka kwa mtu mmoja ? au tupo kwenye Monarchy ?

I had rather Die like a Man than live like a Coward - Tupac Shakur
 
Wote hao ni wahuni waliofurushwa kwenye mapango Yao baada ya hotuba ya kwanza ya mwamba baada ya kesi Yao mchongo dhidi yake kushindwa hivyo yamenuna.
 
Bosi Mbowe kesi bado anayo. Yaani ni kama ilivyokuwa kwa Sabaya tu. Sabaya walivyomuachia akasema ataitisha presa conference aseme yote, mhhhh nikajisemea moyoni huyu kaisha. Sasa mshaurini huyu Mwenyekiti wenu wa kikundi cha ngo ajitafakari

Wewe bado unaamini na kufurahia udikteta. Wakati huyo Rais wewe ndio unamchagua kila baada ya miaka mitano. Wewe ndio chanzo Cha mamlaka yake, lakini bado huoni thamani yako. Wewe ndio unamlisha kwa Kodi yako lakini, huwezi kuona umuhimu wako kisa mtawala ana jeshi?.

Wewe unataka watu waishi kama zombies wasihoji wala kukosoa watawala wanaoomba kura kwao kila baada ya miaka mitano. Lakini wakipewa madaraka wanapokonya Haki za waliowachagua. Kama kuzuia haki ya kuongea au kukusanyika Kama mikutano ya hadhara.
 
Mi ninachojua kulikuwa hakuna kesi, serikali ilisema Ina mashahidi zaidi ya 20.. mwisho wa siku mashahidi zaidi ya 11 wamelaza. Yaani ilikuwa ni ujinga mtupu! Hakuna mtu alimtoa Mbowe..kwa kesi ipi? Acha ujinga
 
Nadhani itakuwa kina mtu magereza anayemfanya apende kurudi huko Kila mara.
 
Mi ninachojua kulikuwa hakuna kesi, serikali ilisema Ina mashahidi zaidi ya 20.. mwisho wa siku mashahidi zaidi ya 11 wamelaza. Yaani ilikuwa ni ujinga mtupu! Hakuna mtu alimtoa Mbowe..kwa kesi ipi? Acha ujinga
Walisema 24,wakaishia 13,hapo walipatwa Hadi matumbo ya kuharisha kisa wameishiwa maneno, mbali na kubebwa hapa na pale ila matumbo ya kuvuruga hayakuwaisha mwisho wakaona yanini kuaibika , wakaona bila kushurutishwa na kwa hiyari Yao wenyewe na wakiwa na akili timamu wakaona bora wabwage manyanga kesi yao mchongo . Halafu wahuni wanakuja huku na porojo zao, nahisi Hawa ni sehemu ya wale michongo 24🏃‍♂️
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…